Na ya nyumbani kwako kuwa umepanga chumba kimoja Tandale kwa mfuga mbwa yanasambazwa PM
Inahu??
Ni wazo zuri ila wanawake wengi tukishakutana hatupikiki chungu kimoja
Halafu naogopaje watu wengi nisio wajua manake binadamu tumetofautiana,kila mtu na tabia zake.
Labda kwa wale wanaohitaji kuanzisha waungane,kama namna ya kuunda marafiki wapya
nakuhakikishia hivi, yote hayo yataongelewa, unajifanyaga na kizungu chako humu kumbe kongosho mwenyewe ndio yule, khaa, umeshafika kwake sasa, ambavyo hajui kuvaa sasa, mbona anakosoaga wenzie sana kule kumbe mwenyewe ndio yule,sijui nini na nini, labda wanawake wa jf wameshushwa na bikira maria, kama ni hawa hawa wa ardhi/dunia hii, wacha wengine tubakie ki jf zaidi, mana tutajiongezea maadui wasio na lazima kabisa, wengine uvumilivu umetushinda, leo kongosho umeniropokea hovyo nimejua kesho nakupita kama ambulance inawahisha mahtuti kcmc,ukitoka hapo unaenda kuchonga umepitwa, wanawake tuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu, kisa kitu gani?
wazo ni zuri sana hata mimi nimeliafiki ila wanawake wengi hatupendani kabisa.
Kwa sababu sipendi makundi wala magurupu.
Nashukuru kwa ushauri mzuri ila itabidi kiwanza tuwe na jukwaa hapa hapa kisha mambo mengine tutayafanya pindi tutakapochagua viongozi wa kundi letu hilo hayo usemayo kweli yapo ila hatutayapa kipaumbele na tukiona kuna mwenzetu anapotoka tutarekebishana sisi wenyewe, na lingine sio kwamba nilisema tunatembeleana majumbani kwetu la hasha! hujanielewa hapo ni kwamba tutakuwa tunatafuta mahali mfano kwenye sehemu za wazi wanazokutana watu hasa wale wenye kamati za harusi huwa wanafanyaga hivyo hizo sehemu tutakuwa tukijali mambo yetu au kama kuna mmoja wetu ana nafasi kwake tutakwenda pale na ndipo patakuwa mahali pa kukutania si vinginevyo mpendwa naomba unielewe
mhm...hapa wanaume tuna kazi...wanawake wanataka kujipanga wajikomboe toka huu mfumo dume....ngoja tuwagegede mara ya mwisho maana karibuni tutambia kugegeda hakuna
Tuwaombe tu watupe jukwaa letu,tuna maswala mengi ya kuzungumzia asee ladyfurahia
Tumechoka nyanyaswa na hawa wanaume japo wengine waume zetu.........tunataka gender balance
G unapenda nini!? :majani7::majani7::majani7:
Tuzungumze ya wanawake yapi hayo?? Unyago?
Kama biashara wanamme wako far, ni bora kutojitenga nao
Yaani, tutaona senema wakigombana
Aya kipenzi, Wengine ni wenzetu humu lakini waala tusikate tamaa,wishing you the best of luck mumie.Nimeyapenda maneno yako na yamenifurahisha sana nitajadiliana nao mafounder wetu kisha wakitaka tutaliona hilo jukwaa soon as possible usijali best, ila kuna watu wengine hapa wanataka kupotoa wazo hili zuri kwetu mioyoni mwao wamejaa vitu visivyopendeza hawajanifurahisha na maoni yao ila si unajua tena mambo jf bhana nawachukulia na kuwasemehe bure acha tuendelee na mkakati huu na acha nianze kulifuatilia nitakufahamisha nitakapofikia asante best
wazo zuri mm nimelipenda, lakini je tutakuwa na makundi, mf:- wanawake wa JF Dar, wanawake wa JF moshi halafu kunakuwa na mkutano mkuu wa mwaka ndipo tunakutana wote, au Inakuwaje?
Nyamayao lile lilikuwa ni wazo tu waweza ongea chochote ukipendacho na kama wewe hauko tayari waache wenzio tufanye vitu na sio kuropoka ovyo utafikiri umewekewa morta mdomoni yakutoke yanayokutoka kila kheri katika vikundi vyako
Hahahahahaaaaa...........akikukamata!!