Ngoja nimwelimishe mtoa mada:
Mungu sio mwanadamu yaani sio mtu:
Hili swala ndio shetani anapo simama na kuwadangaya watu:
Yesu ni binadamu kama anavyo ona mtoa mada:
Hapo kale Mungu aliamua kushuka duniani ili aonge na watu wake:
Sasa anashukaje, maana akija kama alivyo dunia haiwezi kuhimili kishindo chake:
Mungu ni Roho Takatifu na sio mwili, Mungu hana mwili kama huu wetu:
Kwakuwa ni chanzo cha uhai tunamwita Roho Mtakatifu badala ya Roho Takatifu:
Yohana (Joh) 4:24
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Hivyo basi mtu wa kawaida akimwona Yesu anajua kabisa ni mtu:
Kutokana ba Biblia takatifu achaneni na Satanic Verses, Mungu mara nyingi tu alishuka duniani kwa umbo la mtu:
Aliwahi kushuka na kuongena na Ibrahimu kama mtu akiwa na Malaika wawili:
Mwanzo 18:1
Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari.
2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi,
3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako.
4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.
5 Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.
6 Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate.
7 Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa.
........
Yesu alizaliwa kwa mpangu wa Mungu ili ashuke katika mwili wake na aingee na watu wake:
Wengi watashangaa hii hoja lakini hawashangai Jini au Mzimu kuingia katika mwili wa mtu na kuongea mambo wanayopenda:
Jini anaweza ila Mungu hawezi wanavyo fikiri:
Soma hapa:
Luka 4:18
Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
28 Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo.
(Wayahudi walikasirika kwakuwa waliona amekufuru kwa hilo andiko)
.....
Baada ya kubatizwa na Yohana Mungu alishuka katika umbo la Yesu kwa mfano wa ndege Hua yaani Njiwa:
Toka siku ile Yesu akaanza kuhubiri injiri, kufufua wafu kuponya wagonjwa nk.
Tunaposema Yesu ni Mungu tunauangaliw ule muda mchache ambao Mungu alishuka katika mwili wa Yesu:
Hili jambo hata baadhi ya ndugu zake Wayahudi hawakulijua
Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.
31 Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige.
32 Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?
33 Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.
......
Ndi maana kuna wakati Yesu anaonge kama mtu:
"Naona Kiu"
Na kuna wakati anaongea kama Mungu Mwenyezi:
Mathayo 9:2
Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza,
👉Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Hivyo ndivyo ilivyo:
Anayesema Yesu ni Binadamu ni sawa: mwana wa Adam:
Ila katika Lugha ya Kinabii kutokana na Biblia huyu ndiye Yesu na alizaliwa kwa kusudi hili tu:
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele,
Mfalme wa amani.
..........
Puuzeni maneno ya Satanic Verses, hizi za juzijuzi tu:
Manabii wa Mungu walishaongea na it is the FINAL: