Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,713
Habari wakuu,
Baada ya kusomwa kwa bajeti siku ya Alhamis, leo tunaendelea na Tutaanza na kipindi cha kawaida cha maswali na majibu, baada ya hapo kutakua na hati za kuwasilisha mezani, mwenyekiti wa kamati ya bajeti atawasilisha taarifa ya kamati juu ya hali ya uchumi na mpango wa maendeleo ya taifa 2015/16 pamoja na tathmini ya utekelezaji wa bajeti kwa 2014/15 na mapendekezo ya mapato na matumizi ya serikali 2015/16, msemaji kambi ya upinzani nae atawasilisisha.
=========
Maswali kadhaa yameshaulizwa na kutotolewa majibu na sasa ni uwasilishaji wa taarifa za kamati
Mwenyekiti: Waziri mkuu hayupo bungeni hivyo amemkaimisha mama Mary Nagu kuwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.
Rage: Kwanini kocha asifukuzwe baada ya kufungwa na timu ya taifa ya Misri
Mwenyekiti: Hayo mambo baadae
KAMATI YA KUDUMU-BAJETI
Kamati ya kudumu ya bajeti imeendelea kufanya kazi yake, kamati inatoa salamu za pole kwa wabunge wote kwa kuondokewa na wabunge, kamati imekutana na waziri wa bajeti pamoja na wataalamu na ilitoa mrejesho.
Ukuaji wa pato la taifa umechangiwa na shughuli katika ujenzi, usafirishaji, fedha na bima na biashara ya matengenezo. Shughuli za kilimo zimeendelea kusuasua, takwimu zinaonesha ukuaji wa takribani miaka nane ni asilimia 6.5 na Tanzania ni ya pili baada ya Rwanda.
Takwimu zinaonyesha thamani ya shilingi ilishuka kwa kasi, pamoja na jitihada za serikali kamati inaona inaathiri uchumi wa nchi ikiwemo uagizaji wa bidhaa na mzigo madeni ya nje.
Kamati inashindwa inashangazwa muda wa wiki mbili uliobaki mwaka wa fedha uishe bado serikali inaendelea na majadiliano ya mikopo. Kamati inataka serikali ifanyie kazi kasoro zilizobainishwa na mkaguzi mkuu wa serikali kwa mwaka 2013/14 ambazo hazijafanyiwa kazi.
Deni la taifa limeendelea kukua kwa kuwa na nakisi kwenye bajeti ya serikali na kuilazimu serikali kukopa na deni la ndani linaongezeka kutokana na serikali kutofikia malengo.
KAMBI YA UPINZANI
Esther Matiko: Pamoja na ushauri tuliopatia serikali kwa kipindi chote, kutokana na kiburi cha madaraka haijatimiza(anatolea mifano shauri ambazo serikali haijatimiza ikiwemo ada shule binafsi, viwanja vya michezo vilivyohodhiwa na CCM kurudishwa serikalini).
Marry Nagu: Nasikitika kusema kuwa, sheikh mkuu amefariki katika hospitali ya TMJ Dar es Salaam na utaratibu utatolewa na baraza kuu la waislamu Tanzania.
Mbatia: Bajeti ni nyenzo muhimu ya sera ya maendeleo ya nchi yoyote, serikali hii imeshindwa kutimiza ahadi yake ya maisha bora kwa kila mtanzania. Kutokana na takwimu za BOT thamani ya shilingi inazidi kupungua, thamani ya shilingi moja mwaka jana, leo ni Tshs 1.2, ukosefu wa uwazi na nidhamu ya bajeti ni changamoto, Ni muhimu kutambua sera pekee haziwezi kutimiza malengo.
Zakia Meghji: Nampongeza waziri kwa kazi aliyofanya, si kazi rahisi. Napenda kuzungumzia kuhusu mifuko ya jamii, madeni ya mifuko ya jamii ikiwemo deni la PSPF. Deni hili ni la miaka mingi na kwa taarifa nilizopata, wizara ya fedha iliahidi kulipa Tshs bilioni 4.5, Je, jambo hili limefanyika na kama halijafanyika limefikia kiasi gani na anatuambiaje kuhusu ulipai wa deni hili.
Wakati ule mikopo hii ilikuwa inatolewa kwa utashi wa kisiasa ikiwemo UDOM, bunge hili na machinga complex na tunashukuru sasa imewekewa utaratibu. Baadae yanaweza kutokea matatizo makubwa kwa wastaafu, tunatumai serikali itafanya utaratibu wa kulipa madeni hayo. Kwa mwaka wa fedha 2015/16 kutakua na utaratibu wa kulipa wastaafu Zanzibar, tunatumai na huku bara watafanya utaratibu. Kitu kingine ningependa kuuliza daraja la Kigamboni limefikia wapi? Naunga mkono hoja.
Andrew Chenge: Nipende kwa kuanza naunga mkono hoja kwa niaba ya wananchi wa Bariadi, nitoe pole kwa msiba wa mufti. Niipongeze serikali kupitia wizara ya fedha kwa hoja mbili zilizopo. Ni rahisi sana kutoa maneno matamu ya kukosoa kosoa, maana ya upinzani ni kutoa changamoto kwa upande wa serikali kuongeza ufanisi. Serikali imeanza kuondokana na kuongeza kodi kwa vitu ambavyo vimezoeleka ikiwemo bia na soda, nawapongeza kwa hilo. Tufikirie matumizi ya kawaida ya mwezi ujao yaendane na mapato ya mwezi huu, ndio discipline.
Sekta ambayo imebeba watu wengi Tanzania ni kilimo na wengi ni kipato cha chini na inakuwa kwa 3.4%, tusipojibu changamoto ya sekta ya kilimo, tatizo la umasikini halitaondoka. Sekta binafsi ndio engine ya maendeleo yetu na tuonekane sote tuipende na tuisaidie kuongeza tija na ufanisi. Lugha ya kukataa wawekezaji katika sekta ya kilimo haina mashiko, hawawezi kubeba ardhi waondoke nayo. Mfamo wa kodi sio rafiki kwa mtanzania kulipa kodi nyingi kuliko mgeni.
Mradi wa ubia kati ya sekta binafsi na serikali ndio mafanikio, tubadilishe fikra zetu kwa sekta binafsi, tozo ya miundombinu, shirika la maendeleo ya petroli ndio linashikilia leseni, tukiweza kubuni kama wenzetu inaweza ikatusaidia.
Akunay: Naungana na watanzania kuomboleza kofo cha mufti, naunga mkono hotuba mbili zote za upinzani hasa bajeti mbadala. Umekua mtindo kwa miaka mitano iliopita kwa serikali kuleta bajeti na kusema kwa nini haijatimia. Thamani ya pesa inateremka kwa sababu dola inaongezeka, siafiki kwa sababu kwa muda mrefu thamani ya Kenya inaongezeka kuliko yetu.
Wigo wa kodi unatakiwa uongezeke lakini imeachwa sehemu kubwa 'rental charges'. Serikali inashauriwa ipanue wigo, kuna pesa nyingi sana huko. Serikali inasema uchumi unakuwa kwa 7% lakini wananchi hawajaona mifukoni mwao. Inasemekana bia na soda haikupanda lakini tumeshachaji kwenye usafiri.
Taarifa(Waziri): Tozo hili limetokana na wabunge na kamati, waziri wa fedha ameongeza tozo ya Tshs 50 ili iwe Tshs 100 kupeleka umeme vijijini.
Taarifa sizikubali na tumetoa kodi, wapeleke umeme vijijini. Mwaka juzi serikali ilikubali kuwapa pesa wazee lakini leo wanasema wanafanya utafiti.
Anna Abdallah: Niungane kutoa pole kwa kifo cha mpendwa wetu ambae ni sheikh mkuu, naunga mkono hoja, nakusudia kustaafu shughuli zote za bunge baada ya kuwa humu kwa miaka 40.
Serikali inapoamua kuanzisha eneo la utawala, kwanini hatutengi fedha za ofisi mpya na watu kufanyia kazi ofisi zao za zamani na kuongeza gharama, tulipendekeza posho ya polisi na leo tena wanatuambia mpaka mwakani, hivi 6,000 anakula nini, naomba mtuunge mkono alafu mnasema kamati mtukumbushe mwakani, hii si kazi ya kamati ila ni kazi ya serikali.
Tuna wenyekiti wawili wanawake na spika, ni maendeleo mazuri, tunategemea katiba ndio ina majibu, ninawaomba kina mama wakajisajili ili waipigie kura. Pia katika vyama vya siasa ACT mwenyekiti ni mwanamke, NCCR kina naibu mwanamke na CUF wana naibu katibu mkuu mwanamke. Nawashukuru wanawake waliojitokeza kugombania urais na wanawake wenzenu tupo, tupo wengi mno na nikitoka humu ntaenda kufanya hilo na sio kwa chama, vyama vyote.
Mwenyekiti: Muda wa asubuhi umeisha kwa sababu ratiba yetu imerudi kama zamani na tutarudi kama zamani na niwataji wachangiaji wa mwanzo ili wawahi, Ataanza mheshimiwa Msigwa, Mtanda, Chilolo, Pamba, Mkuya Baruani, Mwanjalwe Sanya, Kadege, Kiwanga, Machali.