Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,554
Klabu za Kitayosce iliyoko Ligi Kuu ya NBC, na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship zimefungiwa kusajili wachezaji.
Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya Kocha Ahmed El Faramawy Youse Mostafa Soliman kushinda kesi za madai dhidi ya klabu hizo.
Kocha huyo raia wa Misri ambaye alizifundisha timu hizo kwa nyakati tofauti alifungua kesi FIFA akipinga kuvunjiwa mikataba kinyume cha taratibu.
Baada ya Soliman kushinda kesi, klabu hizo zilitakiwa ziwe zimemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini hazikutekeleza hukumu hizo.
Wakati FIFA imezifungia klabu hizo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezifungia kufanya uhamisho wa ndani.
TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia a wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.
Iwapo Klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu.