Anataka warudi ili baadae aseme walikuepo wakati interahamwe wakijipanga kwa mauaji?Nilikuwa namuona tu mtuta kumbe naye anauwezo wa kujenga hoja nimezipenda sana hoja zake yuko vizuri kujenga hoja zake na kuzielewa ameendelea kusisitiza kuwa katiba inatungwa bungeni siyo mitaani huku akiwataka chadema,cuf, na nccr mageuzi warudi bungeni make katiba haitungwi mitaani.
Nami nakuunga mkono Tetyy ni bora hao wana CCM waliobaki mjengoni wakapitisha hivyo vifungu badala ya kupoteza muda kuwapiga vijembe UKAWA ambao hawapo huko bungeni. Ni upuuzi wa hali ya juu kumsema mtu asiyekuwepo bali tungetegemea wajenge hoja za kuridhisha ili kutetea mfumo wa Serikali 2. Hilo halifanyiki bali ni lugha zile zile zizilizo watoa UKAWA bungeni. CCM hawana hoja za maana ndio maana wanaishia kuongea ujinga mtupu matusi na kejeli kwa wapinzani. Ninawaasa wajue kuwa wakipitisha hivyo vifungu na hio Katiba ya Serikali 2 ni yao wao CCM lakini sisi Watanzania tulio wengi tunasubiri katiba yetu ya Serikali 3 kama ilivyopendekezwa na Tume ya Jaji Warioba. CCM wajue kuwa mabadiliko hayazuiliki ila yanacheleweshwa tu. Wanapigania masilahi yao kwa nguvu zote hata ikiwezekana kwa kuua (ndio maana wanachukia kuitwa Intarahamwe) wala si masilahi ya nchi na kwa ujinga wao huo wajue kila mtu amewajua na hivyo wajiandae kwa mabadiliko na wengine yatawapeleka jela kwa uchafu wao huo.
Ulikuwa humsikilizi
Hivi na ile miwani aliyovaa sijamuelewa? Je mule ukumbini kuna high light intensity?.
Mie nashangaa wanajisifu
kwa heshima na kuwalaumu wengine kwa kuwakashifu viongozi wetu.....Hivi
wenyewe kwa kumkashifu na kumdhihaki Warioba wanaona wako sawa?
Kumdhihaki Warioba ni Kumdhihaki Nyerere....tunaojua tunajua!