Yanga yamtema Mniger wake, yamuongezea mkataba Twite!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,985
Winger wa kimataifa wa Niger Issoufou Boubac
boubacar+222.JPG
Twite.jpg
ar Garbar ambaye alisajiliwa na klabu ya Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili la mwezi January, amepewa barua ya kuvunjiwa mkataba na klabu hiyo.

Garbar ameshindwa kudhihirisha ubora wake kwenye kikosi cha Yanga kwani ameshindwa kupambana na kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga na mara nyingi amekuwa akianzia kwenye benchi huku akianza kwenye mechi chache tu.

Mniger huyo amezumu kwa muda wa miezi minne tu tangu aliposajiliwa na mabingwa hao wa VPL na FA Cup kwenye msimu wa 2015-16 uliomalizika hivi karibuni.
Wakati huo huo Yanga SC imemuongezea mkataba wa Miaka miwili kilaka wake mwenye asili ya Congo Mbuyu Twite.
 
ni wakati sasa wa hizi timu zetu kujifunza namna ya kusajili wachezaji wageni. waache kusajili kwa kutumia maajenti wawaletee wachezaji wawajaribu kwani mchezaji anaweza fanya vizuri kwenye majaribio lakini akafanya vibaya baada ya usajili. staili ya kumsajili mchezaji baada ya kumuona kwenye mashindano kama ilivyotokea kwa ngoma na kamusoko ndio sahihi kabisa.
 
wakati mwingine tendeni haki, sio kulaumu tu. Issoufou ni mzuri, ila majeruhi yamechangia kuachwa. Halafu si kila mchezaji ataendana na falsafa ya kila timu, angalia kina Debruyne kwa mfano
 
Back
Top Bottom