Yapo wapi majina ya wanafunzi na Programu zao za Shahada kutoka TCU?

kabiriga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
861
830
Jana nilipitia tovuti ya wizara ya elimu sayansi na teknologia nikakuta taarifa mpya ilinayoonekana kutolewa na katibu mkuu wa wizara husika.

taaarifa hiyo pamoja na mambo mengine imewataka wanafunzi wa elimu ya juu hususani wanafunzi wa shahada ya kwanza kuangalia majina yao kwenye tovuti ya TCU jana 18 kujua kama majina yao yapo miongoni mwa wanafunzi wanaotakiwa kuendelea na masomo baada ya uhakiki wa sifa za kusoma shahada au la

chakushangaza ukiingia kwenye tovuti ya TCU hakuna taarifa yeyote kuhusu hili.taarifa hizi zinachanganya wanafunzi maana hawajui miongoni mwao kama wanaendelea na masomo au la kwa mjibu wa maelezo ya wizara.hii inaonyesha wizara haijafanya mawasiliano na TCU ktk hili vinginevyo majina yangelionekana katika tovuti ya TCU ktk tarehe iliyotajwa ktk taarifa ya wizara yaani jana.


TAARIFA KWA UMMA: KUHUSU UHAKIKI WA VYUO NA WANAFUNZI WANAOENDELEA NA MASOMO YA SHAHADA

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.



Uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo, vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.

Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.

Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia




Read 2263 times
 
Tangazo halieleweki hasa sehemu ya mwisho.Eti ambaye hataona jina lake afanye nini? Halafu ni nani atakayesitishiwa masomo?
 
Back
Top Bottom