Yanga bado uswahili na ubabaishaji unatusumbua

Smt016

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
2,288
3,019
Kiukweli ukiangalia namna GSM na viongozi wa Yanga wanavyoendesha timu kiukweli inashangaza sana. Nilitoa uzi hapa nikiziomba timu zetu zinazowakilisha nchi zijikite kwenye maandalizi ya uhakika kwa kucheza walau mechi zisizopungua nne ili kuimarisha vikosi na pia kuwaweka wachezaji katika fitness, lakini naona Simba, Azam na biashara ndiyo mpaka sasa ndio walionesha kuwekeza kwenye performance ya timu na huku Yanga ikionesha nguvu kubwa kuwekeza kwenye kupiga domo. Una mechi ya klabu bingwa mapema kabisa mwezi wa tisa lakini Cha ajabu hata haujacheza mechi yoyote ya kirafiki unaenda kuweka kambi Morocco kambi ambayo haina impact yoyote zaidi ya kupoteza muda.

Mechi ya wiki ya mwananchi haitokuwa na msaada wowote kiufundi kwasababu wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza watakuwa kwenye mataifa yao kucheza mechi za kimataifa. Na la pili hata yakionekana mapungufu una muda mchache sana kurekebisha kabla ya kucheza na Rivers United. Na hauwezi kujua kama imerekebishika pasipo kucheza tena mechi ya kirafiki kuona hali ya kikosi. Kwa upande wa maandalizi ya timu, GSM na viongozi wa Yanga wamefeli. Mimi binafsi ikitokea Yanga imeshindwa kuingia hatua ya makundi klabu bingwa sitolaumu mchezaji yeyote wala benchi la ufundi bali uendeshaji mbovu wa timu hakuna usiriazi kwenye uwekezaji wa uwanjani zaidi ya propaganda tu.

Kituko kingine ni hili la kumkaribisha Haji Manara ndani ya Yanga. Hili binafsi ni moja ya tukio lililonipa mashaka juu ya uwezo wa kufikiria kwa hawa watu wanaoionhoza Yanga. Yaani Manara katoa kila aina ya kejeli, kila aina ya tusi na hao hao Wana Yanga walikuwa wanapiga kelele kuwacheka Simba kuwa wanamsemaji mswahili sana lakini leo kageuka keki Yanga. GSM kawaza kibiashara zaidi lakini atambue kuwa hata Manara alivyokuwa yupo Simba, alifanikiwa kuujaza watu kwasababu ya mpira unaoonekana na matokeo yanayoonekana uwanjani na sio kwamba kupiga domo huku timu ikiwa haifanyi vyema.

Hivyo GSM na uongozi wa Yanga mpira sio kupiga domo na propaganda bali wekeni nguvu kwenye maandalizi ya timu, wekeni nguvu kwenye mpira mzuri na matokeo mazuri hata muhamasishaji hatotumia nguvu nyingi kujaza watu. Ila kama matokeo yatakuwa mabaya uwanjani huyo Manara hatoweza kuwafunga kamba watu wakajaze uwanja.

Mimi binafsi safari hii kama timu haitofika hatua ya makundi klabu bingwa, basi sina budi nikae pembeni ushabiki kwenye timu hii itakuwa basi tena nitarejea baada ya mfumo mpya wa uwekezaji.
 
Umenena vizuri mkuu. Hatuwajui wasemaji wa Liverpool, Barcelona , Real Madrid, Chelsea, Bayern Munich, Manchester city, nk tunajua show zao kwa pitch tu. Hao wanao amini Manara atawafikisha ilipofika simba aisee muda utawapa majibu mazuri
 
Nimemsikiliza leo msemaji mpya wa hawa unaowazungumzia nikaona kuna shida yaani press karibu yote ni kuzungumzia ubaya wa alipotoka badala ya kuzungumzia mipango na nini atafanya alipo ni vijembe tu na blahblah

Lilipoulizwa swali kuhusu hiyo mechi na hao wanaijeria ndiyo nikaona hawa watu wategemee maumivu wakijitahidi sana hapa watatoa draw
 
Ushauri kwa mashabiki wa Yanga ni huu-kwanza:wajifunze kukwepa ngumi na mawe mapema kabisa.
pili:mazoezi ya kukimbia,pumzi iwe ya kutosha.
tatu:waandae barua za kudhaminiwa polisi lolote likitokea iwe rahisi kupata dhamana.
Kwa jinsi nyinyi mashabiki wa Yanga msivyo na subira pale Jangwani mkivurunda patachafuka tu lazima.
 
