Yanga fanyeni hesabu za kiuchumi kwa Mayele

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,318
12,622
Hakuna shaka kuwa Mayele ana malengo yake na Yanga wana malengo Yao. Pale kwenye makutano kati ya Faida kwa mayelle kucheza Yanga na Faida ya Yanga kuwa na Mayelle ndizo hesabu za kweli.

Je, vyanzo vya mapato vya Yanga (viingilio vya mlangoni, matangazo, udhamini, mauzo ya gesi na zawadi za ushidi vinamudu kumbakiza Mayelle na wengine Yanga kwa mishahara Yao? Je, dau analopewa Mayelle kutoka nchi nyingine mnaweza kumpatia ili abaki Yanga kwa faida?

Msipokuwa makini club itahangaika sana kumlipa mchezaji mmoja mshahara mkubwa ambao ungeweza kuwalipa wachezaji 4 wenye uwezo unaokaribiana na ule wa Mayelle,, na msipokuwa makini Mayelle anaweza kubaki lakini akiwa hayuko Happy akifikiria dau nono atakalokosa kwa kubaki Yanga (opportunity cost) kutokana na uzalendo na huruma zake kwa Yanga..

Vinginevyo uzeni Sasa mpate faida kabla kiwango Cha Mayelle kwenda chini kwa uzee au majeruhi (in case).

Kama ningekuwa mm ningembakisha Mayelle Yanga lakini ningembakisha kwa kumfanyia biashara kubwa ya matangazo kwenye makampuni, jezi na mavazi. Mfano natengeneza key holders, viatu, nguo/jeans/vuvuzela nk zenye picha/jina la Mayelle kama zinavyofanya timu zenye wachezaji ghali sana duniani.
 
Yanga ni timu ndogo bado (feeder club), haiwezi kuwa na kikosi chenye mchezaji wenye tofauti (variance) kubwa ya mishahara, mmoja anaelipwa 50M na mwingine 5M at the same time. wachezaji wote Yanga Wana wastani wa mishahara ya <10M, halafu mchezaji mmoja TU anakuwa na >40M. Hii 40m kwenye utafiti inaitwa out layer. Outlayer Ina tabia ya kupotosha matokeo ya utafiti. Faida ya kuwa na mchezaji mmoja mwenye 40+ katikati ya wachezaji wenye range ya 5-10 ni kuwa huyu mchezaji atajituma sana, atajikomba kwa uongozi, na akiwa mjinga atajivuna. Hivyo anaweza kukumbana na kukosa ushirikiano ndani na nje ya uwanja kutoka kwa wachezaji wenzake, wachezaji wengine wanaweza kuwa na mgomo wa wazi (Fei Toto) au baridi.
 
Uchumi + Burudani = 0
Hakuna mwekezaji anatumia hesabu kama hizo, ndio maana mo haachi kutoka uvunguni mwa meza yake na kulia anapata hasara. Timu zetu haziwezi kuwaatamia wachezaji kama Mayelle kwenye soko la ushindani. Ni Mayelle TU mwenyewe achague kati ya fedha na furaha. Yanga Kuna furaha bila hela nyingi, lakini uarabuni Kuna fedha bila furaha. Awaulize akina Chama na miquison.
 
Hakuna shaka kuwa Mayele ana malengo yake na Yanga wana malengo Yao. Pale kwenye makutano kati ya Faida kwa mayelle kucheza Yanga na Faida ya Yanga kuwa na Mayelle ndizo hesabu za kweli.

Je, vyanzo vya mapato vya Yanga (viingilio vya mlangoni, matangazo, udhamini, mauzo ya gesi na zawadi za ushidi vinamudu kumbakiza Mayelle na wengine Yanga kwa mishahara Yao? Je, dau analopewa Mayelle kutoka nchi nyingine mnaweza kumpatia ili abaki Yanga kwa faida?

Msipokuwa makini club itahangaika sana kumlipa mchezaji mmoja mshahara mkubwa ambao ungeweza kuwalipa wachezaji 4 wenye uwezo unaokaribiana na ule wa Mayelle,, na msipokuwa makini Mayelle anaweza kubaki lakini akiwa hayuko Happy akifikiria dau nono atakalokosa kwa kubaki Yanga (opportunity cost) kutokana na uzalendo na huruma zake kwa Yanga..

Vinginevyo uzeni Sasa mpate faida kabla kiwango Cha Mayelle kwenda chini kwa uzee au majeruhi (in case).

Kama ningekuwa mm ningembakisha Mayelle Yanga lakini ningembakisha kwa kumfanyia biashara kubwa ya matangazo kwenye makampuni, jezi na mavazi. Mfano natengeneza key holders, viatu, nguo/jeans/vuvuzela nk zenye picha/jina la Mayelle kama zinavyofanya timu zenye wachezaji ghali sana duniani.
Mauzo ya GESI
 
Sioni shida kama Mayelle atabaki au kuondoka. Msiache kuchukua hela ndefu kama inakuja mezani. SEMA TU kama Kuna deal la nje ya Africa ni bora zaidi ili kuepuka kumuuzia silaha kubwa adui yako.
 
Back
Top Bottom