MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 2,507
- 4,933
Wakati msimu unaanza, Miguel Gamondi aliendelea na kazi yake, Ila mashabiki wengi hatukufurahishwa na mwenendo wa matokeo ya ushindi mwembamba, Yanga ilikuwa inashinda lakini kwa taabu, hatimaye Tabora na Azam wakachukua alama. Tukaona isiwe kesi, ikatua mashine ya Kijerumani, pira likaguswa, likaachiwa watu wakaenda kwao! Huenda bila kuyumba kidogo Yanga angetinga robo fainali CAFCL. baada ya kuondoka akaingia silent killer mmoja asiyeimbwa sana, Miloud Hamdi, akampiga mtu 2 akapita akaenda zake. Kwa kifupi pamoja na hekaheka zote za makocha bado wapinzani wameshindwa kufurukuta! Unadhani sababu ni nini?