YATOKANAYO na taarifa za kamati mbili za makinikia ni kusaka fidia!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,181
Pamoja tunaohoji tunaitwa wasaliti lakini uhuru wetu wa kukosoa uko palepale na hapa ninautumia kikamilifu bila hata chembe ya khofu yoyote:-

1) Udhaifu mkubwa wa tathmini za kamati zote mbili ni kukadiria na dhana potofu kuwa makinikia yote kwenye makonteina kuanzia 1994 hadi leo ni sawa.

Hakuna mahakama duniani itakubaliana na ushahidi wa kuhisia. Tathmini ya hizi kamati ni porojo kwa maana ya kuwachukulia hatua wachimbaji migodi watuhumiwa kwa sababu hatuna ushahidi na hisia siyo ushahidi.

2) Acacia kukosa leseni ya biashara hata kama ni kweli lakini kusajiliwa kwenye soko la Hisa la Dar Stock Exchange kunatuweka pabaya. Pia hukumu mbali mbali za African Barrick Gold zilizotolewa hapa nchini zinathibitisha Acacia Gold mine ndiyo jina jipya badala ya African Barrick Gold. Sasa Brella au mahakama ipi maamuzi yake ni final?

Pia, kuwaruhusu kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa kwa miaka yote hii kutachukuliwa ni kampuni ilikuwa ikiendeshwa kwa jina la zamani la kampuni.

3) Taarifa hizi mbili kudhaniwa zinaweza kutumika kujadiliana ili tulipwe kodi za nyuma ambazo watumishi walioaminiwa na serikali walithibitisha takwimu zote ni sahihi. Huku ni kujitapeli wenyewe

4) Haya Makonteina yaliyokamatwa yanapaswa kuchenjuliwa ili kubaini takwimu za kweli na kuachana na makadirio ambayo hayana nafasi mbele ya vyombo vya sheria.

5) Hatua za kijinai nazo ni shughuli pevu kama tutatumia taarifa za ukadiriaji. Tukipata taarifa halisi baada ya uchenjuaji basi waliohusika kuzipika taarifa za sasa tu ndiyo wana kesi ya kujibu na wala siyo kabla ya hapo.

6) Viongozi waandamizi serikalini kuanzia mwaka 1994 hadi sasa wanaweza kuwajibishwa kwa criminal negligence kwa mikataba mibovu ambayo walishauri au hata kusaini.

7) Kama ni kweli, Acacia hawajasajiliwa uongozi mzima wa BOT, Brella, TRA, TMMA na Dar Stock Exchange unapaswa kuondolewa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.

8) Waliojilimbikizia mali wana kesi ya kujibu watueleze walizipataje?

9) Viongozi wa vyombo vya usalama waliofumbia macho haya madudu nao wajumuishwe kwenye uwajibikaji wa kijinai au criminal negligence

10) Kuwatisha wananchi kukosoa hatua za serikali huo ndiyo uzandiki na wakosoaji ndiyo wazalendo namba moja.

11) Taarifa hizi zina msaada kwa kesho yetu na siyo jana yetu

12) Mawaziri wa zamani walikuwa wakitekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri ambapo kuwatoa mhanga wao tu mahakama zitakataa

14) Hoja ya kudai tumeibiwa huku tumejiibia khalafu tudai fidia kwa tuhuma za wizi tulioshiriki kuufanya sisi wenyewe ni kujitapeli wenyewe.

Haiwezekani tupande mbigiri kesho tudai kuvuna shayiri kwa minajili ipi?

15) Kama jina la Acacia halijasajiliwa basi mmiliki halali wa migodi husika anabaki msajiliwa wa awali African Barrick Gold kwa hiyo khoja za yakuwa migodi haina mwenyewe ni njozi za abunuwasi.

16) Tatizo kubwa la huu utawala ni kuwatafuta wachawi bali siyo kujenga misingi ya utawala wa kisheria.

Yakija mambo ya maana na weledi kama kuboresha katiba hudai hawakukampeni kwenye hilo lakini ikija kwenye kufukazana na ngozi baada ya mnofu kuliwa utashangaa bila tone la aibu hujitokeza kimasomaso ati nao ni watetezi wa mustakabali wa taifa hili!

Give us a break, man! They either put up or shut up!

17) CCM wawe wa kweli haya makampuni ndiyo wafadhili wao wakubwa wa chaguzi kuanzia 1995-2015. Huwezi ukavuna ambacho hujapanda! Tumepanda dhuluma sasa tunaivuna hiyo dhuluma.

18) Uvunjaji wa seals za makonteina bila search warrant au amri ya msuluhishi ni kuvuruga ushahidi na hili kuisaidia sana Acacia.

19) Kutafuta usuluhishi kinyume na masharti ya mkataba kwa maana ya msuluhishi ni ukiukwaji wa mkataba na madhara yake ni kazi za kamati zote mbili ni batili machoni pa vyombo vya utoaji wa haki.

