Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Gang Chomba

Gang Chomba

JF-Expert Member
11,293
2,000
yanga ilianzishwa mnamo mwaka 1935 na inasemekana ndo klabu kongwe na yenye mafanikio zaidi hapa nchini. klabu hii ilianzishwa na wazalendo halisi wa nchi hii waliokuwa wakiji shughulisha na uchuuzi wa nazi na samaki na muda wao wa jioni ulipofika walikuwa wakijumuika pamoja kusakata kabumbu na hapo ndipo ilizaliwa yanga.

kama hiyo haitoshi wazalendo hawa waliendelea kujikusanya kwa pamoja na kuanza mishemishe za kusaka uhuru wa nchi hii, na ndipo tarehe 9 disemba mwaka 1961 tanganyika ikapata uhuru, hivyo kama tutazungumzia uhuru wa taifa hili basi hatusiti kwa namna moja au nyingine kuitaja yanga, na kwa heshima yake inatakiwa unapoitaja yanga kama umekaa basi unatakiwa usimame.
MAFANIKIO.
yanga ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi ya bara mara nyingi zaidi, na ndio klabu inayofahamika zaidi kitaifa na kimataifa kwa sababu ndiyo klabu iliyopeperusha vizuri bendela ya taifa hili la tanzania nje ya mipaka.
na kama hiyo haitoshi yanga ndiyo klabu yenye washabiki wengi zaidi ndani na nje ya nchi, ndani ya africa na dunia kwa ujumla.

na pia yanga ndiyo klabu ya mwanzo hapa nchini au hata afrika mashariki kwa ujumla kwa kuwa na makao makuu sambamba na uwanja wa mazoezi ambao unajulikana kwa jina la Kaunda, jina la muasisi na mpigania uhuru mwengine wa taifa la zambia muheshimiwa keneth kaunda.
mfumo huu wa kuwa na makao makuu pamoja na uwanja wa mazoezi ni wa timu kubwa barani ulaya na dunia kwa ujumla.

yanga pia ndio timu ya kwanza kuwa na gazeti hapa nchini. gazeti hili linajulikana kama "Yanga imara". lilipotoka katika wiki ya kwanza liliuzwa takriban nakala 50,000 nchi nzima na baadhi ya nchi za jirani.
mfumo wa kuwa na gazeti la klabu pia umeigwa na baadhi ya klabu hapa nchini lakini unaonekana kusua sua katika mauzo na hata ukisoma nakala ya gazeti lao utakuta limejaa matangazo ya waganga tu.

yanga ndo timu pekee iliyowahi kuuza mchezaji nje ya nchi na kung'aa katika vilabu mbali mbali barani ulaya, mchezaji huyu alijulikana kama Nonda Shaaban al maarufu kama "papii".
nonda ambaye aliwahi kutamba na mashujaa hawa wa jangwani amepata kuchezea vilabu kama val profesional ya south africa, FC zuurich ya uswis, stade rennes na AS monaco zote za ufaransa, AS roma ya italia akicheza pamoja na francesco totti, blackburn ya uingereza na sasa anakipiga katika klabu ya galatasaray yenye maskani yake katika uwanja wa ali sami yen nchini uturuki.

na hapa ndipo tunapoitofautisha yanga na vilabu vingine vya soka hapa nchini ambavyo wachezaji wake huuzwa burundi, rwanda na uarabuni ambako hakuna soka la ushindani.

pia yanga ndo timu ya kwanza hapa nchini kuongozwa na rais.
pia yanga ndo timu ya kwanza kuwa na mfumo wa wanachama kuwa wana hisa wa klabu kama timu nyingi za ulaya, hivyo kumfanya kila mwanachama kuhusika kikamilifu katika mipango na malengo ya klabu, tofauti na majirani zetu ambao mfumo wao wa uongozi haueleweki na hata mishahara ya wachezaji wanalipwa kimkanda mkanda na inafika kipindi mchezaji anakaa miezi minne hajalipwa mshahara mwisho wanatimkia kucheza ligi za mchangani.

MAFANIKIO NJE YA MIPAKA.
Yanga kama yanga ndo timu pekee iliyowahi kuchukua kombe linalotambuliwa na shirikisho la soka barani afrika CAF na shirikisho la soka duniani FIFA. itakumbukwa tu yanga waliwafunga express ya uganda kwa goli 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa afrika mashariki na kati na mechi ya fainali walitakiwa wakipige na SC villa.

yanga waliwacharaza bila huruma SC Villa goli 2-1 katika uwanja wa nakivubo kwenye mechi ya fainali ya kombe lililokuwa na msisimko kipindi hicho la klabu bingwa afrika mashariki na kati na kupelekea serikali ya tanzania kutuma ndege mpaka katika uwanja wa ndege wa entebe kwenda kuwachukua waheshimiwa waliolitoa taifa kimasomaso yaani yanga.
hivyo kuweka adabu kwa waganda ambao hawawezi kuisahau yanga maishani mwao.

yanga katika mechi hiyo iliwakilishwa na:
1) steven nemes
2) mwanamtwa kihwelu
3) keneth mkapa
4) willy mtendamema
5) issa athuman
6) method mogella
7) steven mussa
8) hamis thobias gagarino
9) said mwamba kizota
10) mohamed husein chinga one
11) edibily jonas lunyamila

pia yanga walikuwa na bunduki nje kwenye benchi kama willy martin, rifat said, aboubakar salum "sure boy" david mwakalebela "MP" na wengine wengi ambao walikuwa ni miiba kwa waganda.

katika mechi hiyo mnamo dakika ya 81 beki mahili wa villa na timu ya taifa ya uganda marehemu Paul Hasule alivua jezi na kutoka nje kwa kile ambacho mwenyewe alikiri kuwa ameshindwa kumkaba winga wa yanga edibily lunyamila, lakini alilazimishwa na kocha wake kumaliza mechi kutokana na aibu iliyokuwa inawakabili.

kutokea hapo waganda walitekwa akili kutokana na kabumbu safi lililoonyeshwa na yanga na kupelekea daladala nyingi nchini humo kuandikwa majina kama "lunyamila trans" "kizota trans" au hata wengine walifuta majina ya salon zao na kuandika "gagarino hair salon" na mpaka leo hii waganda wakisikia timu kutoka tanzania inakwenda huko wanauliza "je ni yanga?".

na baada ya ushindi huo mwanamuziki nguli wa afrika marehemu kabasele yampanya al maarufu kama peppe kalle alitunga wimbo wa kuisifia timu hiyo baada ya kuonyesha dhahili kiwango cha juu na kuvutia washabiki wengi wa soka kitu ambacho hakijawahi kufanywa na klabu yoyote nyingine hapa nchini.

HISTORIA ISIYO SAHAULIKA.
mwaka 1972 katika pambano la watani wa jadi lililokuwa lifanyike katika uwanja wa taifa, watanzania walishuhudia kituko cha mwaka pale kilabu ya simba ya dar es salaam ilipoishia chang'ombe na kugeuza basi na kurudi katika mtaa wa msimbazi na kufanya timu ya yanga ya tanzania kupewa ushindi baada ya mpinzani kufyata mkia na kutokomea vichakani.

mnamo pia tarehe 13 mwezi novemba mwaka 1991 katika uwanja huo huo wa taifa timu ya yanga ya tanzania waliingia uwanjani na basi la sharuksi lililokuwa likimilikiwa na mfadhili wa yanga wa kipindi hicho marehemu abbas gulamali, timu ya soka ya simba ya dar es salaam iliweka mpira kwapani wakati wa mapumziko na kutokomea kusiko julikana.

na kauli hii ya kuweka mpira kwapani iltolewa na mtangazaji aliyekuwa anatangaza soka redio tanzania siku hiyo ndugu Charles Hillary, na magazeti kama motomoto, mfanyakazi, uhuru na mzalendo ya kipindi hicho yalipambwa na kichwa kikubwa cha habari "mgonjwa atema dawa".

na kuweka mpira huko kwapani kulifuatia vipigo mfululizo vya august 31, october 9 lakini hii iltanguliwa na kipigo cha Said Sued "Scud" cha mei 18.

baadhi ya mashujaa waliowahi kukipiga yanga miongoni mwao ni rifat said, joseph katuba, peter manyika, anwar awadh, salum kabunda "ninja", godwin aswile "baba subi" au scania, said zimbwe, thomas kipese, joseph lazaro, omar husein, costantino kimanda, sanifu lazaro "tingisha" na wengine wengi.

hili nililokupa hapo ni tone tu la maji, ila bahari ntakupa siku nyingine.
na hii ndo yanga, klabu bora kabisa hapa nchini, isiyotishwa na kelele, adhabu wala faini yoyote.
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
35,912
2,000
KILA LA KHERI TIMU YA WANANCHI DHIDI YA BIASHARA UNITED

"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"
 
M

mbingunikwetu

JF-Expert Member
6,808
2,000
Mbona uzi huu umedoda? Watani wetu kumbukeni wahenga walisema kuwa "kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi"!!!! Haiwezekani siku ya mechi muhimu ya biashara Vs Yanga halafu kila mtu anakula kona wala hakuna wa kuleta updates!!!
 
3llyEmma

3llyEmma

JF-Expert Member
4,697

Wamekata tamaa na kocha wao kasema wajipange next season.. hii imegoma
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
35,912
2,000
Zahera kuwasilisha mapendekezo ya usajili kwa uongozi Yanga

Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, uongozi wa Yanga utakutana na kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera ambapo pamoja na mambo mengine, Zahera atawasilisha mapendekezo yake ya usajili, imefahamika

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kikao hicho ni cha pili kufanyika tangu uongozi mpya uingie madarakani

Amesema kikao cha kwanza kilikuwa cha Kamati ya Utendaji ambacho kiliweka maazimio mawili, moja; kuhakikisha Yanga inashinda michezo mitatu iliyobaki na la pili linahusu usajili "Kikao chetu kilikuwa na agenda mbili, moja ni usajili ambao tutakutana na Zahera baada ya kumaliza mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting na nyingine kumaliza ligi kwa heshima," amesema "Tulivyopewa uongozi, timu ilikuwa inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo tumeweka mikakati kushinda mechi zote tatu zilizobaki na kujua hatima yetu huko mbele"

Katika kikao hicho inaelezwa Zahera atawasilisha majina ya wachezaji ambao ametaka waendelee kubaki Yanga ili kuanza mchakato wa kuhuisha mikataba kwa wale ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu

Zahera pia atawasilisha majina ya wachezaji wapya anaotaka kuwasajili

Jumamosi ya wiki hii May 18 Yanga imeandaa tukio la futari na chakula cha jioni litakalofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo kwenye tukio hilo itafanyika Harambee ya kuichangia Yanga

Wageni mbalimbali wanatarajiwa kualikwa katika Harambee hiyo wakiwemo wabunge, mashirika mbalimbali ya Serikali na binafsi, taasisi za dini na wadau wote wenye mapenzi na Yanga

Aidha siku hiyo Kamati ya Hamasa itakabidhi kwa uongozi kiasi cha fedha ambazo zimekusanywa tangu kuanzishwa kwa kampeni ya kuichangia Yanga
 
M

mshilakule

JF-Expert Member
215
250

Itapendeza kama itakuwa mikakati ya kiukweli na wasifanye siasa kwenye mpira
 
Shadeeya

Shadeeya

JF-Expert Member
35,912
2,000
Kamati ya Utendaji kwa kutumia mamlaka iliyopewa na Ibara ya 28 (1) (d) ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2010, imefanya uteuzi wa wanachama wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga.

1. Dkt Athumani Kihamia - Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

2. CPA Shija Richard Shija - Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Uteuzi huo unaanza mara moja.

Katiba hiyo imetoa mamlaka kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga kufanya uteuzi wa wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.

Uteuzi wa mjumbe mmoja aliyesalia utafanyika baadaye.
 
Forum statistics

Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom