Yanga ya kimataifa yakwama, watembeza bakuli

Keng'oni

Senior Member
Dec 30, 2013
183
147
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KATIKA hali inayoashiria ni kuyumba kiuchumi, klabu ya Yanga imeandika barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikitaka ilipwe malimbikizo ya fedha zake za haki ya matangazo ya Televisheni ya Azam TV, Sh. Milioni 372.

Kwa ujumla Yanga inataka ilipwe Sh. Milioni 422 pamoja na Sh. Milioni 50 za kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Yanga haikupewa zawadi yake ya kutwaa ubingwa wa Kombe la ASFC Mei mwaka huu ikiwafunga Azam FC 3-0 katika fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga pia ilisusa kuchukua mgawo wa haki za matangazo ya Televisheni kwa miaka yote mitatu baada ya kutoridhia mkataba wa TFF na Azam TV.
10.jpg

Lakini katika hali ya kustaajabisha ghafla Yanga wameibua na kuiandikia barua bodi ya Ligi ya TFF kuomba malimbikizo ya fedha zake hizo, Sh. Milioni 372.

Habari za ndani ambazo Bin Zubeiry Sports - Online imezipata zimesema kwamba Bodi ya Ligi baada ya kupata barua hiyo ya Yanga waliwajibu wakiitaka klabu hiyo kwanza iandike barua ya kuutambua na kuukubali mkataba huo wa Azam TV ndipo utaratibu wa malipo yao ufanyike.

Bodi ya Ligi bado inasubiri sasa barua kutoka Yanga wakiikubali Azam TV kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ili utaratibu wa malipo yao uanze.
Na hatua ya Yanga kudai fedha hizo inakuja katika kipindi ambacho kumekuwa na matatizo hadi ya kulipa mishahara ya wachezaji.

Inadaiwa wachezaji wa Yanga walipitisha miezi mitatu bila kulipwa mishahara kati ya Julai na Septemba na hiyo inatajwa kama sababu ya timu kufanya vibaya kwenye mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika.

Aidha, wiki iliyopita wachezaji wa Yanga waligoma kwa simu mbili kufanya mazoezi, Jumatatu na Jumanne wakishinikiza kulipwa mishahara yao ya Novemba.

Kwa ujumla hali ya kiuchumi si njema ndani ya Yanga tangu kuondoka kwa waliokuwa wadhamini wakuu, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) waliokuwa wakiidhamini klabu hiyo pamoja na mahasimu, Simba kupitia bia ya Kilimanjaro.

Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit alipotafutwa katika simu yake alisema hawezi kuzungumza chochote kwa leo kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi.

“Jamani hata siku za sikukuu pia mnatupigia simu?”alihoji Baraka na baada ya kuuliwa kuhusu klabu kuiandikia barua Bodi ya Ligi ya TFF kudai malimbikizo ya fedha za Azam TV, alisema; “We nani kakuambia, kwanza siwezi kuzungumza chochote nipo nje ya ofisi, nipigie kesho nikiwa ofisini,”alisema.

Source: Bin Zubeiry

Hivi ile logo ya Quality Group mnayotumia watani wangu Mkataba wake kwa Mwezi Sh. Ngapi?!

Au Mnapunguza lile Deni la 11bn?
 
Timu kudai haki nu kutembeza bakuli?
Je mnyama anayedai million 50 za Kessy atakuwa anatembeza ndoo kabisa?
Kutochukua hela muda wote wakati mikia wanaziotea siku zote inaonyesha Yanga hawana dhiki
 
Subirini zifike Yanga ili tape ile hamsini ya Kessy. Mwakani tunachukua mwingine na kuwapa 50 nyingine
Mkuu ukweli unauma eti??
Haya andikeni barua kuutambua mkataba wa azam

Yakheee mwajitia mnapesa kumbe ni makapuku,
Any way hiyo ndio hasara ya kumtegemea mtu mmoja katika malipo ngoja nI
 
Subirini zifike Yanga ili tape ile hamsini ya Kessy. Mwakani tunachukua mwingine na kuwapa 50 nyingine
Pesa ya kuendea msalani hamna. Jamaa kazima simu. Bakuli mtindo mmoja. Wewe umechangia?Au ndio wale mchango wao ni kupiga magoti?Si mlisema mkataba wa Azam ni wa kinyonyaji?Vipi leo kurudia matapishi?
 
Pesa ya kuendea msalani hamna. Jamaa kazima simu. Bakuli mtindo mmoja. Wewe umechangia?Au ndio wale mchango wao ni kupiga magoti?Si mlisema mkataba wa Azam ni wa kinyonyaji?Vipi leo kurudia matapishi?
Ngoja tukakope kwa Mo. Wapiga dili wa mikia hawana simile. Wanapiga hesabu za wizi wizi tu
 
Ngoja tukakope kwa Mo. Wapiga dili wa mikia hawana simile. Wanapiga hesabu za wizi wizi tu
Lipeni za jamaa. Billioni 11.Akichachamaa litauzwa hilo bwawa la kufugia vyura.Mnampigia magoti binadamu huo ndio udhalili wa mwisho mtu ukiwa hai.
 
Kwenye ile picha ya wapiga magoti wewe ndio huyo mwenye shati la light blue?
 
Tatizo la watanzania tuko wavivu.. Yanga timu yetu wote..tukiwa na wanachama laki tano na Ada ya kadi elfu tano kwa mwaka .2.5 Bilioni . Na tukipata na makampuni ya kutufadhili hii timu inajiendesha yenyewe bila ya kutegemea matajiri..
NB:kadi za kieletroniki
 
Lazima ifikie hapo maana jamaa anadaiwa bil 13 wakati huo yeye anaidai yanga bil 11

Hapo lazima mmoja anyoshe mikono
 
Back
Top Bottom