Tulieni hivyo hivyo dawa iendelee kuwaingia vizuri.

Mnajitekenya wenyewe na Kujichekesha wenyewe

Kama ninyi mnaendelea na kambi, kitu gani kinachokufanya ufatilie mambo ya Yanga,kila mmoja ashinde mechi zake na afanye mambo yake anayo ona ni ya msingi

Mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu
 
Mokorokoro mko busy na yanga
IMG_20210826_102448.jpg
FB_IMG_16299622399538730.jpg
 
Lilipoulizwa swali kuhusu hiyo mechi na hao wanaijeria ndiyo nikaona hawa watu wategemee maumivu wakijitahidi sana hapa watatoa draw

Huwa nasoma press za wenzetu huko kuhusu mechi zinazokuja, wenzetu ndio maana wameteka ulimwengu wa soka.

Kocha ndiye anayehusika kuzungumzia mechi maandalizi ya mechi hiyo, ila kwetu huku msemaji ndio anazungumzia ambapo hajui hata kocha kaandaaje wachezaji
 
Kiukweli ukiangalia namna GSM na viongozi wa Yanga wanavyoendesha timu kiukweli inashangaza sana. Nilitoa uzi hapa nikiziomba timu zetu zinazowakilisha nchi zijikite kwenye maandalizi ya uhakika kwa kucheza walau mechi zisizopungua nne ili kuimarisha vikosi na pia kuwaweka wachezaji katika fitness, lakini naona ni Simba pekee ndiye mpaka sasa ndio walionesha kuwekeza kwenye performance ya timu na huku Yanga ikionesha nguvu kubwa kuwekeza kwenye kupiga domo. Una mechi ya klabu bingwa mapema kabisa mwezi wa tisa lakini Cha ajabu hata haujacheza mechi yoyote ya kirafiki unaenda kuweka kambi Morocco kambi ambayo haina impact yoyote zaidi ya kupoteza muda.

Mechi ya wiki ya mwananchi haitokuwa na msaada wowote kiufundi kwasababu wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza watakuwa kwenye mataifa yao kucheza mechi za kimataifa. Na la pili hata yakionekana mapungufu una muda mchache sana kurekebisha kabla ya kucheza na Rivers United. Na hauwezi kujua kama imerekebishika pasipo kucheza tena mechi ya kirafiki kuona hali ya kikosi. Kwa upande wa maandalizi ya timu, GSM na viongozi wa Yanga wamefeli. Mimi binafsi ikitokea Yanga imeshindwa kuingia hatua ya makundi klabu bingwa sitolaumu mchezaji yeyote wala benchi la ufundi bali uendeshaji mbovu wa timu hakuna usiriazi kwenye uwekezaji wa uwanjani zaidi ya propaganda tu.

Kituko kingine ni hili la kumkaribisha Haji Manara ndani ya Yanga. Hili binafsi ni moja ya tukio lililonipa mashaka juu ya uwezo wa kufikiria kwa hawa watu wanaoionhoza Yanga. Yaani Manara katoa kila aina ya kejeli, kila aina ya tusi na hao hao Wana Yanga walikuwa wanapiga kelele kuwacheka Simba kuwa wanamsemaji mswahili sana lakini leo kageuka keki Yanga. GSM kawaza kibiashara zaidi lakini atambue kuwa hata Manara alivyokuwa yupo Simba, alifanikiwa kuujaza watu kwasababu ya mpira unaoonekana na matokeo yanayoonekana uwanjani na sio kwamba kupiga domo huku timu ikiwa haifanyi vyema.

