Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,468
- 119,621
Wanaume na wanawake, let's say umetongoza au unampenda mtu yeye akakujibu 'You are not my type' au ukasikia anamwambia mtu kuwa you are not his/her type utalipokea vipi?
Mimi ninavyojua mtu akisema wewe sio type yake anamaanisha wewe si aina ya mtu ambaye angependa kuwa naye, haimaanishi amekudharau, amekushusha na kukuona una hadhi ya chini kuliko yeye kama wengi tunavyofikiria.
Kwenye mapenzi kila mtu kipo anachopenda iwe ni katika mwonekano au personality kiujumla. Wapo wanaume wanapenda chubby girls, wengine wanapenda English figure, wapo watu wanapenda mtu mchangamfu, anayeweza kufanya acheke muda wote lakini wengine wanapenda makauzu, kuona jino lake mwaka mpya hadi mwaka mpya. Kwa hiyo akikutana na wewe upo kinyume cha hapo ni kwamba wewe si type yake.
Japo si busara kumchana mtu live kuwa 'wewe si type yangu' lakini haina haja ya kukasirika, kuumia na kujenga chuki ukisikia kitu kama hicho. Maana wengine wakiambiwa hivyo wanaanza kuchambua demu mwenyewe miguu yote ya kushoto, sura kama anaramba ndimu anawezaje kutamka maneno kama hayo? Relax, kunywa maji then tafuta wa kufanana na wewe, yupo mahali anakusubiri.
Pengine kilichomfanya Diana asikupende ndio hichohicho kitakachomfanya Mwajuma asilale kwaajili yako.
Thanks