You are Right BASHE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

You are Right BASHE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ExpertBroker, Apr 2, 2012.

 1. E

  ExpertBroker JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 454
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  chadema.jpg

  [h=6]Ndg zangu Kwanza Nitumie nafasi Hii Binafsi kuwapongeza Chadema kwa Ushindi Wa Arumeru Mashariki,Kiwira,Kirumba,Liziboni na Pia Cuf kwa Ushindi Wa Kata ya Tanga

  Nimeamua kufanya hivi kwa Misingi ya kidemokrasia ni wapongeze mmepewa heshima hiyo watumikieni

  Ninawapongeza Pia kwakua uchaguzi huu Kama Viongozi Wa CHAMA changu Watatumia Busara basi hili nifunzo kubwa na Nina washaukuru CDM Matokeo haya kutupa Ishara kuwa Kaskazini inaanza kupotea mikononi Kwetu,Kusini Nyanda za Juu inaanza kupotea,Kanda ya Ziwa inaanza kupotea hii ni Alarm kwa CHAMA changu umewadia wakati kwa ujumbe huu Viongozi wakuu warudi ktk Round Table kujadili upya na kutazama Kama makundi yetu yakaisaidia CHAMA

  Kwa Matokeo haya Kanda ya Ziwa Alikuwepo Samwel Sitta,Kwa Maana ya KIRUMBA,Mbeya Alikuwepo Mama Anne Kilango,kwa Maana ya Kiwira, Arumeru Alikuwepo Mzee MKAPA,Mzee Mkama,Mzee Lowasa,Ndg yangu Nape ,Liziboni Dk Nchimbi na maaneo haya yote Tumeshindwa umewadia wakati Wa KUJITAFAKARI na kujiangalia kwa kina na si kuja na majibu Kama Yale tuliokuja nayo Baada ya Uchaguzi Mkuu 2010,Tunatakiwa kuja na MAJAWABU

  Ninadhani demeokrasia imeheshimika na CCM tumekua tukisahau wajibu wetu Wa kujadili matatizo ya watu toka mwaka 2007 Mpaka sasa 2012 ,wananchi walitupa 1st Workup call 2010 hatukuamka and this is a 2nd Workup Call hatuna Budi kuwashukuru wananchi bcs Wametupa 2nd chance ya kuamka Tujitafakari UPYA

  Nimelizie kuwwapongeza CUF na CDM kwa Ushindi wao niwatakie kila la kheri Asanteni kwa kutuamsha Mara ya Pili! [​IMG][/h][h=6]Hussein Bashe Bashe

  [/h]
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyo Bashe alishiriki katika hujuma dhidi ya mtiririko wa haki ya kidemokrasia huko Arumeru. Alitumia gazeti lake la RAI kupenyeza opinion poll za uongo kuonyesha CCM ingeshinda kwa asilimia 68 -- kumbe ilikiwa ni maandalizi kwa CCM+NEC kuiba kura! kulikuwa hakuna waandishi wa RAI waliokwenda kufanya opinion poll kule. Aache unafiki.
   
 3. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bashe CCM siyo Mungu kwako,siyo mama wala baba yako.Kama unadhamira ya dhati basi jiunge na wapambanaji wa kweli kwa lengo la kulikomboa taifa kutoka kwa mafarao wa CCM!Siyo leo unasema hivi halafu kesho unawaambia wandishi wa magazeti yenu na Tbc yenu kuponda ukweli!yuko wapi Tido Muhando?eti kisa alijitahidi kutoa wigo sawa wa habari wakati wa uchaguzi 2010!Magamba hamfai kabisa!
   
 4. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  fair play; vizuri
   
 5. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  hivi ndivyo siasa zinapaswa kuendeshwa..... for every win there is a reason..for every failure the postulate holds to be true as well!
   
 6. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Huyu Bashe ni kibaraka tu wa wazee walafi wa CCM hana moral authority ya kutushauri pengine ata kutupongeza vijana tulikatika ukombozi wa hii nchi ameshiriki kutaka kuchakachua kura ARUMERU eti leo anapongeza vijana wa namna hii tunawavutia kasi itafika siku hatajuta kung'ang'ania uraia wa nchi yetu.
   
 7. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Angalau ktk vijana wa ccm ww ndo muungwana lkn umezungukwa na vijana wajinga kama akina nape,mwigulu,lusindè n.K ambao bado wanaamini ktk siasa za majitaka.Wataendelea kukiharibu chama kwa umbumbù wao wa siasa.Nape alipuuza ushauri wa wazee akina kitne etc sasa ndo atayaona mwenyewe.Ccm mnapoambiwa mmechafta wageukiéni wanaowaambia hvyo na waulizeni kwa upole wawaelèze mmechafka wapi na mfanye vp sio kuja na kauli za kejeli eti ccm itatawala milele
   
 8. i

  iMind JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kinacho imaliza ccm siyo makundi ila ni vitu viwili. Moja kushindwa kuondoa umasikini na pili ni uzee. Kwa sasa hakuna namna ya kukinusuru zaidi ya kukiondoa madarakani. .100% ya watu wote wanaovaa nguo za kijani wanafanya hivyo siyo kwa sababu ya kupenda sera bali ni kulinda maslahi.
   
