Yanga CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga CCM!

Discussion in 'Sports' started by Mbu, Mar 31, 2009.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...sasa nimethibitisha uhusiano baina ya hawa kandambili na CCM, ndio maana hata wakishinda utawasikia,

  "...CCM! CCM! CCM!..."​

  ...kama hilo halitoshi kila kiongozi anayeingia madarakani (tangu Uhuru) anatokea kwenye mizizi ya hawa 'sie Yanga khakhaaaaa...!'

  ...Jakaya Mrisho wa Kikwete yeye ndio mnazi hasa, tena maskani yake yalikuwa pale mwembe Yanga, Mzee Mwinyi ndio ohoooo..., 'Mchonga' yeye angalau alificha ficha makucha japo mnh(!?), Mzee Karume yeye hakujizuia, aliwajengea pale Jangwani!

  Mbaya zaidi (kwetu sie Taifa Kubwa), leo huyu Makamba naye analeta viroja vyake;

  ...yaani huyu bwana mkubwa hakuona mfano mwingine kama SIMBA TAIFA KUBWA, yeye kakazana Yanga, Yanga... pheeeeeeww, tunaongozwa na YANGA injii hii!
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Achana na Makamba bwana hapo anapiga Kamba zake!
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mgosi yule alitakiwa angalau ashabikie African Sports (mnh?, na hawa nao tawi la yanga Tanga!) au Coastal Union...
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Habari ndio hiyo..... upendi sio?
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Ndo maana yake na hata CHADEMA,CUF,NCCR,UDP,TLP you mention viongozi wake wakuu ni yanga damu, nyie simba hamna pakutokea kila kiongozi wa nchi hii ni yanga. usisahau wafanya biashara maarufu wote ni yanga Mengi, Manji you name! Naona kabisa kuna haja ya kufanya research kwa nini watu wote wenye mafanikio ni YANGA DAMU? au kuwa yanga ni sign ya miakili kibao? nakuibia siri obama naye yanga damu.
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kazi ipo, mtapiga kelele weeeee, lakini mambo yote ni Wekundu wa Msimbazi, Simba.
   
 7. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Pole mtani Simba ishakuwa nyanya siku hizi kiwango cha mbagala united, du hivi ligi bado inaendelea?juzi niliwasikia watani wanashangilia
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mbu hata nafasi ya 2 kuna hati hati msifikie sijui...
   
 9. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Hii yote ni kutokana na kauli ya Mr.Makamba;lakini yeye alikuwa anamaanisha jinsi Yanga ilivyotangaza ubingwa mapema kabla ya kuisha kwa ligi pia ndiyo wanaolishikilia kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa CCM huko jimbo la Busanda.Hiyo ilikuwa ni kauli ya majigambo kutoka kwa Yusuph Makamba.
  Haina maana kila kiongozi lazima awe mshabiki ya Yanga!Kuwa wengine hata mambo ya soccer kwao haya nafasi,ili zungumzia issue ya fedha;hata majani watanzania watakula ili mradi yeye na jamaa zake wapate.
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yani Simba ni kama Mbagala United?, Mkuu Burn siku tukikutana Yebo Yebo hata kama mmeshakuwa bingwa mtafungwa. Hasira za kukosa ubingwa lazima ziwashukie.
   
 11. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Du nasikia mna struggle kupata nafasi ya pili? sisi mechi ya simba kwetu sio dili sana, maana hawana wanachoweza ila fitna tu, tunaweza kuwaachia kwa sababu kwetu haina umuhimu na tukiwafunga kinachofuatia ni mgogoro msimbazi.
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Basi kama yanga ni CCM basi
  Simba ni CUF
  Kagera ni Chadema
  n.k
  Mi nadhani Makamba alichemka kutoa mfano kama huo nanivyo jua mimi makamba ni simba ama..
  Kesho atasema CCM ni Wakritu
  hajui anapo tamuka simba unawagusa nusu ya watanzania au ndiyo changamoto yenyewe.....
  au aliimanisha YANGA NI MAFISADI KAMA CCM MAANA WANAZAMINIWA NAFISADI
   
 13. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Du kaazi kwelikweli hapo timu lenu likiboronga mtamlaumu nani? maana mashabiki hata kuandika hawajui, kweli Simba ni nyanya.
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Na wengi wao ni Mafisadi ndiyo maana wana mafanikio unajua pesa haramu inamafanikio kwa sana tu...Hivi na RA nae ni yanga ila sia mini kama obama ni Yanga...Timu simba
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwanza tunafukuza kocha, Hasira ndiyo maana nilichemka...vipi waume zenu wameshatua (Al Ahly)...............................mtajuta kukutana nao au msipeleke timu kama kawaida yenu tetetetetetetetetetetetetetetetete..
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Kufukuza kocha ndio suluhisho nawashauri uzeni na timu yote kwa Azam united muanze upya, hao vibonde wa Misri tunakwenda kuwachinjia uwanja mpya wala usihofu huku hakuna hujuma kama kwao..pole hivi Simba wanashiriki mashindano gani tena?
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kombe la mbuzi kule Mabagala!! umesahau?
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Sawa mkuu yetu macho na masikio lkn msije tafuta visingizio oooooooh!! hawa jamaa walishazoea kutumia viwanja vizuri ndiyo maana wametufunga, eti hujuma kwani nyie hamuwezi fitna za michezo tumie pesa za kifisa kufanya hujuma, kwanza nini kiliwafanya mng`ang`anie uwanja wa uhuru au ilimuweze kuchimbia matunguli yenu vizuri....nawatakia ushindi wa 2 -1 ili tubanane hapa, tunashiriki mashindano gani, kwani lazima kila timu tushiriki zamu yenu lkn aibu tu..
   
 19. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Eagle is not A Chicken!!
  YANGA IMARA
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Simba Nguvu moja upo hapo kaka
   
Loading...