Yanayo tufanya tuwe waswahili... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanayo tufanya tuwe waswahili...

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Jan 26, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  YANAYO TUFANYA TUWE WASWAHILI...

  1.Unawasalimia watu usiowajuwa na kutaka

  urafiki na kila anayetaka kuzungumza na wewe,

  halafu unaanza kumwita mtu huyo(usiyemjuwa

  undani wake wala tabia zake)aunt au anco!.  2.Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za

  muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original

  copies).  3.Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa

  kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku

  utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.  4.Una machupa ya maji matupu na ya shampoo,

  chupa za perfume pamoja na vipodozi vingine

  umeweka tuu kwenye rafu au meza yako wala

  huna shughuli navyo.  5. Watoto wako wote wana majina ya utani

  mfano babu ali,chidi,mamu, dida, kibabu, n.k.  6. Hakuna mtu katika familia yako anayetoa

  taarifa kwako anapo kuja kukutembelea,

  wanajileta tu, hata hawatazami idadi ya watu

  wanaokuja wala kufikiria watalala wapi!
  7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya

  kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua

  sehemu kama vile mgahawani (Restaurant).  8. Mama yako anamigogoro na ndugu na

  hawazungumzi kwa muda wa siku 10 au zaidi.  9.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao

  gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana

  )na mara nyingi huwa una beep tu hutaki kujitia

  hasara hata kama wewe ndiye uliye na haja

  hiyo.  10.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja

  na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa

  muda mrefu zaidi.  11.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa

  uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa, kwa kuwa

  unataka kumridhisha kila mtu kwa zawadi huko

  unakokwenda.


  12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi

  utakuwa unapita na huku unasema kama sio

  mimi asingekuwa vile yule.


  13. Wale tunaowasaidia wengi wanakosa

  shukurani na badala yake wanasema, eti

  kaniletea kijisimu hiki, si hata hapa ningeweza

  kukipata? Ndio, zawadi ya Ulaya hii?! Halafu

  wanacheka!


  14. Hatuvai nguo nzuri au mpya na kujipamba

  tunapokuwa majumbani mwetu isipokuwa

  tunapokwenda maharusini, khitma au kwenye

  mialiko ya futari au pale tunapoalikwa vyakula

  na marafiki!


  NOTE: Basi wapelekee waswahili wengine ili

  wajuwe ni kitu gani kinawafanya wao wawe

  Waswahili... ......... ......... ..... kama mimi na wewe


  ,
  lakini si wakati umefika wa kubadilisha khulka

  hizi, zilizopitiwa na wakati? (out dated

  traditions and customs)!!?....mmh?  Cheers  |
  .
  [​IMG]
   
 2. NILHAM RASHED

  NILHAM RASHED JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mambo yo ya kwanza mpaka ya mwish ni vichekesho vyote.. hahahahaahha lol... mzizi mkavu....
   
Loading...