Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,634
- 870,319
Amos Makala: CHADEMA wanakwenda kuleta virusi vya ebola na M-pox nchiki ili kuangamiza taifa letu.
John Mwakangale: (akiwa kaburini) uli nhaaji!
Jeshi la Polisi: Sisi kazi yetu ni kulinda amani mikutanoni hatuhusiki na siasa za majukwaani.
Tundu Lissu: CCM na Serikali yake wasiposikia na wasipokubali kubadili mifumo ya uchaguzi ili tuwe na Tume Huru ya Uchaguzi na tubadili sheria mbaya za uchaguzi ili tuwe na uchaguzi huru na wa haki; tutakinukisha na pia tutauzuia uchaguzi usifanyike.
Afande IGP: Afande OCD nenda kule Mbinga, Ruvuma kawapige mabomu watu wote hata wanaomsikiliza Lissu kisha ukamkamate huyo Lissu mlete kwa DCI afunguliwe kesi ya uhaini.
Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza: Kama mlimvumilia yule aliyeleta taharuki aliposema CHADEMA wanaleta virusi vya ebola na M-pox, kwa nini msimvumilie na huyu wa kukinukisha?
Kigogo Kigogo: Baba Askofu! Hao wakikujibu, nipo pale nimetulia!
Jakaya Kikwete: (kutulia kimya Msoga) kuwaza jinsi kitabu cha zama hizi kinavyochapishwa. JK ni muumini wa usemi usemao: 'kila kitabu na zama zake'!
Ramadhani Kailima: CHADEMA hawajasaini kanuni za maadili - kwisha habari yao hao!
Godbless Lema: 'Mimi ni mtumishi wa Mungu, mnaiharibu nchi hii'!
Mzee wa Lumumba: Kesi ya CHADEMA na Kesi ya CCM ni mbingu na ardhi, hazifananishwi hata kama Mahakama ni moja na hakimu au jaji ni yule yule!
Mtaa wa Lumumba: Hiena! Hiena!
Mtaa wa Mwembechai: Sisi tunapenda mchuzi wa kasa ingawa nyama yake ina sumu.
Prof. Anna Tibaijuka: Vijana wanapaswa wajue kuwa haki hupiganiwa, haiji kwa silver plate!
Watawa: Subirini ujumbe wetu wa Pasaka!
Binti Mwamakula: (akimuuliza baba yake) Baba, nilipokuwa ziara ya kimasomo niliona kwenye vyombo vya habari kuwa Tundu Lissu kufunguliwa makosa ya uhaini. Kakosa nini?
Askofu Mwamakula: (akimjibu bintiye) Lissu aliwaambia Wamatengo, Wangoni, Wanyasa na Wamanda kuwa tani za makaa ya mawe kutoka Ruvuma zilitosha kuwafanya wao kuwa tajiri!
Binti Mwamakula: (akipigwa butwaa) uxfjkhlyt!
Hii ni tafakuri yangu asubuhi ya leo ili kuondoa stress za mvua huku Mzizima iliyotanda hadi Lango la Jiji. Kama wewe ni Mfipa, achana na tafakuri hii waachie Wapimbwe ndio watu walio na akili ya kuelewa maandishi yatokayo Itunge!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 14 Aprili 2025; saa 4:35 asubuhi