Yamenikuta, uchawi kweli upo

Yamenikuta, uchawi kweli upo

Unachuma dhambi bure tatizo si uchawi.Kwa Tanzania baadhi ya maeneo huwa yanapata umeme mdogo sana ikifika wakati wa jioni kwa sababu matumizi ya umeme yanaongezeka.Kwa mfano mimi ninapokaa ikifika wakati wa jioni 'voltage' huwa inasoma 150 badala ya 220-250 na hii inasababisha baadhi ya vifaa vya umeme kushindwa kufanya kazi na utatuzi wa tatizo hili ni Tanesco kufunga transformer. Vilevile hata jenerata uliloweka inawezekana lilikuwa halitoi umeme unaotosheleza kuwasha firiji.
Inawezekana tatizo la jamaa limeanza kutokea baada ya huyo mfanyabiashara mwenzie kuwa ndio atakuwa kaongeza matumizi ya umeme?
 
Maisha ni vita! Anaingia panya mmoja anatoboa (zile juice kubwa) zote matundu madogo kiasi cha kuziharibu. Unanunua gunia la mchele kesho unakuta wadudu wa ajabu. Yapo mengi unayofanyiwa kishirikina. Pole! Hapo Kawe ni penyewe. Kuna usemi "kaa Kawe ukawie " Usikate tamaa name tupia vya kwako mpaka akome!
 
Nilifungua biashara ya chakula mbali kidogo na ninapo ishi. Miezi minne ya kwanza biashara ilikuwa ikienda vizuri, hivyo nikajiwekea mipango kadhaa ya kupanua biashara yangu.

Baada ya miezi kama sita hivi akaja mama mmoja kufungua biashara jirani na kwangu, yani frem ya pembeni yangu kabisa. Tukaanza kugawana wateja, hivyo biashara ikawa inasua sua si kama mwanzo.

Baada kama ya miezi miwili toka yule mama afike kila nikifika asubuhi nakuta friji imejizima; vyakula vimeharika, juisi na maziwa vimeharibika pia.

Ile friji nilinunua mpya kabisa, ilibidi nimuite fundi aikague lakini akasema ipo sawa. Cha ajabu, kuanzia asubuhi mpaka jioni tunapokuwepo tukiwasha friji haijizimi, nikasema tujaribu tusiwashe siku nzima kisha usiku tu ndio iwake lakini bado tukirudi friji imezima na vitu vimeharibika.

Kwa bahati mbaya si kil ulichopika watu watanunua na kitaisha, hivyo ilibidi nibadilishe friji lakini hali ikawa ile ile. Nikaweka jenereta lakini wapi

Kipindi hicho wateja sipati kabisa mpaka nikaamua kufunga ile biashara.

Wewe mama wa kimakonde ulichonifanya pale Kawe sokoni sitakusahau, SITAKUSAHAU MILELE.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nichek pm naweza kukusaidia ,umesema upo kawe soko jipya ,we nichek bila kujal
 
Inawezekana kbs alikua anapandajuu ya dari anadisconect...kwanini usifikirie na Hilo pia?
 
Uchawi unatokana na fikra zako mwenyewe jinsi unavyo waza. Kabla hata ya friji kuanza kukusumbua ulishajijengea dhana potofu kua kuna mama anakuchukulia wateja kimazingara

Hivyo kwa dhana hiyo ukajikuta unafanya vitu bila kutafakari mara mbili kwasababu kila jambo ambalo kwako hulielewi ulilihesabu kama ni sehemu ya kurogwa

Majibu ya fundi hayatoshi kuhitimisha kua friji limerogwa. Kwanini hukufikiria kua fundi pengine hana taaluma nzuri yakutosha kuweza kubaini tatizo??

Au fundi hana vifaa vya kisasa vitavyoweza kupima tatizo la hiyo friji?

Mara ngapi hata madaktari ukienda hospitalini unaumwa lakini ukipimwa wanasema hakuna ugonjwa halafu ukienda sehemu nyingine unaambiwa aina ya ugonjwa unao kusumbua?

Kama madaktari wanakosea sembuse fundi friji ndo umuamini kua hakosei na majibu yake aliyokupa ni sahihi?

Nakuhakikishia ukiendelea ku concentrate na dhana ya "kurogwa" utapoteza umakini hadi kufikia hatua unawazidishia watu chenchi na katika hesabu zako utakuta hasara then uanze fitina kua yule mama kaanza kukuwekea chuma ulete

Kuna njia nyingi za kiushindani katika biashara na namna ya kumshawishi mteja. Unaweza ukawa na mtaji mkubwa lakini ukikosa baadhi ya vigezo utasema umerogwa. Na wale ambao utawaona wamefanikiwa utawaita wachawi kitu ambacho sio kweli

Hakuna uchawi kijana, huyo mama angekua mchawi na kwanamna ambavyo tumekua tukisikia sifa zake, huyo mama asingekuja hapo kufungua duka. Angeweza kupiga bingo za maana akiwa amelala tu kwake halafu tungemuona hapa kwenye top 3 ya mabilionea

Naunga hoja
 
Ni rshisi kukataa uchawi,unajua uchawi ni kama hisia au mawazo ya mtu yanayomsukuma kufanya jambo fulani. Unaweza kuona mtu akikuonesha hali ya kukujari ila usiweze kujua kilichojificha kwamba kinachomsukuma kufanya hivyo ni hisia za upendo au ana mawazo yenye nia hovu mbeleni. Sasa uchawi ndio uko hivyo kwamba unaweza kufanya itokee ajali na hiyo ajali ikaelezeka kabisa imetokeaje na chanzo ni nini ila kumbe sababu hasa ni ule uchawi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom