Yemenikuta Mwenzenu

kila siku kunaibuka mbinu mpya ya kuibiwa.
pole sana. tumejifunza kupitia yaliyokukuta.
 
Asanteni jamani, nashukuru Mungu hakunifanya kitu chochote zaidi ya kuchukua hizo pesa simu na kadi za benki ambazo napo by the time asubuhi nareport amekwisha toa hela zote kabakiza elfu kumi tu kwenye kila kadi.
Gari ilikuwa ni Verosa nyeupe namba T116 BGH nimejaribu kutrace na TRA wanasema imesajiliwa kwa jina la kampuni inaitwa African king cars ambao wao huagiza magari from abroad na kudistribute kwa dealers,wananisaidia kuangalia chasis number wajue waliziuza kwa dealer gani then dealer atasema alimuuzia nani then from there huyo mmiliki wa gari kama ndo yeye tapeli mwenyewe au si yeye atajua..nina hakika nitampata tu hata baada ya miaka mia saba na kama anasoma ajue kabisa.kwa kweli sijawahi kukasirika kama hivi loooh,nimejifunza..
 

So kwa hiyo haihusishi uchawi wala mazingaombwe
 
Kwa kuwa una police report ya kuibiwa nenda TRA kaulizie details za mwenye hiyo gari zinaweza kukusaidia kujua pa kuanzia katika kumsaka huyo tapeli. Pole sana.
 
hakuna uchawi mkuu ni namna ya kucheza na akili ya mtu tu na kuzifata hatua kwa mikini bila kupoteza mwelekeo

Thanks.........kimsingi mtu wa aina hiyo ni lazima awe na confidence na akili yenye kufikiri kwa haraka. Na labda utujuze mtu anayetapeliwa ni lazima anayemtapeli awe na details zake au anamvaa mtu yeyote anayehisi ana mkwanja?

Hebu tupe step kwa step angalau kwa ufupi inavyofanyika:
 


ni lazima awe anajiamini sana na kama amesoma haya makitu lazima awe ameyaelewa vizuri na pia awe na uwelewa wa kutosha juu ya psychology....so haihitaji mpaka uwe na uhakika mtu flani ana pesa ndio umfanyie haya makitu..kwa aliyefuzi vizuri hii kitu anaweza kuyasoma mawazo ya mtu yeyote anayekutana nae na kujua nini kinaendelea katika kichwa chake na kwa haraka akaweza hypnotize...

kikubwa n kwamba katika hili yule anayefanyiwa huwa ana submit akili yake pasip kujua kwa huyu hypnotist na hypnotist akaikontroo akili ya mtendwa huku mtendwa akiwa na ufahamu kamili katika kichwa chake...

sasa inategemeana na njia anayoitumia huyo mtu maana zipo nyingi tu mfano:

1. Influence And Persuade People(Without Them Being Aware Of It) In Everyday Situations...

2 .How To Instantly DevelopA Deep Connection With People So You Can Almost "Read" Their Minds!

3.How To Alter Anyone's StateOf Mind On The Spot And Lead Them Into A Mesmerizing Hypnotic Trance!

4,Secrets Of Getting People To Follow Your Suggestions Without Giving It A Second Thought!

5.The Key To Changing Another Person's Behavior And Getting Them To Act Now On Your Specific Commands!


na nyingine nyingi...so kila moja ya hizo hapo juu ina hatua zake za kufata kulingana na mazingira na mtu unayetaka kum-hypnotize... i
 
shit happens,lamsingi samehe na sahau maisha yasonge mbele.
 
shit happens,lamsingi samehe na sahau maisha yasonge mbele.

pole sana,kwa kweli hawa watu wanakera sana na wanarudisha nyuma maendeleo ya watu, hata mi nimejifunza not to talk with just anybody,especially strangers... unakuta mwingine from nowhere eti anakuuliza saa ngapi..!!? khaaa.. tena ukimjibu tu ndo kosa linapoanzia....
:A S cry:
 

kwenye purple kama nimekusoma vizuri huyu jamaa hana kesi ya kujibu
 
Kosa Ni ulipomsikiliza, usikae kumaikiliza mtu sentence ya pili Kama ya kwanza hukuelewa.


 
Pole sana mkuu.next time uwe makini na stragers.hii kitu ishamtoke dada mmoja mwanza.
 
Aisee pole sana, na asante kwa kuleta taarifa, wengine yasiwafikie
 
Watu wenye hasira kama wewe wanahitaji msaada wa FP.
 
Hiyo namba ya gari itakuwa ya uongo.

Wadada siku hizi wanatapeliwa sana kwa staili maana wengi wapo desperate na mambo ya mahusiano.
 
Utapeli!!

samehe tu dada!! Je ukupata utamfanya nini??

Mungu amekupa mikono na ubongo utapata tu vingine!
 
Shukuru hajakufanya kitu mbaya.We jipange upya,fedha ni matokeo.

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
mhhh mbona dunia imebadilika binadamu hatuaminiani hee jamani mimi ndo maana hata simsalimiagi wala kumsikiliza mtu nisiyemjua khaaa simwamini banadamu yeyote jamani keeleeuuuwiii poel sana kua makini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…