Ni sawa kabisa na kutwanga maji kwenye kinu na kutegemea upate makande yaliyoiva!
 
Mkuu naheshimu mawazo yako. Lakini naona yana mapungufu somewhere.

Mfano point number mbili. Kama Acacia anatumia jina la zamani..basi hana locus ya kutusumbua aondoke amuite yule aliyempa jina.

Mkuu the good news, hata wazungu wanajua hii mikataba ni ya kifisadi. I am pleased that at the end of the day kutakuwa na accountability kwa akina Chenge, Kafumu, Yona et al! I can bet my last coin. Hawa jamaa lazima jua liwawakie aiseeee...si kwa ufisadi huu. Na usisahau kwamba the same people ndo hao hao wa IPTL.

Ila huu ulikuwa ni wizi wa kiwango cha Uprofesa aisee.....Lord Have mercy!
 
Sitetei popote, niko upande wa maslahi mapana ya nchi....

Technology uliyotumia kuposti hapa mkuu, ilivumbuliwa na waliojua kuhisi e.g kwenye hesabu, assumptions zimetumika ku-derive formulae....

Kwenye sheria, wanahisi, wananakili, wanadhania, na wanaendelea kujifunza kulingana na matukio mapya.

Si mbaya tukiwa wa kwanza.....
 
Pamoja tunaohoji tunaitwa wasaliti lakini uhuru wetu wa kukosoa uko palepale na hapa ninautumia:-

1) Udhaifu mkubwa wa tathmini za kamati zote mbili ni kukadiria na dhana potofu kuwa makinikia yote kwenye makonteina kuanzia 1994 hadi leo ni sawa.

Hakuna mahakama duniani itakubaliana na ushahidi wa kuhisia. Tathmini ya hizi kamati ni porojo kwa maana ya kuwachukulia hatua wachimbaji migodi watuhumiwa kwa sababu hatuna ushahidi na hisia siyo ushahidi.

2) Acacia kukosa leseni ya biashara hata kama ni kweli lakini kusajiliwa kwenye soko la Hisa la Dar Stock Exchange kunatuweka pabaya.

Pia, kuwaruhusu kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa kwa miaka yote hii kutachukuliwa ni kampuni ilikuwa ikiendeshwa kwa jina la zamani la kampuni.

3) Taarifa hizi mbili kudhaniwa zinaweza kutumika kujadiliana ili tulipwe kodi za nyuma ambazo watumishi walioaminiwa na serikali walithibitisha takwimu zote ni sahihi. Huku ni kujitapeli wenyewe

4) Haya Makonteina yaliyokamatwa yanapaswa kuchenjuliwa ili kubaini takwimu za kweli na kuachana na makadirio ambayo hayana nafasi mbele ya vyombo vya sheria.

5) Hatua za kijinai nazo ni shughuli pevu kama tutatumia taarifa za ukadiriaji. Tukipata taarifa halisi baada ya uchenjuaji basi waliohusika kuzipika taarifa za sasa tu ndiyo wana kesi ya kujibu na wala siyo kabla ya hapo.

6) Viongozi waandamizi serikalini kuanzia mwaka 1994 hadi sasa wanaweza kuwajibishwa kwa criminal negligence kwa mikataba mibovu ambayo walishauri au hata kusaini.

7) Kama ni kweli, Acacia hawajasajiliwa uongozi mzima wa BOT, Brella, TRA, TMMA na Dar Stock Exchange unapaswa kuondolewa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.

8) Waliojilimbikizia mali wana kesi ya kujibu watueleze walizipatyetu

9) Viongozi wa vyombo vya usalama waliofumbia macho haya madudu nao wajumuishwe kwenye uwajibikaji wa kijinai au criminal negligence

10) Kuwatisha wananchi kukosoa hatua za serikali siyo uzandiki bali nao ni uzalendo.

11) Taarifa hizi zina msaada kwa kesho yetu na siyo jana yetu

12) Mawaziri wa zamani walikuwa wakitekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri ambapo kuwatoa mhanga wao tu mahakama zitakataa

Tatizo lako unajifanya kuwatetea Wazungu wkt Wazungu wenyewe wanaona wamefanya makosa ila wewe house nigga unajifanya unawajua sana, unafikiri Mzungu atakaa kimya kama anaonewa? Sasa hivi tayari Balozi zao hapa nyumbani zingeshaingilia kama kweli wangekuwa innocent kama wewe house nigga unavyojaribu kuwatetea, Bomboclat!
 
Sitetei popote, niko upande wa maslahi mapana ya nchi....

Technology uliyotumia kuposti hapa mkuu, ilivumbuliwa na waliojua kuhisi e.g kwenye hesabu, assumptions zimetumika ku-derive formulae....

Kwenye sheria, wanahisi, wananakili, wanadhania, na wanaendelea kujifunza kulingana na matukio mapya.

Si mbaya tukiwa wa kwanza.....
Maslahi "mapana" yanapelekea "kupanua" na "kadri unavyozidi kupanua ndivyo watu wanazidi kutamani"
 
Pamoja tunaohoji tunaitwa wasaliti lakini uhuru wetu wa kukosoa uko palepale na hapa ninautumia:-

1) Udhaifu mkubwa wa tathmini za kamati zote mbili ni kukadiria na dhana potofu kuwa makinikia yote kwenye makonteina kuanzia 1994 hadi leo ni sawa.
Bila kuzunguka zunguka... katu hayawezi kuwa sawa! Kwanza, makinikia ya Buzwagi yalianza kuzalishwa almost 10 years baada ya kuanza kwa Bulyanhulu!

Anyway, sitasema sana kwa sababu sijasikiliza hiyo ripoti lakini kama walichukua yale makontena 277 wakazidisha kwa miaka yote hayo uniformly basi watakuwa wame-mislead watu!!!
 
Pamoja tunaohoji tunaitwa wasaliti lakini uhuru wetu wa kukosoa uko palepale na hapa ninautumia:-

1) Udhaifu mkubwa wa tathmini za kamati zote mbili ni kukadiria na dhana potofu kuwa makinikia yote kwenye makonteina kuanzia 1994 hadi leo ni sawa.

Hakuna mahakama duniani itakubaliana na ushahidi wa kuhisia. Tathmini ya hizi kamati ni porojo kwa maana ya kuwachukulia hatua wachimbaji migodi watuhumiwa kwa sababu hatuna ushahidi na hisia siyo ushahidi.

2) Acacia kukosa leseni ya biashara hata kama ni kweli lakini kusajiliwa kwenye soko la Hisa la Dar Stock Exchange kunatuweka pabaya.

Pia, kuwaruhusu kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa kwa miaka yote hii kutachukuliwa ni kampuni ilikuwa ikiendeshwa kwa jina la zamani la kampuni.

3) Taarifa hizi mbili kudhaniwa zinaweza kutumika kujadiliana ili tulipwe kodi za nyuma ambazo watumishi walioaminiwa na serikali walithibitisha takwimu zote ni sahihi. Huku ni kujitapeli wenyewe

4) Haya Makonteina yaliyokamatwa yanapaswa kuchenjuliwa ili kubaini takwimu za kweli na kuachana na makadirio ambayo hayana nafasi mbele ya vyombo vya sheria.

5) Hatua za kijinai nazo ni shughuli pevu kama tutatumia taarifa za ukadiriaji. Tukipata taarifa halisi baada ya uchenjuaji basi waliohusika kuzipika taarifa za sasa tu ndiyo wana kesi ya kujibu na wala siyo kabla ya hapo.

6) Viongozi waandamizi serikalini kuanzia mwaka 1994 hadi sasa wanaweza kuwajibishwa kwa criminal negligence kwa mikataba mibovu ambayo walishauri au hata kusaini.

7) Kama ni kweli, Acacia hawajasajiliwa uongozi mzima wa BOT, Brella, TRA, TMMA na Dar Stock Exchange unapaswa kuondolewa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.

8) Waliojilimbikizia mali wana kesi ya kujibu watueleze walizipatyetu

9) Viongozi wa vyombo vya usalama waliofumbia macho haya madudu nao wajumuishwe kwenye uwajibikaji wa kijinai au criminal negligence

10) Kuwatisha wananchi kukosoa hatua za serikali siyo uzandiki bali nao ni uzalendo.

11) Taarifa hizi zina msaada kwa kesho yetu na siyo jana yetu

12) Mawaziri wa zamani walikuwa wakitekeleza maamuzi ya baraza la mawaziri ambapo kuwatoa mhanga wao tu mahakama zitakataa
Mkuu ninakufahamu hii si akili yako, hebu rudia taratibu uone ulicho andika...
 
Nakuombea Mh. Magufuli fanya maamuzi magumu ili Tanzania ya kesho ineemeke. Ndugu wanaokosoa hatua zinazochukuliwa si watanzania, lazima tuwe na shaka nao mimi nafarijika na uthubutu wako, wengine walipita na wakaacha, na wengine walithubutu hata kusema ni vita kubwa wakaogopa kuchukua hatua
 
Akina Karamagi watasumbuliwa tu ila mwisho wa siku wataachwa waendelee kuenjoy fedha walizotupiga . Unadhani hii haitawagusa JK na Ben Mkapa?Bahati mbaya sana JPM alishasema "waachwe wajipumzikie tu na atawalinda"

Nadhani kuliko kupoteza muda kutafuta nchawi, tuelekeze nguvu kwenye kuifumua mikataba yote ya kinyonyaji kwa kunegotiate terms mpya. Tuanze na huu wa IPTL.
 
Back
Top Bottom