Elections 2010 Yanayojiri kwenye kampeni za CCM Mwanza

Ningependa nione na nisikie JK anawaomba wananchi kwa matamshi yake mwenyewe wamchague Andrew Chenge na Basil . Patakuwa patamu hapo
 
kwani serikali ya tanzania unahitaji afya kuiongoza?!

sidhani kama JK huwa anatumia akili wakati akiwa ikulu......................namuona kama ni mtu wa kusaini makaratasi anayopewa bila ya kuzingatia sna ndani kimeandikwa nini.

simlaumu kwa sababu wananchi hatujali either way....:confused2:
 
Tumpe kura za ndiyo,hao chadema wanaanzia kwenye maendeleo ya ccm. Hawana cha kutueleza walichokichangia kwenye kuendeleza jamii zaidi ya kuba documents
Tunawatambua kwa kauli zao. AIBU
 
pumbafu kabisa...hii picha sio ya mwanza na huyo unayesema ana afya kaongea dakika 19 tu jana..hakuna cha maana alichoongea zaidi ya kusema kwake mafanikio ni kuwanunulia wasanii mastering studio ..hahaaaaaaaa..CCM mgombea mnaye mwaka huu
 
Kwan slaa alipoangaka bafuni>?
Kwani kuanguka bafuni ni ugonjwa, hapa tunaongelea afya mgogoro kama ya kikwete mwenye sijui kifafa, hivi wewe ukijikwaa na kuanguka utasema ni ugonjwa? elimu tu inakusumbua.
 
huyu MALARIA SUGU ANAWASUMBUA NA UPUUZI, UIMARA WA AFYA YA MTU HUPIMWA KWA TABASAMU ?
Kikwete kaanguka jukwaani akihutubia, ameanguka kwa maradhi yaleyale ya miaka mitano nyuma, ni maradhi ambayo yanamtesa, yanamfedhehesha, yanamnyima raha, na yanampa unyonge.
POLE JAKAYA KIKWETE, usikubali kutetewa na wapuzi, usikubali maneno maneno. simama Sema unachoumwa, usitoe majibu rahisi kuwa SAUMU Imekukamata, watu wanafunga, wanacheza soka juani kwa dakika 90, na wala huwezi kuona unyonge, sasa Kikwete , anahutubia tu jukwaani, anatudanganya nguvu zinamuisha, mbona Mwinyi alikua anafunga, hatukuwahi kusikia akila mwereka , kuna Lipumba amefunga, anapambana majukwaani bila kudondoka.
Najua JK, mara moja moja anapashwa habari za jukwaani humu, tafadhali, mwambieni ukweli, aseme anachoumwa, kuficha kutamuangamiza zaidi.
pole JK.
 
Unatuwekea picha za maktaba jana hakuvaa suti, angalia picha ya jana anapepesuka
mz6.jpg
 
helo jamani mm nazani huyu rais wetu anafaa kuangaliwa afya yake tena kwa makini zaidi maana inatutia shaka kwamba anamatatizo gani maana kila inapofikia msimu wa kampeni yeye huwa anaanguka tuu je? kuna nini kinachoendelea
 
Anaondoka Jukwaani baada ya kutoa ahadi ya ziada ambayo haipo katika Ilani . . . nadhani ni barabara

Kwanza SUPERMAN nikushukuru sana kwa kuwaupdate wana JF kwa hii post niliyoianzisha. WajanJF wamepata updates ambazo ni za moto moto.
Nilitimkia kwingine si unajua tena mambo ya mjini. Asante sana ndugu. Leo JK yuko wapi vile?
 
Kilimo . . . tutoke jembe la mkono twende kwenye matrekta. serikali imejizuia kununua magari for 2 years. Matrkta 3000 yameagizwa
Na yale ya GX V8 yaliyojaa maofisi ya serikali ni baiskeli zile, na kilimo kwanza au kilio kwanza kwa wakulima? Maana mfuko wa mbolea laki na mifugo ndio kwanza hulisha hayo mashamba ya wakulima kwa rushwa iliyojaa serikalini.Kaka mkuu bado anatusanii tu hamna lolote hapo.
 
lkn ameisha sema kuwa ni swaumu sasa unataka nini

Mwanza imemkubali

Acha uongo,
Jana niliangalia kuanzia alipoongea Katibu wa CCM mkoa Mwanza, Bilali, mpaka Raisi mwenyewe. Ilikuwa aibu tupu. Uwanja ulikuwa zii, utafikiri watu wamemwagiwa maji. Mpaka Pius Msekwa alikuwa anajisikia vihbaya, na mara nyingi alikuwa akijaribu kuanzisha makofi lakini wapi! Ukisema CCM hoyee, watu kimya! unasikia sauti za watu kama 20 hivi walio pale jukwaani.Bilali alijaribu kujitutumua wapi! Uwanja Zii! Kwa kweli CCM pale wameshajua, hawatakiwi. Alipoanza tu JK kuhutubia na takwimu za ajabu ajabu, watu wakaanza kutoka uwanjani.
Pale palijaa wanafunzi na walikuwa bored kichizi........ huu ndio ukweli wa CCM< Kirumba jana.
 
Back
Top Bottom