Yanayomkuta Lema yawe fundisho kwa wanasiasa wengine

Yanayomkuta Lema yawe fundisho kwa wanasiasa wengine

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,417
Ni zaidi ya mwezi sasa Godbless Lema haoni jua isipokuwa kwa masaa machache tu anapopelekwa mahakamani. Wapo wanaolalamika kuwa Lema kakaa muda mrefu sana mahabusu ilhali kesi yake ina dhamana. Malalamiko haya yanatokana tu na hisia zao na si uhalisia kisheria.

Mara zote tunawasikia wafuasi wa chadema na viongozi wao wakijigamba kuwa "Tutawapiga Mahakamani". Kwamba, wao wana mawakili bora sana hapa Tanzania na kwa hiyo kiongozi au mfuasi yeyote wa chadema anaweza kusema ama kufanya lolote kwani kisheria Serikali haina nguvu. Hizi ni dharau za hali ya juu sana ambazo kwa hakika zinapaswa kukomeshwa.

Lema yupo Mahabusu sasa. Haijulikani lini atatoka kwa vile uzito wa mashtaka yanayomkabili ni mkubwa sana. Kesi zinazomkabili zinachukuliwa kwa uzito mkubwa sana kwa sababu ametoa kauli ambazo si tu hazikupaswa kutolewa na mtu kama yeye bali hata na mtu mwingine yeyote.

Kumzulia kifo Mkuu wa nchi ni kosa la uhaini ambalo kwa nchi nyingine huchukuliwa kwa uzito mkubwa sana na adhabu yake ni kifo. Sina hakika kwa sheria za hapa kwetu. Hii ni kwa sababu unaposema Mkuu wa nchi atakufa kabla ya muda fulani maana yake ni kwamba wewe mwenyewe unaingilia Malmala ya Mungu ambaye ametanabaisha kwenye vitabu vyake kuwa hakuna ajuaye siku wala saa ya mtu kuondoka duniani isipokuwa Yeye.

Rais kama Mkuu wa nchi anao maadui wengi hasa kwa huyu ambaye kila uchwao anatumbua. Kupitia kauli ya Lema maadui wa Rais wanaweza kutembea na maneno yake na wakafanikisha mauaji ya Rais ili watu waamini kuwa alichoongea Lema kimetimia.

Pia ikiwa Lema ataachwa huru, anaweza kushiriki kwenye mipango ya kumdhuru Rais ili tu kutimiza maono yake. Lema si wa kispot kispot. Ameshiriki matukio mengi makubwa ambayo kama yakiwekwa hapa hadharani hakika hakuna atakayemuamini Lema. Msifikiri ni masihara pale watu wanaposema kuwa kazi yake ya mwanzo kabla hajawa Mbunge ni ya kutisha sana. Si masihara hata kidogo.

Yanayomkuta Lema yawe fundisho kwa wengine. Kipindi hiki tu cha Lema kuwa Mahabusu naona nidhamu imeanza kurejea. Zitto Kabwe katelekeza Akaunti yake ya Twitter tangu Oktoba 21. Ni akaunti hiyo ndiyo aliyokuwa anatumia kuandika mabaya dhidi ya Rais.

Julius Mtatiro naye kaamua kurejea kazi yake ya awali ya uchambuzi. Biashara ya kumshambulia Rais hailipi.

Tundu Lissi naye kaamua kujirekebisha. Aliahidi kupambana na Rais kiangazi na masika ila kwa yanayomkuta Lema hakika hathubutu tena. Kikubwa zaidi ni pale Lissu alipojiengua kumtetea Lema baada ya kuona uzito wa kesi yenyewe.

Naamini kuwa wanasiasa wataendelea kujifunza kupitia sakata hilo la Lema.
 
kwani kifungo ni kifo?alifungwa mandela nini ajabu?hangaikeni na serikali lenu ambalo limewashinda na kila mfanyabiashara,mfanyakazi,mkulima wamelipa kisogo,swali ni je kama ndoto ya lema ikatimia na lema akiwa bado ndani mtafanya nini?mtu mwenyewe anatafuta mtu wa kufa naye.
 
khaaa..

As if unadhani lema anaogopa jela

Lema isn't a coward

Lema is right and he said the right thing

Weka k umbukumbu zako sawa...sio utamaduni wa Lema kuogopa vitisho na jela zenu.

In fact kwa nchi za kiafrika wanasiasa wa upinzani kuwekwa Jela ni kawaida

Rest assured Lema akitoka huko usidhani kwamba ndio mtakuwa mmemziba mdomo

Lema is fighting against the same dictatorial African Regimes
 
Akili Finyu za Lumumba! Sijui huwa mnawaza nini!... Kwanza, akili zako na wenzenu mnapojikalia hapo na kutoona post za Zitto kwenye mtandao wa Twitter ndo kunawaaminisha kuwa wanamuogopa Rais?