Hivyo GSM na uongozi wa Yanga mpira sio kupiga domo na propaganda bali wekeni nguvu kwenye maandalizi ya timu, wekeni nguvu kwenye mpira mzuri na matokeo mazuri hata muhamasishaji hatotumia nguvu nyingi kujaza watu. Ila kama matokeo yatakuwa mabaya uwanjani huyo Manara hatoweza kuwafunga kamba watu wakajaze uwanja.

Mimi binafsi safari hii kama timu haitofika hatua ya makundi klabu bingwa, basi sina budi nikae pembeni ushabiki kwenye timu hii itakuwa basi tena nitarejea baada ya mfumo mpya wa uwekezaji.
Hivi wewe,huwa unaona hayo mazoezi wanayofanya yanga?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Nimemsikiliza leo msemaji mpya wa hawa unaowazungumzia nikaona kuna shida yaani press karibu yote ni kuzungumzia ubaya wa alipotoka badala ya kuzungumzia mipango na nini atafanya alipo ni vijembe tu na blahblah

Lilipoulizwa swali kuhusu hiyo mechi na hao wanaijeria ndiyo nikaona hawa watu wategemee maumivu wakijitahidi sana hapa watatoa draw
Manara aliitwa lopo lopo alivyokuwa Simba leo kaja Yanga mashabiki wanaona kama njia ya kuifanya Simba kuwa wanyonge. Tunasahau kuwa namna nzuri ya kumfanya awe mnyonge ni kumzidi kimafanikio katika wakati husika. Matokeo bora na mataji ndio njia pekee ya kumziba mwenzio mdomo.
 
Haji Manara anapata platform kubwa kwa sababu Watanzania tunapenda Propaganda , Tatizo kubwa la mpira wa Tanzania umeegemea zaidi kwenye Propaganda na sio uhalisia wenyewe .
 
SAWA UNAISIFIA SIMBA NA KUIKEJELI YANGA, THEN UNAMLAUMU GSM, WEWE CHUKI INAKUSUMBUA, WALA HUNA POINT YA MAANA APO ILA NI USWAHILI TU.

NIKUULIZE

KWANI WAKIINGIA AU WASIINGIE WE YANAKUHUSU NINI? TUACHIE TIMU YETU WE KAA NA MIKIA YAKO.
 
Watu hawapendi kuambiwa ukweli unasema sina hoja. Je wewe mpira ni mfuatiliaji au ndio shabiki wa Yanga mkumbo usiyejua mpira? Hoja yangu kubwa ni maandalizi ya timu kuelekea mechi dhidi Rivers United. Katika mpira mguu kuna kitu kinaitwa muunganiko hauletwi kwa mdomo wa Haji Manara wala wiki ya mwananchi bali kwa kucheza mechi nyingi nyingi za kirafiki ili kujua wachezaji wanaofiti kwenye mfumo. Kuna kitu kinaitwa metch fitness inaletwa kwa kucheza mechi za majaribio. Kuna mbinu na ufundi kujua ni formation gani na watu sahihi wa kwenye mfumo hilo pia linapatikana kwa kucheza mechi za majaribio. Nimeisifu Simba kwasababu mpaka sasa wameonesha usiriazi kwenye maandalizi ya kikosi. Wamecheza mechi moja ya majaribio na leo wanacheza mechi nyingine.

Wapinzani wa Yanga wapo nchini Benin kujipima na timu mbali mbali wakati Yanga wapo bize na mwananchi.
 
Mimi binafsi safari hii kama timu haitofika hatua ya makundi klabu bingwa, basi sina budi nikae pembeni ushabiki kwenye timu hii itakuwa basi tena nitarejea baada ya mfumo mpya wa uwekezaji.
Ndugu kwani ni nani aliyekuleta kuwa mshabiki ya Yanga SC?

Nadhani huyu ndiye anaye hitaji zaidi kujua kuwa utajitoa kuwa mwanayanga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom