Mnaogopa kusema wazi wakati Rais alitamka wazi mbele ya hadhara kuwa hata yeye ana boss wake ambaye ni Msoga.
Huo ulikuwa ni ujumbe mzito kwa wananchi kuwa hana uwezo wa kuamua chochote mpaka aruhusiwe na boss wake.
Hii ina maana Msoga alimaliza miaka yake 10, halafu sahizi amemaliza miaka 4 kwa jina la mama, anataka tena 5 kupitia mama, na huenda kama atakuwa hai, atataka mingine 10 kwa jina la mwanae. Huyu ni mseveni wetu, lakini kwa kupitia majina ya watu wengine. Ndiyo maana wakati wote anawataka wale ambao anajua hawana uwezo wa kusimama wenyewe, ambao wanajua kabisa ni yeye aliyewasimika, hivyo ni lazima watakuwa watiifu kwake, na siyo kwa wapigakura.