Alafu usituletee story za Kijiweni. Nambie ni nchi gani ambayo ukimzushia Rais Kifo adhabu yake ni Kifo. Uchunguzi lazima ufanye na udhibitishwe na mahakama kwamba mtu tajwa alikua na maana gani katika matamshi yake.

Pengine, Mungu anampigania Lema aendelee kukaa Gerezani ili endapo maono yake yakatimia Lema asihusishwe.
 
Hivi ule utaratibu wa maaskari magereza kuwakagua mahabusu kila wakiingia magerezani bado upo?
Utaratibu ule unadharirisha sana mahabusu na wafungwa,utaratibu mbaya sana, yaani mahabusu anavua nguo anakaguliwa sehemu za haja kubwa ili kukagua kama hajaficha vitu visivyotakiwa kuingia navyo mahabusu kama sigara na bangi,halafu unakuta mahabusu wengine ni waheshimiwa.
 
Kilichokuwa pia kinawapa jeuri ni pesa za walipa kodi walizokuwa wanapata enzi za jk ambazo hazikuwa na kazi..ni aibu kutiwa ndani kwa kumtukana Kiongozi wa nchi ambaye africa na dunia nzima
nzima imemuelewa pamoja na mapungufu machache japo wao upinzani pia walisema wanahitaji wa aina hii..na ndio maana hata Joshua nasari hana muda wa kufika mahakamani..hata msigwa Rafiki yake hajawai hata kugusa huko...jiulize why?? Ni kwamba magufuli ni mpango wa mungu..si kila mpinzani ni boya..wengine ni wazalendo na wamekubali mwelekeo wa nchi kwa 70%..kwao ni bora sasa kuliko huko tulikotoka..japo nao walinufaika
 
Akili Finyu za Lumumba! Sijui huwa mnawaza nini!... Kwanza, akili zako na wenzenu mnapojikalia hapo na kutoona post za Zitto kwenye mtandao wa Twitter ndo kunawaaminisha kuwa wanamuogopa Rais?

Alafu usituletee story za Kijiweni. Nambie ni nchi gani ambayo ukimzushia Rais Kifo adhabu yake ni Kifo. Uchunguzi lazima ufanye na udhibitishwe na mahakama kwamba mtu tajwa alikua na maana gani katika matamshi yake.

Pengine, Mungu anampigania Lema aendelee kukaa Gerezani ili endapo maono yake yakatimia Lema asihusishwe.
Tanzania hatupendagi Ujinga. Lema ni mwanasiasa wa kwanza kutamka maneno ya kijinga na kwa hali hiyo lazima aonje shubiri.
 
Huo ni mtazamo wako.Mbona Marehemu Ditopile aliua dereva wa daladala kwa risasi na alipewa dhamana?.Sisi wananchi tunachoogopa ni mhimili wa mahakama kuingiliwa na mhimili mwingine.Mbona wapo watu wengi magereza wamekosa dhamana na wameendesha kesi zao hadi kushinda? Mazingira ya kesi ya lema ni ya kisiasa hivyo hatushangai acha wenye mamlaka wafurahishe viongozi wao lakini "mkuki kwa nguruwe .,,....
 
Kama tulifanya ujinga hapo awali hatuwezi kuendelea kuufanya sasa
 
Kwani lema kakutwa na lipi???maana dhamana yake ipo wazi kilichopo ni mahakama kutenda.kulingana na maagizo ya.mr malaika.
 
wewe lizaboni mama yako si mwanasiasa pia nahisi atakuwa amejifunza kitu
 
Akili Finyu za Lumumba! Sijui huwa mnawaza nini!... Kwanza, akili zako na wenzenu mnapojikalia hapo na kutoona post za Zitto kwenye mtandao wa Twitter ndo kunawaaminisha kuwa wanamuogopa Rais?

Alafu usituletee story za Kijiweni. Nambie ni nchi gani ambayo ukimzushia Rais Kifo adhabu yake ni Kifo. Uchunguzi lazima ufanye na udhibitishwe na mahakama kwamba mtu tajwa alikua na maana gani katika matamshi yake.

Pengine, Mungu anampigania Lema aendelee kukaa Gerezani ili endapo maono yake yakatimia Lema asihusishwe.
Achana nao hao wamefundishwa English tokea darasa la tatu,Leo hii wanatafuta translator!!
 
Kwani lema kakutwa na lipi???maana dhamana yake ipo wazi kilichopo ni mahakama kutenda.kulingana na maagizo ya.mr malaika.
Bahati nzuri mahakama inatenda ila mawakili wake ni vihio
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom