Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Picha hapo chini ni majina ya wafanyakazi na mashine walizopangiwa katika Gati No.8 - 11 Bandarini. Hiyo chini ni taarifa ya jana tar.6/Julai /2023.Ukisoma hapo bado taarifa zote zinaandikwa TICTS ,mifumo yote kuanzia RDS hadi SSG ya kuongozea inasoma TICTS alafu tunaambiwa TICTS iliondoka tangu Dec 2022.
Wakati huo huo wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi chini ya TICTS waliitwa na TPA @tpa_tz kutambulishwa Kwa CEO wa kampuni ya ADANI GROUP ,kwamba wafanyakazi wote waliokuwa chini ya TICTS wamerithiwa rasmi na ADANI GROUP (Wahindi) .
Lakini jambo la kushangaza hadi sasa wafanyakazi hawa hawajapewa mkataba wowote wa kufanya kazi ingawa wanaambiwa wapo chini ya ADANI GROUP
,vitambulisho vyao bado vinaandika TICTS ikiwa wanaambiwa wapo chini ya ADANI GROUP , Mifumo katika mashine zote inasoma TICTS kuanzia mifumo ya Mashine za YARD za kuongozea huitwa RDS hadi mifumo ya Mashine za Baharini huitwa SSG bado inasoma TICTS.
Wafanyakazi hawa baada ya TICTS kuondoka , wengi walitaka wachukue mafao yao NSSF @nssftz lakini @tpa_tz chini ya Mkurugenzi Mbossa imegoma kuruhusu wafanyakazi hawa kuchukua mafao yao ,wakiambiwa wamerithiwa na ADANI GROUP.
Maswali ya msingi .
1.Huyo ADANI GROUP alipatikana vipi kupewa hiyo kazi ya Operation katika Gati No.8 hadi No.11 ikiwa hakuna tenda iliyotangazwa (Competitive Bidding) ? .Nani alimleta ADANI GROUP na kwa utaratibu Gani ? .
2. Kwanini mitambo na mifumo yote RDS hadi SSG bado inaandikwa TICTS ikiwa serikali kupitia Waziri Mkuu Mh. @kassim_m_majaliwa na Mh. @prof.mbarawa_m mlisema TICTS hayupo tangu Des.2022 , kitu gani kinaendelea ambacho ni siri ? .
3.Kwanini vijana na wafanyakazi wote waliokuwa wanafanya kazi chini ya TICTS, hadi sasa wanafanya kazi bila kupewa mkataba wowote , ikiwa TPA @tpa_tz imewaambia kwamba sasa hivi wapo chini ya ADANI GROUP na wamerithiwa na ADANI GROUP. Huyu ADANI GROUP kwanini hajatoa Mkataba ?.
4. Kwanini tunafichwa fichwa yanayoondelea sasa hivi, hapo Bandarini kuhusu huyu ADANI GROUP na TICTS katika Gati No. 8 hadi 11, Serikali inaficha nini ambacho sisi Wananchi hatupaswi kukijua ?.
Abdul Nondo.