Yanayo kufanya uonekane Mswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanayo kufanya uonekane Mswahili

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by MziziMkavu, Oct 15, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  1. Unamwita mtu usiyemjua(wala kukutana nae kabla)aunt au uncle.

  2. Asilimia 90 ya CD pamoja na cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki (sio original copys).

  3. Stoo yako imejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano kapet ukilitoa hulitupi n.k.

  4. Una machupa matupu ya maji, shampoo, perfum pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo.


  5. 5. Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali,chidi
  mamu,dida n.k.


  6 . Hakuna mtu katika familia yako anaetoa taarifa kwako anapo kuja kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k.


  7. Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mikahawani.


  8. Mama yako wanamigogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa siku 10 au zaidi.


  9. Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana)na mara nyingi huwa una beep tu10.

  10 Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.


  11. Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa.

  12. Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi itakua unasema kama sio mie asingekuwa vile yule.
   
 2. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  hii tayari ilikwishatumwa hapa mkuu, tena ilikua kule kwenye jokes nenda kachek kule utaikuta
   
Loading...