Wakati akijubu hoja mbalimbali za wabunge,mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali,alisoma mapendekezo ya kamati yake kwa bunge ambayo yote yaliridhiwa na bunge na sasa kuwa mapendekezo(maazimio) ya bunge.
Kinachomgusa Pinda ni lile pendekezo linalosomeka "mawaziri wote wa TAMISEMI(huku akimtaja Pinda kwa msisitizo) wajipime,wajitafakari kama wanatosha kuongoza wizara kubwa na nyeti kama TAMIDEMI".Pia,ifahamike kuwa, mwenyekiti huyo baada ya kusoma pendekezo hilo kwa mara ya kwanza alirudia tena kwa kusema na hapa akimtaja waziri mkuu Pinda kwa jina "narudia labda mh.Pinda hakunisikia,mwaziri wote wajipime,wajitafakari kama wanatosha kuendelea kuongoza wizara kubwa na nyeti kama TAMISEMI" ,alisema mwenyekiti huyo wa kamati ya bunge ya LAAC.
Pia,tukumbuke bunge limeridhia mapendekezo yote ikiwa ni pamoja na hilo la kuwataka mawaziri wote wa TAMISEMI kujitafakari.
Sasa mapendekezo haya si ndio kama yale ya kamati ya Mwakyembe kwa aliekuwa waziri mkuu wa wakati huo,mh.Edward Lowassa?
Katika mazingira haya, Pinda na mawaziri wenzake(Hawa Ghasia na Aggrey Mwammry) watapona kweli?
Tusubiri tuone.