ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
- Thread starter
-
- #141
mi naomba niwe mpanga bajeti...halafu acheni ku2nyanyapaa bhana
sina hamu na kujuana na watu asee!!!! kuna mdada nilikutana nae humu najuta kumfahamu, hanijui simjui jf ikatukutanisha hata wiki haijaisha kishagawa na namba yangu.... tujuane tu kwa keyboard tu.
hata wanaume?
ladyfurahia nimenuna hujanitaja. kwangu mimi naona ni jambo zuri na linawezekana. Kwa yeyote anayejiona ni mwanamke regardless avatar na majina yetu anaweza kuomba kujiunga na kundi hilo. I we kama ilivyo dini na mambo ya kikubwa. Binafsi, nitakuwa tayari kukuunga mkono
Habari marafiki zangu
Natumai mko fiti na mnaendelea na shughuli,kazi na masomo yenu vyema
Leo nimeonelea nizungumze nanyi akina dada/wanawake wa humu mjengoni
kuhusu masuala yetu wanawake.
Moyoni mwangu niliwaza na kufikiri kuwa tuanzishe kitu ambacho kitatupa
umoja/ushirikiano/uhusiano wa karibu yetu na vilevile hata kutembeleana
kama itawezekana kwa wale walioko mkoa kwa mkoa,
na kupeana mambo ya baraka au huzuni pia kwani ziko ndani ya maisha
yetu ya kila siku. Kitu ambacho ningependa kuwashirikisha hususani
wanawake wenzangu, tuwe na jukwaa la akina mama au wanawake wa
jf. Mnaonaje tumshauri huyu Founder wetu atuwekee jukwaa hilo lihusulo
wanawake kama atapenda, jamani marafiki hili ni wazo langu tu ambalo
nimependa kuwashirikisha.
Hilo jukwaa tutakuwa tunazungumzia mambo mbalimbali yanayotuzunguka
yanayotupata, na vilevile tutajadili ni jinsi gani twaweza kuwasaidia wanawake
wa kitanzania katika matatizo/ misukosuko inayowakumba wanawake wenzetu
na vilevile tutajadili namna ya kumkomboa mwanamke aliyekandamizwa na
unyanyasaji toka upande wa pili. (Mfumo dume), kumpatia fursa ya kujikwamua
na kujinasua toka katika makucha hayo hususani wanawake waishio vijijini hasa.
Kitu kingine tutajadili na kupeana taratibu mbalimbali katika mambo yatuzungukayo
kama wanawake, hasa mambo mbalimbali kama ukiwa na shughuli yako unaweza
kutualika nasi tukajumuika nawe kufurahia hiyo shughuli yenyewe. mfano: ngoma,
kitcheni party, sendoff, tafrija fupi, mambo yahusuyo watoto wetu n.k. Hapo ndipo
tunafahamiana na kuleta ushirikiano na mahusiano mazuri katika yetu. Hili ni wazo
tu sijui kama wanawake wa humu mjengoni jf mtalifurahia na kulipenda na kulifanyia
kazi kama mko tayari basi msisite kufanya maamuzi na kutoa michango, ushauri na
jinsi gani twaweza kufanya haya yote kusaidiana na kuendelezana katika kuleta
maendeleo kwa mwanamke. Kama mtakuwa tayari tutawandaa viongozi wa kuongoza
kitu hichi na kuleta motisha katika majukwaa mengine. Ushauri tafadhali.
Kama mwanamke/ mdada wa jf utapenda kushirikiana nami katika hoja/wazo hili
basi usisite kuandika ushauri, kutoa maoni yako tufanyeje ili kuanzisha kitu hiki nami
nitamwomba Founder wetu, afuatilie na kulifanyia kazi kama atapenda naye.
Maoni/Ushauri wako mdada utafanya tuwe na jukwaa hili hapa jf. Naomba tuepuke
mizaha na maneno yasiyopendeza kwani hii wazo tu binafsi ambalo nimependa
kuwashirikisha nanyi kama mnapenda toeni maoni yenu hapa. TUFANYEJE KWA
JAMBO HILI(hata wewe mwanaume wa jf unaweza kutushauri ukipenda)
Copy: charminglady, sweetlady, Mamndenyi, snowhite, Paloma, Passion Lady, Zion Daughter
gfsonwin, Sean, Madame B, madame X, Preta, CUTE, na wanawake wengine waliopo
hapa jf mmu wote kwa ujumla wengine sijawashika majina yao mtanisamehe bure wapendwa.
Yani umekaaaaaaaaa then ndo umekuja na wazo hili la kijinga eh/
hebu acha upuuzi wako. sasa ukija jua mi ni dada yako na wanawake wengine humu ni nduguzo tu si utachoka ukizingatia michango yao hapa JF.
hili wazo halitekelezeki
ni zuri lakini mtawezaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa:A S 39:
asante ubarikiwe nashukuru sana ila jua kuwa linatekelezeka kwani tumeshaanza mchakato na wenye mji huu, kwa hiyo kauli yako imeshindwa na imelegea kwa jina la Bwana Mungu ila ubarikiwe sana
sina hamu na kujuana na watu asee!!!! kuna mdada nilikutana nae humu najuta kumfahamu, hanijui simjui jf ikatukutanisha hata wiki haijaisha kishagawa na namba yangu.... tujuane tu kwa keyboard tu.
Ni wazo zuri ila wanawake wengi tukishakutana hatupikiki chungu kimoja
Halafu naogopaje watu wengi nisio wajua manake binadamu tumetofautiana,kila mtu na tabia zake.
Labda kwa wale wanaohitaji kuanzisha waungane,kama namna ya kuunda marafiki wapya
Juzi tu tumeenda kwenye white party watu washaanza kusema walioenda ni mijimama mipashkuna?!!wakati watu tuna heshima zetu.Sasa kwa aina hii ya mitazamo itakuwa ngumu sana
Naunga mkono, na kama tunaweza kutumia fursa hii kuendeleza jamii yetu, mimi naamini wanawake tunawenza kuleta mabadiliko mengi katika jamii kama tu tukiweza shirikiana na kuhabarishana mambo yanayoendelea sehemu tofauti kupeana challenge thats all
Nimesoma post nyingi sana sana naona sisi wanawawake wenyew tunalalamika tuna matatizo kila post
Kumbe tunajijua ni kweli tuna matatizo ?
Ila mie natamfuta mmoja tu mpenda mungu .mwenye umri kidogo ili tuwe tunashauliana ..Maana kwenye maisha kuna mastress unaweza kutembea umevua nguo..watu wakasema hee FL1 amekuwa vip kumbe maswaiba tu yanatesa ..