Uchaguzi 2020 Yanayotokea Tanzania Leo yalitokea Indonesia 1998

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Indonesia ilikuwa na utawala uliojulikana kama The New Order ulioendeshwa na Rais Surharto. New Order ili dumu madarakani kwa miongo mitatu, watawala walikuwa wamepumzika na hawakuangalia tena matatizo ya wananchi walala hoi.

Mwaka 1998 upinzani ulifanya campeni ya nguvu. Pamoja na The New Order kuwa na jeshi, polisi na Usalama wa Taifa, ushindi wa upinzani ulikuwa mkubwa mno.

Mabadiliko makubwa ya kiutawala yalifanywa na Upinzani ulipoingia madarakani. Haikua kazi rahisi na walipitia mwaka mzima wa mtikisiko wa kuichumi. Baada ya hapo mpaka sasa hali ya siasa a uchumi iko shwari.

Mnaopenda kusoma zaidi nendeni Wikipedia msome The history of Indonesia.
 
Suala la maendeleo ya watu kwa sasa kutoka kwa viongozi wa CCM na itikadi wanayoisimia, ni kama mfano wa uliopo ndani ya maandiko matakatifu kuhusu kiriba cha kale na divai ya kale. Ukale huo unahakisiwa ktk sura ya maendeleo toka Tanganyika ilipopata uhiru wake mwaka 1961 mpaka nchi yetu ilipo hivi sasa.

Huwezi kuweka divai mpya ktk kiriba cha zamani, kwa kuwa kiriba cha zamani huifadhiwa divai ya kale, na hali kadhalika divai mpya ktk kiriba kipya, la sivyo kwa kufanya hivyo kiriba cha kale kitapasuka na divai mpya itamwagika yote na kupotea.

Nchi hii inahitaji viongozi wapya na maono mapya ya kiitikadi kwa ajili ya kesho ya siha na afya njema ya mama Tanzania. Kauli za kibabaishaji za CCM mpya ni kutaka kucheza kamari na maisha na maendeleo ya ways kwa mara nyingine tena.
 
bado hatujawa na wapinzani wanaoweza kufanya haya uloyaandika, ikiwa wapinzani wetu wanauza uzalendo wao na kukubali kua watumishi wa mabeberu je wanastahili kukabidhiwa nchi?

ni bora tubaki na fisiem kuliko hawa wapinzani uchwara.
 
Sky Eclat tuacheni na utani wakati mwingine tunawasema CCM ila wale jamaa wamejipanga sanaaa kwenye kila kitu

Upinzani unatafunana wenyewe kwa wenyewe
Maana ya upinzani ni kutegemea kushika dola siku moja. Sasa upinzani usipokua na jitihada za kuchukua dola si upinzani.

Ndiyo maana kuna ushindani atakaeshindwa akubali matokeo.
 
Umeongea vema mkuu... tanzania inahitaji uongozi nje ya ccm..... hapo tutapiga hatua.
 
Back
Top Bottom