Ndiho
JF-Expert Member
- Feb 23, 2013
- 2,306
- 1,531
Tanzania imejaa watu wa ajabu sana. Haya mambo wanapotosha kwa faida ya nani? Hivi sisi tuna sifa tofauti na watu wengine ktk hii dunia? Tuna mawazo ya kimaskini ajabuuuu...Kwa haraka haraka ukisikiliza hiyo hadithi ya upande mmoja unaweza kuamini kabisa kwamba cdm hawako tayari mtu kumuunga mkono rais Magufuli. Na iwapo utaamua kuishia na kufanya hitimisho basi utawaona cdm ni chama cha kijinga sana kwa hicho wanachofanya. Ni dhahiri cdm ni wapinzani wa ccm kisiasa, lakini aina ya siasa zinazoendeshwa na awamu hii ya tano kwao siasa ni uadui, na uadui wao uko dhidi ya cdm na hiki ni kitu kilichopandikizwa na rais mwenyewe.
Mh. Lema aliwekwa magereza kwa kile kilicho wazi kwamba ilikuwa maagizo toka juu, na juu panafahamika ni wapi. Wabunge wenzake walio katika kamati ya bunge toka ccm walitaka kwenda kumsalimia, walipata ujumbe toka huko huko juu kwamba kwenda kumsalimia Lema ni usaliti. Hayakuishia hapo, wapinzani hata huko bungeni imetoka amri ya nyuma ya pazia na mbele ya hadhara kwamba washughulikiwe ndani ya bunge na hata nje ya bunge. Na mtoa amri zote hizo anafahamika. Ikatokea Tundu Lissu kapigwa risasi, hakuna mbunge yoyote wa ccm aliyethubutu na aliyethubutu ambaye ni Nyalandu yakamkuta. Spika hajaenda wala wasaidizi wake. Leo kunaletwa maelezo ya upande mmoja ili kupotosha umma kwamba wapinzani wanazuia rais kusifiwa. Lakini ukiangalia sababu yote ya uhasama huu ni rais huyo huyo anayetetewa leo kwa utetezi wa upande mmoja.
Kilichofanyika jana kwa safari ya Lowassa imetajwa kama ya kibinafsi, lakini imetumika kutaka kuonyesha kwamba Lowassa alibeba ujumbe wa wapinzani kitu ambacho si kweli. Hakuna mpinzani anayepinga Lowassa kwenda ikulu, akitaka ahamie hata na familia yake hakuna mwenye shida, lakini mambo yake binafsi yasitumike kama muwakilishi wa wapinzani. Inafahamika wapinzani wana ajenda na malalamiko yao mengi dhidi ya rais huyu. Inasemekana Lowassa aliongea mambo mengi lakini hayajawekwa wazi bali ya kumsifia ndio yamewekwa wazi. Ifahamike Lowassa aliikuta cdm ikiwa taasisi imara, idadi ya wabunge na madiwani waliopatikana sio kwa juhudi za Lowassa maana cdm hakikuwa chama kipya alichoanzisha yeye. Pia naweza kusema Lowassa sio mpinzani bali alikuja upinzani akaelewana na viongozi wachache kwa vipande 30 vya fedha ili apate nafasi ya kugombea urais.
Wanacdm wengi tunaamini ujio wa Lowassa ulipunguza wingi wa kura, idadi ya madiwani na wabunge iliostahiki kupata kutokana na taswira yake mbaya mbele ya jamii. Na tunasema hata baada ya uchaguzi Lowassa hajawahi kutoa mchango wowote wa maana kwa chama. Kama kuna mtu anamtetea aonyeshe hata ofisi ya room 5 aliyojenga tujue kweli alikuja kuinyanyua cdm. Hakuna mwanacdm anayemtukana Lowassa, tunaomba upotoshwaji huo uachwe mara moja bali tunasema Lowassa alienda ikulu kwa mambo yake binafsi na sio ajenda za chama. Na pia tunapenda kusema kwamba Lowassa ndio alileta kura nyingi, wabunge na madiwani wengi sio kweli kwani cdm ilikuwa na mpango kazi wake wa 2010-2015 wa ondoa ccm, ambao Lowassa hakushiriki na matokea ya hiyo 2015 ilikuwa ni matunda ya operation hizo. Asipewe sifa ambazo sio zake.
CC: msemajiukweli, misuli, thetallest, kipara kipya, jingalao
Rais wa maskini..
Wananchi wote maskini....
Mawazo yetu ya kimaskini... Kufikiri na kutenda kimaskini...
Kula na kulala kimaskini....
Kufanya kazi kimaskini....
Kutembea kimaskini...
Propaganda za kimaskini....
Uongo nao wa kimaskini....
Daaaaahhh, Eeehhh Mungu wangu....