Yaweza Kutokea TZ? (Disturbing Pictures)

Mimi napenda Amani, wote tunapenda amani. Lakini ni amani gani tunayoiongelea?? kutosikia mlio wa bunduki ndio amani tunayoimanisha kwamba ni amani?? Sasa, kuna watu katika amani yetu hii tunayoisemee kila kukicha wao ni sawa na nchi yao kuwa vitani. Angaslieni wimbi la vijana mitaani na vijiweni hawana kazi, hawajui watakula nini, hawajui kesho itakuwaje, kwao hiyo ni vita. Kwa upande wa pili, wenye nacho, wana uhakika wa kula chakula bora, watoto wao wanapata elimu bora kwenye shule bora, wanapata matibabu bora nje ya nchi, wana usafiri wa uhakika kama si wakwao binafsi kwa fedha walizoibia serikali basi wanatumia mashangngi ya serikali hawa hawataki kabisa kusikia mtu anadai haki yake, watazusha anahatarisha amani ambayo nchi yetu imeitafuta kwa muda mrefu.

Nasikitika sana, vijana wengi ni wamachinga, aidha anatoka tegeta mpaka mbagala akiwa ana viatu pea 2 au 4 na hakuna wa kununua takribani wiki nzima, sasa chakula atapata wapi, akiumwa je, atajitibia na nini. Rafiki yangu ni MAJOR WA JESHI, tuliteta kuhusu machinga kwamba wakianzisha vurugu na akatokea mwendawazimu akiwa-facilitate siraha, je tutakaa au nani wa kuwazuia? MAJOR alisema hawatafua dafu, mimi nikamkatalia na kusema hakuna wa kuwazuia. MJOR, nilimwambia, askari wetu ni wenye wapo kwenye raha, kuna kantini bia sh.800/-, kuna mchemsho na nyama choma, akimaliza kazi kuna gari la jeshi litampeleka huko aendako nyumbani, matokeo yake wameota vitambi sasa je, ukiwalinganisha na machinga ambaye atakuwa na SMG kama yao wataweza kukimbia naye kutoka tegeta mpaka mbagala?????? Machinga haya ni maisha yake ya kila siku haona tofauti kama kuna vita na hakuna vita. MUNGU atuepushie lisitokee.

Ninalotaka kusema hasa, yawezekana amani na utlivu wetu ukafikia kikomo. Shida na taabu walizonazo WTZ na hasa vijana wetu ndio hizo zitawafanya wadai haki zao. Haki haigawiwi kama keki, haki inapiganiwa na wakati mwingine mpaka damu imwagike (sitake tumwage damu) ila wezi wa mali za umma (EPA, IPTL, RICHMOND, MIKATABA HEWA) waache ili fedha wanazoiba ziwasaidie vijana (machinga) ili waweze kupata ahueni katika maisha yao vinginevyoo Buuuubuuuuuubuuuuuuu!!
 
Kwa jinsi Kikwete anavyotawala, nchi hii inaelekea huko huko kwa kasi isiyo kifani!! Ee MOLA tunusulu na balaa hili!!
 
Jmaani! Disturbing pictures!!!!!!!!!!! God save Africa...................tune elekea vapi jamani? life has no value?/////
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom