Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,230
- 6,471
Habari wadau.
Kutoka Kenya ni kuwa vikosi vya polisi na vifaa vyao vimeamuriwa kuondaka uwanja wa Uhuru park na kupisha kuapishwa kwa Raila na Makamu wake. Hapo Jana na Leo asubuhi vikosi mbalimbali vya usalama vilikuwa vimeuzingira uwanja huo.
Hata hivyo kuondolewa kwa vikosi hivyo huenda ni mtego wa kuwafungulia mashitaka ya uhaini watakaoapishwa. Uwanja umefurika wafuasi wa NASA kutoka kote nchini Kenya.Viongozi wakuu wa NASA wameingia ktk kikao cha dharura kabla ya hafla hii ya kuapishwa na haijulikani kikao kitachukua muda gani.
Kutokana na kikao hiki cha mikakati kuibuka, Rais mtarajiwa na Makamu wake bado hawajafika uwanjani.
MREJESHO: Raila odinga ameshakula kiapo na kujitaja yeye ni kama Rais wa wananchi. Amekula kiapo huku akiahidu Makamu wa Rais ataapishwa baadae na kwamba wananchi watajua nini kimetokea kwa Kalozo hadi kushindwa kufika uwanjani. Vigogo wengine wa NASA pia hawakufika uwanjani na kutokufika kwao nitawaletea baadae.
Nitaleta updates mara kwa Mara.