Yanga yafutiwa adhabu ya kutosajili baada ya kumlipa Bigirimana

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
GBN3fVPW4AAPCmq.jpeg
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea Yanga adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kukamilisha malipo ya aliyekuwa mchezaji wake Gael Bigirimana.

Awali mchezaji huyo alifungua kesi FIFA dhidi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya NBC kwa kushindwa kumlipa baada ya kumvunjia mkataba.

Bigirimana alishinda kesi hiyo, na Yanga ilitakiwa kumlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa, lakini haikutekeleza na kusababisha ifungiwe kusajili.

Baada ya kukamilisha malipo hayo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungulia Yanga kufanya uhamisho wa ndani wa wachezaji.

===

Pia soma
1.
Yanga yafungiwa kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana
 
Hapa Injinia akubali tu alicheza pata potea kwenye usajili wa huyu mchezaji.
 
Back
Top Bottom