Yatupasa turudi kwenye Analojia

Yatupasa turudi kwenye Analojia

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Mawimbi kwenye luninga zetu si mazuri hata kidogo. Matangazo yanakwamakwama. Hayapendezi. Yanakera. Pia,wengi wetu hawapati kabisa matangazo ya luninga kwa kukosa ving'amuzi au kushindwa kulipa. Wanaachwa nyuma. Hawahabariki. Ni muda wa kurejea kwenye Analojia. Safari yetu toka Analojia hadi Dijitali haikuandaliwa vyema. Tusione haya kuifuta.
 
Mawimbi kwenye luninga zetu si mazuri hata kidogo. Matangazo yanakwamakwama. Hayapendezi. Yanakera. Pia,wengi wetu hawapati kabisa matangazo ya luninga kwa kukosa ving'amuzi au kushindwa kulipa. Wanaachwa nyuma. Hawahabariki. Ni muda wa kurejea kwenye Analojia. Safari yetu toka Analojia hadi Dijitali haikuandaliwa vyema. Tusione haya kuifuta.

Kama unatumia king'amuzi cha StarTime na kinakwama kwama, kitie shoti ya umeme, tatizo litakwisha kabisa kabisa.
 
nilitarajia serikali ingeweka deadline kwa wamiliki wa ving'amuzi kuboresha huduma...
 
Digitali aah, kumradhi, dijitali bado. Mi naona hii trial ya mfumo huu ni sawa na trial waliyopewa vijana wa 60% failure aaah, form four eti wanawatahini kwa competence based, matokeo yake daaah!
 
Mpango mzima bwana ni DSTV! Haina chenga wala Haina Kuremba!
 
Digitali yakera...tena inakera!!!
Mimi binafsi sina hamu ya kuangalia tv siku hizi coz unaweza kuwa na hamu kuangalia program fulani lakini yanazuka matatizo yafuatayo:
a) picha unaziona kama zilizovaa sura bandia au pengine kupata ajali.
b) program kwa kila dakika moja inanasa mara tano
c) program inaskrach kila baada ya nusu dakika,
d) picha inaonekana kama cd iliyorekodiwa tangua miaka ya 1940
e) picha zipo kama cd iliyotolewa kopi mara nyingi
f) Stesheni wenyewe tunazipata nne tu na pengine siku nyingine tunapata mbili
Yaaani ni balaaaa tumerudi kwenye redio
KWA MAONI YANGU TUNAIOMBA SIRI KALI KAMA WAMESHINDWA KUBORESHA DIGITAL BASI WATUREJESHEE ANALOJIA YETU ILI TUONE ZILE STATION TULIZOKUWA TUNAZIPATA.....MBONA ZILE ENZI ZA ANALOJIA TULIKUWA KAMA ULAYA TU, LAKINI LEO UTAFIKIRI TUKO VIJIJINI TENA VIJIJI VYA "THE LOST TRIBES"
 
Kama ni mwanasheria basi pata kitu cha DSTV........hutajutia........mimi ni karani na ninaenjoy DSTV.......
Mkuu Preta,mimi nazungumzia jamii kubwa zaidi.Asante kwa ushauri wako lakini.Pamoja sana!
 
Last edited by a moderator:
mawimbi kwenye luninga zetu si mazuri hata kidogo. Matangazo yanakwamakwama. Hayapendezi. Yanakera. Pia,wengi wetu hawapati kabisa matangazo ya luninga kwa kukosa ving'amuzi au kushindwa kulipa. Wanaachwa nyuma. Hawahabariki. Ni muda wa kurejea kwenye analojia. Safari yetu toka analojia hadi dijitali haikuandaliwa vyema. Tusione haya kuifuta.
acha kutumia vingamuzi vya bei rahisi tena promotio 39000 tsh tafuta vya uhakika ukishindwa jf members tutakuchangia lawyer wetu
 
Huu Mfumo wa Digitali Ni kero tupu Japo mimi binafsi Nlianza kuutumia tokea Mwaka 2008 nikiwa Na "EASY TV" Pamoja na Free to Air. Hawa "Easy TV" Wamejizatiti vizur ukilinganisha na wenzao wa StarTimes. Cha kushangaza hata hawajipromot kabisa, lakini wanawateja wengi sana. Pia wana Channels zilizoenda shule hadi TVZ ndani. Wamekosa tu SIBUKA,TBC2,CTN, CEN DTV na C2C. Ila nyinginezo zote zipo.
Kwa Ubora wa Matangazo wana uafadhali ukilinganisha na Startimes a.k.a King'amuzi cha kurusha Matangazo ya picha za Mnato kwa Staili ya SlideShow.


Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mpango mzima bwana ni DSTV! Haina chenga wala Haina Kuremba!

Ni watanzania wangapi wanauwezo wa kulipa DSTV??!!

Hawa jamaa hawabadiliki, ni jeuri...nafikiri kuna TATIZO...hasa katika utoaji wa leseni za kuruhusu USHINDANI...

Nafikiri DSTV angepata washindani MAKINI, market behaviour yake as a producer ingebadilika
 
Binafsi nipo anxious kweli kusikia habari za ZUKU...naomba mwenye ufahamu kuhusu hawa jamaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom