Yamenikuta, uchawi kweli upo

Yamenikuta, uchawi kweli upo

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,533
Reaction score
3,837
Nilifungua biashara ya chakula mbali kidogo na ninapo ishi. Miezi minne ya kwanza biashara ilikuwa ikienda vizuri, hivyo nikajiwekea mipango kadhaa ya kupanua biashara yangu.

Baada ya miezi kama sita hivi akaja mama mmoja kufungua biashara jirani na kwangu, yani frem ya pembeni yangu kabisa. Tukaanza kugawana wateja, hivyo biashara ikawa inasua sua si kama mwanzo.

Baada kama ya miezi miwili toka yule mama afike kila nikifika asubuhi nakuta friji imejizima; vyakula vimeharika, juisi na maziwa vimeharibika pia.

Ile friji nilinunua mpya kabisa, ilibidi nimuite fundi aikague lakini akasema ipo sawa. Cha ajabu, kuanzia asubuhi mpaka jioni tunapokuwepo tukiwasha friji haijizimi, nikasema tujaribu tusiwashe siku nzima kisha usiku tu ndio iwake lakini bado tukirudi friji imezima na vitu vimeharibika.

Kwa bahati mbaya si kil ulichopika watu watanunua na kitaisha, hivyo ilibidi nibadilishe friji lakini hali ikawa ile ile. Nikaweka jenereta lakini wapi

Kipindi hicho wateja sipati kabisa mpaka nikaamua kufunga ile biashara.

Wewe mama wa kimakonde ulichonifanya pale Kawe sokoni sitakusahau, SITAKUSAHAU MILELE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah pole sana muathirika kwa hali iliyokukuta.
Swali la kukuuliza: Umejuaje kuwa jirani yako (huyo mama wa kimakonde) anahusika kwa kufirisika na kufunga biashara yako?
 
Ndio dunia ya leo hii..uchawi upo..ni mwendo wa ndumba kwenda mbele..yaani shiriki imekua fashion.. hatari sana.
 
Uchawi unatokana na fikra zako mwenyewe jinsi unavyo waza. Kabla hata ya friji kuanza kukusumbua ulishajijengea dhana potofu kua kuna mama anakuchukulia wateja kimazingara

Hivyo kwa dhana hiyo ukajikuta unafanya vitu bila kutafakari mara mbili kwasababu kila jambo ambalo kwako hulielewi ulilihesabu kama ni sehemu ya kurogwa

Majibu ya fundi hayatoshi kuhitimisha kua friji limerogwa. Kwanini hukufikiria kua fundi pengine hana taaluma nzuri yakutosha kuweza kubaini tatizo??

Au fundi hana vifaa vya kisasa vitavyoweza kupima tatizo la hiyo friji?

Mara ngapi hata madaktari ukienda hospitalini unaumwa lakini ukipimwa wanasema hakuna ugonjwa halafu ukienda sehemu nyingine unaambiwa aina ya ugonjwa unao kusumbua?

Kama madaktari wanakosea sembuse fundi friji ndo umuamini kua hakosei na majibu yake aliyokupa ni sahihi?

Nakuhakikishia ukiendelea ku concentrate na dhana ya "kurogwa" utapoteza umakini hadi kufikia hatua unawazidishia watu chenchi na katika hesabu zako utakuta hasara then uanze fitina kua yule mama kaanza kukuwekea chuma ulete

Kuna njia nyingi za kiushindani katika biashara na namna ya kumshawishi mteja. Unaweza ukawa na mtaji mkubwa lakini ukikosa baadhi ya vigezo utasema umerogwa. Na wale ambao utawaona wamefanikiwa utawaita wachawi kitu ambacho sio kweli

Hakuna uchawi kijana, huyo mama angekua mchawi na kwanamna ambavyo tumekua tukisikia sifa zake, huyo mama asingekuja hapo kufungua duka. Angeweza kupiga bingo za maana akiwa amelala tu kwake halafu tungemuona hapa kwenye top 3 ya mabilionea
 
Uchawi wa kuroga umeme 😂😂.. siku moja ungefanya ukalala ndani ya mgahawa wako ukaona hio fridge inakuwaje
 
Nilifungua biashara ya chakula mbali kidogo na ninapo ishi. Miezi minne ya kwanza biashara ilikuwa ikienda vizuri, hivyo nikajiwekea mipango kadhaa ya kupanua biashara yangu.

Baada ya miezi kama sita hivi akaja mama mmoja kufungua biashara jirani na kwangu, yani frem ya pembeni yangu kabisa. Tukaanza kugawana wateja, hivyo biashara ikawa inasua sua si kama mwanzo.

Baada kama ya miezi miwili toka yule mama afike kila nikifika asubuhi nakuta friji imejizima; vyakula vimeharika, juisi na maziwa vimeharibika pia.

Ile friji nilinunua mpya kabisa, ilibidi nimuite fundi aikague lakini akasema ipo sawa. Cha ajabu, kuanzia asubuhi mpaka jioni tunapokuwepo tukiwasha friji haijizimi, nikasema tujaribu tusiwashe siku nzima kisha usiku tu ndio iwake lakini bado tukirudi friji imezima na vitu vimeharibika.

Kwa bahati mbaya si kil ulichopika watu watanunua na kitaisha, hivyo ilibidi nibadilishe friji lakini hali ikawa ile ile. Nikaweka jenereta lakini wapi

Kipindi hicho wateja sipati kabisa mpaka nikaamua kufunga ile biashara.

Wewe mama wa kimakonde ulichonifanya pale Kawe sokoni sitakusahau, SITAKUSAHAU MILELE.

Sent using Jamii Forums mobile app
HIII N IMANI TU
YAANI UKO PEMBENI KWA MWAMPOSA UNALALAMIKA

WATU WANATOKA GNGOLAMBOTO WANAMWAGIA MAJI NA MAFUTA OFISINI
WACHAWI WANAKUJA ULIZA UNAUZAA EEH HONGERA TENA UKIWAONA UNAMIMINA MAJIYA BARAKA YAUPAKO AWAKANYAGI NGO USIKATE TAMAA NA YA DUNIA
 
Ila ndugu yangu uchawi haupo. Ni wewe tu umekata tamaa mapema. Halafu hujazungumzia ubora wa huduma yako, inawezekana hapo ndo umepigiwa bao wewe unadhani ni uchawi
 
Ngoja nimsikilize mkufunzi na DK wa HESHIMA wa HAYA mambo mshanajr
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom