Yawaje sasa mwapeana migongo, kulikoni?

Yawaje sasa mwapeana migongo, kulikoni?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,505
Reaction score
911,249
Bedroom-02.jpg Kitchen from a distance.jpg Kitchen layout.jpg Sitting Room_1.jpg
Hicho ni kitanda chako, hakistahili kupeana migongo, lol

Mlipoanzana sisi hatukuwepo kabisa!
Mlipotongozana siye hamkutualika!
Mlipokuwa mkibipiana ilikuwa siri yenu!
Mlipokuwa mkikonyezana mlikuwa pweke!
Mlipoanzana kufukuziana hamkutujuza hata!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

Mlipowekana sawa sote mlitualika!
Mlipovalishana pete ilikuwa karamu!
Mlipovikana vilemba vya ukoka...........
Mlipotumiana posa si mliniita mshenga?
Mlipomiminiana mizawadi mbona furaha?
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

Miaka kweli haina subira, hupeperuka tu!
Miaka kweli imesonga tangia uushike ufyagio!
Miaka kweli imetupa kisogo tangia uuteme ukapera!
Miaka kweli imeishia tangia ufue na kusuuza kufuli zako!
Miaka kweli haichelei tangia uunguze kidole gumba jikoni!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

Yaelekea sasa umemchoka na humtaki tena!
Yaelekea sasa umegundua kumbe ni chongo tu!
Yaelekea sasa umetambua havielei hivi hata!
Yaelekea sasa umefumbuka macho, hakuna chenga!
Yaelekea sasa mtaani umeonjeshwa asali na manenge!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

Zile ahadi na mapochopocho kweli hukumbuki?
Kama kazeeka na wewe je ungali mbichi?
Kama hawaki je na wewe nawe wawaka?
Kama kajiachia na wewe kweli hujioni?
Mbona hivyo walakini wawaka tamaa hivyo?
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?

duh izo tenzi mkuu....emu toa kitabu kwanza wa kwanza kununua mimi

Sawa Franky ngoja nijipange........................umekiona kitanda chako nilichokubandikia hapo kwenye mada? Kweli kinastahili kupeana migongo, kweli?
 
Last edited by a moderator:
wapeeeeeeeeee wapeeeeeeeeeeeeeeeeeeee !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!hadi kieleweke wee wamwagie sera wakirudi wakutane na lecture za mwl hadi mwaka uishe wamekoma ubish na kuamua kubadilika.

safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Rutashubanyuma
 
gfsonwin Hivi kitanda kilivyo na mvuto hivyo na mandhari safi ya nyumba yao lakini hawana amani hata chembe, kulikoni?
 
gfsonwin Hivi kitanda kilivyo na mvuto hivyo na mandhari safi ya nyumba yao lakini hawana amani hata chembe, kulikoni?
Rutashubanyuma kwa muda nilioishi duniani nimekuja kuconclude kwamba akili ya mtu husikiliza zaid ushahid wa kushndwa kuliko wa kushinda na ndio sabbabisho kubwa la haya yote.

tizama hata kama mke ni mbaya ama mume lkn mtu haangalii upande wa pili ambao ni mwema bado anaangalia upande mbaya na ndo panapomwambia haya mpe mgongo lol!
 
Last edited by a moderator:
wapeeeeeeeeee wapeeeeeeeeeeeeeeeeeeee !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!hadi kieleweke wee wamwagie sera wakirudi wakutane na lecture za mwl hadi mwaka uishe wamekoma ubish na kuamua kubadilika.

safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Rutashubanyuma

Umewalenga wakina nani?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Ruta bana!!

Tuache kuwapa migongo...inawatesa............ Nyani Ngabu..........kheri alala na njaa lakini ahakikishiwe uso kwa uso............
 
Last edited by a moderator:
Umewalenga wakina nani?

Acha kumwaga Sumu saa hizi.................. gfsonwin kawalenga wanaopeana migongo tu.........kama nawe umo humu basi nd'o hivyo............
 
Last edited by a moderator:
Rutashubanyuma kwa muda nilioishi duniani nimekuja kuconclude kwamba akili ya mtu husikiliza zaid ushahid wa kushndwa kuliko wa kushinda na ndio sabbabisho kubwa la haya yote.

tizama hata kama mke ni mbaya ama mume lkn mtu haangalii upande wa pili ambao ni mwema bado anaangalia upande mbaya na ndo panapomwambia haya mpe mgongo lol!

gfsonwin ukipewa mgongo si inaumiza sana...........ehhhhhhhhhhh
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom