Makoye Matale
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 6,490
- 2,104
Timu ya wananchi, Young Africans Sports Club maarufu kwa jina la 'Yanga' usiku huu inashuka uwanjani kusaka pointi 3 dhidi ya Shaba FC ya Pemba. Kwa mujibu wa Jerry Muro alipoongea na Radio One Stereo, kutakuwa na sura ngeni za wachezaji ambao hawakupata nafasi katika mechi mbili zilizotangulia. Muro amesema mabadiliko hayo yatampa fursa mwalimu kuona uwezo wa wachezaji wote alionao. Muro amedai kuwa Yanga itaendeleza dozi na huenda dozi ya leo ikawa kali zaidi.
Wasioipenda Yanga wataendelea kuiombea mabaya na kuisema vibaya, sisi wanazi tunasema, semeni vyovyote mnavyoona inafaa, Yanga inasonga mbele, nyuma mwiko.
Mungu ibariki Tanzania, ibariki Zanzibar na ibariki Yanga Afrika.
=============
=============
Matokeo ya mwisho:
Young Africans SC 1-0 Shaba FC.