Yeyote aliye tayari kuwekeza kwenye jiko, aje tushirikiane

Omary Ndama

JF-Expert Member
Apr 16, 2017
3,367
4,056
Katika kupambana na hali zetu ajira hamna sasa tunatakiwa kujiajiri.

Kuna jiko limepatikana katika bar maarufu Mbagala na kwa uzoefu wangu jiko hilo linalipa sana. Jiko hilo limeachiwa kutokana na ugomvi binafsi baina ya meneja wa bar na wamiliki wake.

Nimekuja jukwaani hapa kuhitaji mfadhili katika biashara hiyo. Narudia tena "inalipa" na nathibitisha hilo kutokana na ninavyoijua bar hiyo ilivyokuwa ilivyo na inavyoelekea, ila tu jiko liliyumba kutokana na msimamizi kutokuwa na uzoefu na kazi hiyo.

Hivyo mwana jukwaa yeyote aliye tayari kuwekeza katika hilo namkaribisha sana kuwekeza. Tatizo kinachotusumbua vijana wa Magufuli ni mtaji. Mfadhili aliye tayari aje PM tuyajenge tupunguze tatizo la ajira nchini maana jiko lile linakamata ajira ya vijana wasiopungua kumi wenye uhakika wa kuendesha maisha yao pasipo tatizo lolote.

Nawasilisha....
 
Kazi hamna kabisa mtaani, tutakufa wakija pm nicheki na Mimi kijana mwezio tuje tupige kazi
Sawa mkuu ngoja niwasubir, ila toka Jana sijamuona mtu...na leo natakiwa nikadhibitishe jiko nalihitaji....
 
Inacost how much? Huyo Mdhamini atanufaikaje?
Ushauri andika Uzi mwingine Jitahidi heading iwe so impressive watakuja tu pm
 
Boresha vizuri tangazo mkuu ili mtu asijiulizeulize mfano inahitajika kiasi gani kufanya uwekezaji hapo, misosi gani inatakiwa, ni mbagala gani nk

Maana wengine kuja pm ni mtihani kidogo
 
Inacost how much? Huyo Mdhamini atanufaikaje?
Ushauri andika Uzi mwingine Jitahidi heading iwe so impressive watakuja tu pm
Mwenye Nia ya dhati ya kupambana na umaskini ututoke vijana atakuja tu pm apate ufafanunuzi mkuu...tatizo kubwa pale kwa tunaoelewa biashara si uchawi Bali mazingira, cost yetukubwa pale panatakiwa ukarabati wa miundo mbinu ya mazingira ya Afya ndo tatizo nililoliona pale, mazingira si rafiki kwa wanaoipenda afya yao, na itacoast si chini ya laki nne, Lkn habari njema zaidi,mmiliki wa bar ile kwa mujibu wa mkataba,alouandika hatutalipa pango kwa muda wa miezi sita....na lingine biashara pale inafanyika mpaka bidhaa zinakwisha....
 
Kila la kheri
 
Mbagala sehemu gani
 
Fursa unayo nzuri ila umeshindwa kuweka andiko lenye ushawishi..angalau ungegusia kdg kiasi kinachotakiwa kwa ujumla wake, mwenye uhitaji angepima nguvu yake.
 
mkuu mbagala wapi 400K nyingi bana tufikilie nasie wa 150k angalau tuunganike, hata kesho nakuja kwa mguu tu.
 
Mbagala purchasing power iko chini, sidhani kama bar au jiko vinalipa labda wauziane balimi na makongoro, ila siyo mbaya kujaribu
 
fafanua kila kitu hapa

weka bei na bar gani ili tutathimini biashara itakua vp kulingana na eneo
 
Mkuu hata kapicha hakuna?
Zakheem sawa lakini ni Bar gani maana zinapishana kwa thamani
unaweza kuta ina guest, wanapenda supu na Kongoro au washabiki wa Kitimoto
kabla ya PM fafanua
 
Back
Top Bottom