Kabla na baada ya tukio la kutekwa na kujeruhiwa vibaya kwa Dr.Ulimboka, hapo usiku wa kuamkia June 27 mwaka huu na hata baada ya tukio hilo, tuliweza kusikia matamko na kauli mbalimbali kutoka katika makundi na watu tofauti, kama vile, viongozi wa serikali, dini,vyama vya siasa, wanasiasa,n.k akiwemo Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova. Jambo ambalo halipingiki ni kuwa mbali na tukio la Dr.Ulimboka na hata kabla ya tukio hilo, Kamanda wa Kanda (Dar) ndg. Suleiman Kova alikuwa akisikika sana katika vyombo vya habari, akiwa anatoa taarifa mbalimbali za hali ya usalama katika eneo lake la kazi, ingawa tukio la Dr.Ulimboka lilimfanya Kamanda Kova kuwa maarufu (afahamike)zaidi ya alivyokuwa hapo awali.
Ila ni kipindi kirefu sasa, kamanda huyu amekuwa kimya sana, haonekani na wala hasikiki kwenye vyombo vya habari kama ilivyokuwa kawaida yake? Je ni mambo gani yamempata Kamanda Kova, amekwenda masomoni kuongeza ujuzi? Anaumwa? (ninampa pole), Amestaafu? yupo likizo amesafiri? amehamishwa? ama cheo chake kimefutwa?Tafadhali mwenye habari na Kamanda wetu atujuze.