Yapi ni makato ya mshahara wangu endapo nikiajiriwa?

Yapi ni makato ya mshahara wangu endapo nikiajiriwa?

Lukaku Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2017
Posts
843
Reaction score
740
Poleni na kazi lakini pia hongereni kwa mlio ktk ajira maana naamini mnakula vinono tu.

Nasikia ukiajiriwa kuna makato kutoka Serikalini kama vile nusu kwa nusu ya mshahara wako. Je, ni kweli?

Naomba kuyajua hayo makato kama kweli yatafika nusu kwa nusu au ni maneno ya watu tu. 50%50 from the government mimi siamini kama kweli makato yanafika nusu kwa nusu.

Naomba anayeyajua ayaweke hapa tupige hesabu wote.
 
Sasa wee jamaa kama unaamini makato 50% au hauna habari makato gani mfanyakazi anatakiwa kukatwa hata kama sio kwa undani, utaajiriwa kweli?

Inategemea na taasisi au idara.
Mfano mfuko wa uzeeni inaweza kuwa 5% au 10% ya mshahara wako. Kuna kodi inayotegemea mshahara wako kiasi gani.

Usichanganye madeni ya mikopo, mikopo ya elimu ya juu kwenye makato ya msingi ya mfanya kazi.
 
Mkopo wa chuo 15%
Bima ya afya 3%
Mfuko wa jamii 15%
Chama cha wafanyakazi kama upo...
Pay as you earn(PAE)...hapo ni kutokana na mshahara wako kima cha chini 9%.Nadhani hapo ukifanya hesabu utaelewa vizuri.
 
Na bado bodi ya walimu. Pindi waki activates tu
 
Back
Top Bottom