Mchezaji Yaya Toure wa Manchester City amefunguliwa mashtaka kwa kuendesha gari akiwa amezidisha kiwango cha ulevi, polisi wamethibitisha.
Polisi wamesema mchezaji huyo umri miaka 33, alikamatwa katika kitongoji kimoja cha Jiji la London akiendesha gari huku akiwa na ulevi ulio juu zaidi inavyoruhusiwa na sheria za usalama barabarani.
Alikamatwa siku ya Jumanne iliyopita akiwa anaendesha gari na kuachiwa kwa dhamana. Anatazamiwa kusimama kizimbani kujibu mashtaka hayo tarehe 13 Desemba 2016 ktk mahakama ya hakimu mkazi wa Barkingside.
Mchezaji huyo alicheza katika mechi ya Manchester City na Chelsea, Jumamosi tarehe 03 Desemba 2016 na timu yake kulazwa mabao 3 -1 na Chelsea ktk uwanja wa Etihad Stadium , mjini Manchester.
Yaya Toure alirudishwa kundini ktk timu ya Manchester City baada ya kuomba radhi mapema mwezi October 2016. Sababu ya ''kususiwa'' ni kutokana na matamshi ya kuudhi ya ajenti wake Dimitri Seluk kuhusu uongozi wa timu ya Manchester City.
Mwaka 2012, Yaya Toure alisema yeye ni muumini mzuri wa dini hivyo alikataa zawadi ya kinywaji cha Champagne baada ya kuteuliwa kuwa ''man of the match'' Yaya Toure turns down MOTM champagne on religious grounds | Daily Mail Online , sababu kubwa ikiwa ni kutokana na imani yake ya kidini.
Source: Manchester City's Yaya Toure on drink driving charge - BBC News