Makangarawe
Senior Member
- Nov 19, 2013
- 101
- 24
Bunge maalum la Katiba leo limepata mgeni kutoka Kenya mh. Amos Wako ambaye alikuwa mwanasheria wa Kenya na alishiriki katika mchakato wa kuandaa katiba.
Lengo la ujio wake ni kutoa fursa kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kujifunza jambo alilolifanya akiwa Mwanasheria wa Kenya aliyeshiriki Mchakato wa Kupata Rasimu ya Katiba ya Nchi hiyo hadi kupatikana kwa Katiba yake.
=== Updates ====
Kikwazo cha lugha aliyotumia Mh. Amos Wako
===
====
Rev. Mtikila naye anena,
Lengo la ujio wake ni kutoa fursa kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kujifunza jambo alilolifanya akiwa Mwanasheria wa Kenya aliyeshiriki Mchakato wa Kupata Rasimu ya Katiba ya Nchi hiyo hadi kupatikana kwa Katiba yake.
=== Updates ====
Kikwazo cha lugha aliyotumia Mh. Amos Wako
Wanajamvi.
Nimefanikiwa kushuhudia asilimia kubwa ya Wabunge wa Bunge la Katiba wakilalamika kuhusu matumizi ya lugha ya kiingereza kwenye uwasilishaji wa Mh. Amos Wacko.
Baada ya kuona ombi lao halikubaliwi kwa kigezo cha kuleta mtiririko mzuri wa kile anachokitoa Mh. Amos Wacko.
Wabunge wameingia mitini kiaina kwa kusinzia ama kutokujitokeza kupeleka majina ya kuomba kuuliza swali. Hadi muda huu ni wabunge kumi tu kati ya mia sita ndo wameomba kuuliza maswali au kuchangia.
Pia kimetolewa kisingizio cha kwa kuwa mjadala unaangaliwa na kusikilizwa na wananchi kupitia vyombo vya habari inabidi tafasiri itumike ili watu wengi waelewe.
Swali langu ni: Mbona kila siku muda wa saa mbili asubuhi TBC1 kituo cha Taifa kinaungana na CCTV na wanatangaza kwa kiingereza? Au matangazo hayo hayatuhusu wabongo?
Pia: Kwani wajumbe walikuwa hawajui kama Mh. Amos Wacko atakuja kushusha nondo kwa lugha ambayo siyo yao?
Mwenye uelewa anisaidie.
===
Nimefurahi kusikia kwamba kutoka kwa Mwanasheria Mstaafu wa Kenya, Amos Wakko kwamba Kenya nafasi nyingi mfano: Katibu Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Jaji Mkuu, Wakuu wa Taasisi zote za Umma, wanaomba ajira kama wafanyakazi wengine wowote wale. Na Interview kwa nafasi muhimu mfano Jaji Mkuu hufanywa kwenye TV Live. Hii ni jambo muhimu sana, tunahitaji kuwa nalo maana rushwa na wizi wa rasilimali utapungua katika Ofisi za Umma. Kila mtu yuko huru kufanya kazi kwa utaalamu bila kuogopa aliyemteua...
====
Rev. Mtikila naye anena,
WanaJF,
Katika hali ya kushangaza bungeni, mch Mtikila ametokea kukurupuka na kuingizia mambo ambayo hayahusiki katika mjadala unao endelea bungeni kwa sasa ambao ni kuhusu semina ya uzoefu wa nchi ya Kenya katika kuandaa katiba yao.
Mchungaji Mtikila bila ya aibu ametokea kuingizia mijadala mingine kabisa ambayo haina mahusiano ya kile ambacho kinajadiliwa bungeni na kupelekea kutokea kwa hali ya taharuki miongoni mwa wajumbe wa bunge maalumu. Jambo ambalo limemdhalilisha sana Mtikila.
Kubwa ambalo Mtikila alikuwa anang'ang'ania ni kupigania Tanganyika bungeni eti akidai kuwa kuna vitisho kutoka kwa mhe Sitta vya kuwashughulikia wale watakao ipigania Tanganyika kama ambavyo Dr Ulimboka, Dr Mvungi na Kibanda walivyo shughulikiwa. Jambo ambalo limepingwa vikali na Mhe Sitta kwa kumwambia yeye kama Mwenyekiti atatumia kanuni za bunge na sio vinginevyo katika kushughulikia hoja.
My take,
Mhe rais Kikwete amefanya makosa sana kuteua watu ambao vichwani mwao haijulikani kama ni wazima ama lah.
Hivi huyu Mtikila anashindwa kuelewa kuwa kuna mjadala wa semina na pia kuna mgeni!? Tanganyika nani anaitaka? Kama sio yeye na CHADEMA tu?