Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Imefichuka kuwa klabu ya Yanga imemwaga dau nono ili kumshawishi kiungo mahiri Feisal Salum "Fei Toto" kurejea Jangwani. Kwa mujibu wa taarifa, Yanga wameweka mezani ofa ya shilingi milioni 750 kama sign-on fee pamoja na mkataba wa miaka miwili. Aidha, kiungo huyo ameahidiwa mshahara wa shilingi milioni 40 kwa mwezi endapo atatia saini.
Yanga wanaonekana kuwa makini kwenye dili hilo, huku wakitumia nafasi ya mauzo ya nyota wao Stephane Aziz Ki kama chanzo cha kujiamini kifedha katika vita hiyo ya usajili. Mauzo hayo yanatazamiwa kuwaingizia mabilioni ya shilingi, jambo linalowawezesha kusukuma ofa nzito kwa wachezaji muhimu.
Kwa upande wa wapinzani wao Simba SC, taarifa zinasema ofa yao ya mwisho kwa Fei Toto ilikuwa shilingi milioni 600 kama sign-on fee, ambapo wamepanga kulipa shilingi milioni 400 msimu wa kwanza na milioni 200 katika msimu wa pili.
Mpambano wa kuwania saini ya Fei Toto unaonekana kuwa mzito, huku Yanga wakionekana kutaka kufunga dili hilo haraka ili kumrudisha kiungo wao wa zamani kambini.