 9. t

  tongi JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  BASHE IS NOT RIGHT, anachofanya hakitoki ndani ya moyo wake, alishavaa gamba, na anakula fadhila za magamba mpaka leo, huo ushauri aitane na wanamagamba wenzake wapeane pale lumumba, ukiona kijana kama bashe anakimbila ccm, basi anatafuta mteremko wa maisha tu, vijana wote wa kazi na wanaojiamini wako katika harakati za kukomboa nchi yao kupitia kambi ya upinzani inayoongozwa na cdm
   
 10. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Bashe,siasa za kistaarabu hivi ndizo zinazotakiwa . Kama utakubalianana itikadi ya chama changu,hamia chadema tufanye kazi.Chama kilichothubutu kusahau kuwasikiliza wananchi (kama ulivyosema) kwa muda wa miaka 5 (2007-2012) hakistahilimandate,kime-cease kuwa chama cha siasa

  Kama utasukumwa na uzalendo wa dhati kwa taifa letu na kama umekosa imani kabisa na chama chako(of course hakina tumaini) basi ungana na upande wa harakati,ungana na chama chenye rekodiya kusikiliza wananchi wake.Najua kwa mawazo yako haya,chama chako kitaanza kukuona adui kwani CCM hakitaki tena fikra mpya.Karibu kamanda
   
 11. n

  ngararumu JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 470
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  bravo bashe
   
 12. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pole sana Bashe najua unaumia ungependa sana kujiunga na vijana waleta mabadiriko walioko CDM, Lkn unogopa swala la uraia litaibuka upya! CCM ni kama mbwa mzee wanafanya kazi kwa mazoe na wamelewa madaraka. Si unajua ni vigumu kumfunza mbwa mzee mbinu mpya.
   
 13. k

  kbhoke Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Bashe, heshima kwako. Nakupongeza wewe pia, kwa kusema waziwazi na kutoa wito kwa Chama chako. Wakikusikia utakuwa umekisaidia Chama chako kurudi kwenye 'the right track' na kuwasaidia watanzania.
   
 14. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Uchambuzi makini toka kwa gamba aliyepo katikati ya magamba!
   
 15. maphie

  maphie Senior Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bashe kwa hili umewaambia wazee wako ukweli; lakini kama kawaida watukuambiwa ww sio mtanzania! Uje CDM na ukionyesha uadilifu tutakutambua! Mabadiliko daima
   
 16. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  M just thinking a loud....................can this be done openly kwenye inner circles??????? If so please redirect the message
   
 17. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Bashe historia, itaandikwa mioyoni mwa watu, ikiwa utafanya maamuz magum leo, ingawa kila mtu analifaham hil kuwa utapoteza utendaji katka kampun ya NHC 2006 LIMITED. wewe ni kijana mpambanaj though your in the wrong truck, mungu atasimama upande wako coz utasimamia haki, karibu M4C tulikomboe taifa letu.
   
 18. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nami nikupongeze wewe Bashe kwa kuipongeza Chadema. Unaakili sana na uwezo kisiasa lakini wenzio CCM hawakutaki. TAFAKARI CHUKUA HATUA.
   
 19. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Natofautiana nawewe kabisa, mimi sidhani kama siasa zinatakiwa ziwe za mpiga kura linda kura yako ikiwezekana hata kwa damu, hivi unajua ulinzi mkubwa wa kura na hofu ya CCM dhidi ya wananchi ndiyo vilivyopelekea matokeo yatangazwe hivyo unavyo yaona? Hivi ingekuwa vipi Wapiga kura wangepiga kura na kujiondokea?
   
 20. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kama hicho, wewe Bashe naona bado unaendelea na matusi mazito kwa watanzania, Na katika hili unaombwa kutuomba radhi.

  Ulichokifanya wewe ni kimbelembele cha kutoa kauli hii ili uonekane muungwana, au una au umebakiwa na hekima kiasi kichwani mwako na ni jitihada za kujivua jinamizi la kushindwa, wewe ulikuwa arumeru ukifanya kampeni, kama wakati wote wa kampeni na kabla ya Kampeni of course,ulikuwa haujui kwamba Watanzania hatuitaki CCM na kama ni kweli matokeo ya Arumeru ndio yamekufumbua macho kwamba CCM haitakiwi nchi hii basi wewe ni mmoja kati ya watu vilaza sana wenye lika kama lako.

  Nani kakumbia kwamba watanzania wamekasirishwa na makundi yaliyo ndani ya CCM, nani? Funguka Macho we mgeni, CCM mmeonyesha mshikamano mkubwa sana Arumeru Mashariki, Nape Niyauwe amepnda Jukwaa moja na Manywele, what a solidarity? mbona wanaarumeru hawakudanganyika.

  CCM moja au yenye makundi haihitajiki Tanzania, tena umeniudhi sana, na hapa umezidi kunithibitishia kwamba wewe sio Mtanzania, watanzania wanalilia elimu, huduma za afya, unafuu wa bei na upatikanaji wa vyakula wewe unasema wanachukizwa na mkundi.

  Kweli akutukanaye akuchagulii tusi, nashukuru kwa kuniharibia furaha yangu ya ushindi.
   
Loading...