Hivi serikali ya Muungano inapata wapi hela sasa hivi na itaacha vipi kuendelea pata hela?
Huyu Dovutwa anapoteza muda tu hana hoja.
Watanzania ktk suala la Uchumi tuko nyuma GDP yetu ni ndogo sana ukilinganisha na Mauritius, Libya,Israel Nchi hizo zinaongozwa na Rais 1 na Waziri Mkuu hatuna ubavu wa kuendesha Serikali 3 kama tutaruhusu ziwepo ujue tutatumia pesa ambayo tungeweza kuwapa wachimba madini mtaji au mama ntilie,pembejeo za kilimo ,mkopo kwa wanavyuo wetu serikali 3 ni mzigo kwetu wananchi.
Kwani CCM hela yote waliyoiba inaweza endesha serikali ngapi?Watanzania ktk suala la Uchumi tuko nyuma GDP yetu ni ndogo sana ukilinganisha na Mauritius, Libya,Israel Nchi hizo zinaongozwa na Rais 1 na Waziri Mkuu hatuna ubavu wa kuendesha Serikali 3 kama tutaruhusu ziwepo ujue tutatumia pesa ambayo tungeweza kuwapa wachimba madini mtaji au mama ntilie,pembejeo za kilimo ,mkopo kwa wanavyuo wetu serikali 3 ni mzigo kwetu wananchi.
Katika majadiliano yanayoendelea inaonekana wazi kwamba wazanzibar sasa wanaamsha hisia za utengano zilizokuwepo zamani. Weusi wamekuwa wanawatukana na kuwabagua wenye asili ya kiarabu kaisi kwamba unashindwa kuelewa muafaka kule zanzibar utabaki kweli baadaya katiba hii? Nimependa mbunge mmoja amemuonya kingwangala aliyesema kwamba katiba hii ikipitishwa itawalazimu zanzibar kubadili katiba yao na kumwambia hizo ni ndoto za mchana na halitokaa litokee zanzibar. Huu ubaguzi wa rangi ambao Sitta amekuwa anaulea bila kuukemea haliwezi kuleta ufa mkubwa zanzibar?
Mbarouk mzima kweli eti anasema mfumo wa serikali mbili utainufaisha Zanzibar itakuwa half london my God! Kwa miaka 50 hamjakuwa half london kwa mfumo huu sasa ndo utawanufaisha? And this and the Rages r the one to decide our fate. R.I.P TANZANIA
Sasa serikali mbili utasemaje hakuna upande ambao haujaweka mamlaka yote kwenye serikali ya muungano? Tanganyika mamlaka yao yanakaa wapi?
Hivi Dodoma kuna baridi kali sana? namuona Mwigulu amejitanda ile mitandio inayovaliwa nchi zenye baridi kali hasa na mashabiki wa mpira.
Ni dhahiri hakuna uwezekano wa kuwa na katiba mpya kutokana na msimamo wa wajumbe wa chama Tawala. HAKUNA MJUMBE ALIYETAYARI KUSHAWISHIKA KWA HOJA YEYOTE KUTOKA UPANDE ASIOUSHABIKIA HATA INGEKUWA BORA NAMNA GANI. Tegemeo la wajumbe kubadili mIsimamo kutokana na ubora wa hoja za mwenye mawazo tofauti halipo kamwe. kukijaribu kulazimisha maamuzi yeyote bila marithiano hatutapata katiba bora. Aidha nakubali kuwa hatua tuliyofikia sasa ya bunge la katiba kujadili rasimu ya katiba iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba ni nzuri. Sasa Rasimu ipo bado kuijadili tu kwa maana ya kuifanyia marekebisho.
Mawazo yangu yananituma kusitisha kazi ya kujadili katiba kwa sasa, na tuende kushughulika na Tume ya uchaguzi pamoja na kuboresha daftari la wapiga kura. Hii nikwasababu yawezekana kukatakiwa kura ya maoni kuhusu muundo wa muungano kabla ya kupigia kura ya maoni ya katiba mpya. Vilevile yawezekana mjadala wa bunge la katiba ukaendelea mpaka baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Yatupasa kukataa kuendelea na mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi uliopo sasa. athari zake tumeziona katika bunge linaloendelea sasa. Tunahitaji tume huru ya uchaguzi na kila raia mwenye sifa ya kupiga kura atumie haki yake ya kupiga kura, hapo ndipo katiba tuitakayo itaweza kupatikana.
Tukikubali kuendeleza marumbano ya mipasho yaliyopo sasa na hatimaye wanaojiita wengi wakafanikiwa kupenyeza serikali zao mbili, hatutokaa tusahau fursa hii maana mabadiliko yeyote yanayofuata yatakuwa na shinikizo kubwa sana ambalo huenda likasababisha muundo mbovu wa muungano na katiba mbovu au hata kuvunja muungano.
Kutokana na mjadala unaoendelea bungeni, nimejifunza kwamba Zanzibar hakuko salama, na waliopendekeza serikali nne huenda wanahoja kwa mazingira yalivyo zanzibar. Wazanzibar hawaaminiani kabisaaaaaa! hivyo huenda serikali ya Pemba, Serikali ya Unguja, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano vikawa ndio suluhisho la migogoro tunayoiona.
Wananchi tuelekeze nguvu zetu katika kuhakikisha tunakuwa na tume huru ya uchaguzi na daftari la wapiga kura linaboreshwa haraka. Tujipange kwa lolote linaloweza kutokea.
Lakini pia nawashauri Ukawa wakati wa kuchangia hoja jiandaeni kwa takwimu na vielelezo:
Mfano: Naunga hoja muundo wa serikali iliyopendekezwa ktk rasimu ya katiba sababu:
1. kuondoa kero : orodhesha kero na njiaambazo serikali mbili zilijaribu kuzitatua na zilishindwa kivipi.
onyesha jinsi serikali tatu itakavyoziondoa
Gharama za uendeshaji wa serikali tatu: orodhesha namba ya wizara zote za sasa, onyesha wizara zitakazo baki ktk serikali ya muungano baada ya kuingia katika serikali tatu, onyesha wizara unodhanina zinafaa kusimamiwa na serikali washirika, hapo sasa onyesha tofauti ya gharama kama utavyoweza kujenga hoja. Onyesha jinsi bunge la muungano litakavyo kuwa dogo na laweza kutumia ukumbi wa karimjee DSM, onyesha jinsi bunge la Tanganyika litavyo kuwa na litakuwa likiendeshwa wapi shughuli zake wapi, bila shaka ni Dodoma Onyesha Kiongozi wa Tanganyika atakapoendeshea shughuli zake kuwa ni ofisi ya sasa ya Waziri mkuu Dodoma. Onyesha Kuwa ofisi ya Raisi wa Muungano iendelee kuwa pale Magogoni, hivyo hoja kuwa hakuna ardhi ya ofisi ya rais wa muungano haipo. Zungumzia suala la Urai mmoja kwa wananchi wote washirika kwamba wote ni raia wa Jamuhuri za Tanganyika na Zanzibar. Onyesha wepesi utakaokuwepo kwa nchi washirika kuhudumia wananchi wake na jinsi serikali ya muungano itakavyowajibika kwa nchi washirika.
Ndugu zangu pambana, hakuna kulala, jini la Katiba limeishachomoka katika chupa, halitarudi mpaka katiba mpya ipatikane.
Bunge la Muungano limefikia hatua ambayo ni ile ama lako au langu.naona tushauri jinsi ya kutoka hapo kwa kuanda katiba ya sote.Naona katiba iwe ya win win kwa kuweka vipengele vifuatavo;usipotoshe. serikali kuu itakuwa ndogo sana kwa hiyo hakuna litakalobadilika.rasimu inaonesha serikali 3 garama zitapungua. na kama utanganyika ni mbaya mbona uzanzibar hamsem ni ubaya una garama?kuweni makini