Ushauri: Yearning for love

MadameX

JF-Expert Member
Dec 27, 2009
7,792
3,848
Hamjambo humu ndani? Nina shostito wangu tumekuwa toka udogo na anatatizo linamuumiza kichwa ofcourse na mimi pia huwa inanikosesha raha na amenitaka ushauri.

Huyu dada yuko early 30s, Mungu amembariki kupata vishahada, good job ya kuwezesha kuisha maisha mazuri hana, matatizo ya financial, physical or mental.

Hajawahi kuwa na mahusiano na mwanamme kwa muda mrefu ya kuaminika sababu ni kuwa anakuwa anahisi kila ananiemkaribia saa zingine unaona mtu anakuwa na interest halafu anasepa.

Wako wale wanaomng'ang'ania ambao sio katika preference zake, mojawapo ikiwa waume za watu, sugar daddy's wengine wataka kulelewa. Akaamua kuwa hatapoteza muda wake yearning for love, she think at her age that it wont happen naturally.

Kitabia hana tabia za kuruka na wanaume, wao wamelelewa kidini zaidi na maadili, siyo mjeuri, I can see her as wife material lol.

Tatizo ni kwanini hajapata mwenza mpaka sasa? Siko hapa kumtafutia mtu bali ushauri. Her concern, ni kuwa biologically umri unakimbia na chances za kuwa na watoto zinazidi kupungua na kutokana na maadili aliyokulia kuzaa nje ya ndoa ni big NO.

Now, ushauri ninaoomba ili niweze kumsaidi huyu dada ni kuwa asubiri for what she want (prince charming) or take the reality the life has to offer, meaning akubali kuwa 2nd wife or atafute anayetaka kulelewa for the sake of getting babies.

Jamani sitaki PM.
 
Kama kweli kalelewa kidini na ana msimamo wa kiimani. Akimuomba Mungu ernestly akaomba msaada wa kuombewa na watu walio vizuri kiimani kisha tena akawa na patience(aache kuwakubalia kila wanaokuja bila intention ya kumuoa) atampata...
Ila dada zetu mnakosea kitu kimoja tu! hamna uwezo wa kukaa bila mahusiano, yani hata kama hayakufaidishi wewe twende kazi, sasa unakuta prince charming akukuthaminisha kwa mbali anaona uko kwenye uhusiano so anasepa zake! kisha wewe unabaki kulalamika kumbe shida ni huna subira na you are not preparing yourself for the prince charming arrival!

Sasa we unataka aje aanze kufukuzana na midume mingine ndo akuoe? Wanaume wengine hatuna hizo swaga, nakukuta na mtu nakuacha zako naenda kwa niliyepangiwa na Mungu...
 
Mwambie asifanye haraka asije akaanza kulia bure mara wanaume this, wanaume that...she'll definitely get the person she needs hata kama sio leo wala kesho..wanaume wapo tu ila its up too her to know which is the right man kwake...tell her not to forget prayers as well..
ULIKUWA WAPI BWANA HADI NIMEUMWA KWA AJILI YAKO?:welcome:
 
Wanaume wapo wengi tu atapata mwambie aache kulala ndani atoke toke aje ata huku jf
 
Mwambie asifanye haraka asije akaanza kulia bure mara wanaume this, wanaume that...she'll definitely get the person she needs hata kama sio leo wala kesho..wanaume wapo tu ila its up too her to know which is the right man kwake...tell her not to forget prayers as well..


Umeibuka from Guatanamo Bay
Mkuu hiyo jela uliyowekwa kwa sasa inabidi tuongee na mkuu wa gereza awe anakupa hata kasimu kake ka mchina usurf kidogo maana huko kupotea kunatisha
Jana karibu niweke tangazo la kukuitafuta kokote ulipo au ukionekana watoe taarifa kituo cha JF kilicho karibu
:welcome:
 
wao wamelelewa kidini zaidi na maadili, siyo mjeuri. I can see her as wife material lol. Tatizo ni kwanini hajapata mwenza mpaka sasa siko hapa kumtafutia mtu bali ushauri

Jamani sitaki pm
Mwambie aje MMU, ajinadi atapata wachumba kibao.....! alafu ndio nini kupiga biti la pm?
 
Utulivu tuu wako wengi nao wako single wanatafuta walio kama wao ili waanzishe maisha
Asiwe na wasi wasi na asiparamie maana kuparamia huko atakujapata kitu kisichoeleweka
Maana wengi watakuwa wamevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu
 
Umeibuka from Guatanamo Bay
Mkuu hiyo jela uliyowekwa kwa sasa inabidi tuongee na mkuu wa gereza awe anakupa hata kasimu kake ka mchina usurf kidogo maana huko kupotea kunatisha
Jana karibu niweke tangazo la kukuitafuta kokote ulipo au ukionekana watoe taarifa kituo cha JF kilicho karibu
:welcome:
Hahaha!! Mkuu si unajua huku Azerbaijan palivyo....nilimuona Mama Tuli mitaa jana...niko nacheki na Madame X hapa....
 
Hahaha!! Mkuu si unajua huku Azerbaijan palivyo....nilimuona Mama Tuli mitaa jana...niko nacheki na Madame X hapa....

Angalia tuu mabomu yasikipate kisimu hicho cha mchina maana tutaishia kukupoteza
Karibu sana mkuu jisikie uko sebuleni mwa JF na wanakuandalia kila jema humu ndani
 
Mwambie hata sie waume za watu ni wanaume tuu ajipende kuji-umbia mr right wake..atupokee tuu sie waume za watu tuzae nae tulee watoto...kwa umri wa 30's sioni jinsi anavyompata wa kwake peke yake zaidi ya mume wa mtu, serengeti boys na kina mariooo... Am sorry to say that truth..but has to be told.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom