The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 372
- 720
MAAZIMIO YA KAMATI KUU
Baada ya kutafakari matukio hayo na mengine, Kamati Kuu ya Chama imeazimia mambo yafuatayo;
1. Kamati Kuu inatamka kwamba kilichotokea tarehe 27 Novemba, 2024 hakukuwa na uchaguzi halali, huru na haki bali uporaji na uhalifu wa kiuchaguzi.
2. Kamati Kuu inalaani mauaji, vipigo/kujeruhi na ukamataji kwa wagombea, mawakala, viongozi na wanachama kabla, wakati na baada ya uchaguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi.
3. Kamati kuu inawapongeza wagombea wote waliojitokeza kugombea kupitia Chadema.
4. Kamati kuu inawapongeza wadau wote ambao wamejitokeza hadharani na kulaani uchafuzi huu ambao ni hatari kwa uhai wa taifa letu, tunaendelea kutoa rai kwa wadau wengine kusema hadharani misimamo yao kuhusu uchaguzi huu; Aidha tumesikitishwa na baadhi ya taasisi na watu ambao wameendelea kupongeza uchaguzi huo ambao unahatarisha uhai wa taifa letu.
5. Kamati Kuu imethibitisha bila shaka yoyote kwamba hakuna utashi wa kisiasa (political will) kutoka kwa Rais, Viongozi na mfumo mzima wa Serikali ya CCM juu ya uboreshaji wa mifumo ya uchaguzi ili kuleta chaguzi huru, haki na zinazoaminika nchini. Imethibitika kuwa kauli zao haziaminiki tena hivyo ni lazima pawepo na maboresho ya kisheria juu ya mifumo ya uchaguzi nchini.
6. Kamati Kuu inatoa wito kwa wadau wote nchini wakiwemo vyama vya siasa, Taasisi za dini, makundi ya kijamii,Asasi za kiraia,wasomi,wakulima ,wafanyabiashara, watu mashuhuri katika jamii na wananchi wote kuunganisha nguvu zza pamoja ili kutafuta na kudai mifumo huru ya uchaguzi nchini.
7. Kwa kuwa, wananchi wanawafahamu viongozi waliotangazwa kwa wizi, bila kushinda; Kamati Kuu inawahimiza kwamba, wananchi wa maeneo hayo kuwanyima ushirikiano viongozi wote wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa/vijiji na kata walioshiriki kuharamisha uchaguzi wa tarehe 27 Novemba, 2024.
8. Kamati Kuu imeazimia kuendeleza vuguvugu la kudai Katiba Mpya na kushinikiza kufanyika maboresho ya sheria na mifumo ya Uchaguzi itakayowezesha uwepo wa Uchaguzi Huru na wa Haki kuelekea 2025.
9. Kamati Kuu itaendelea kushinikiza kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na yenye watumishi wake walioajiriwa na Tume ambao watasimamia Uchaguzi wowote nchini kwa mujibu wa sheria badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa kuazima watumishi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kusimamia chaguzi.
10. Kamati kuu imeazimia kuwa Jumuiya ya kimataifa na taasisi zake wachukue hatua dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuminya Demokrasia na kutokuwepo kwa uchaguzi huru, haki na za kuaminika nchini.