Kuna kila dalili mama hatagombea 2025. Inavyoonekana kuna vita kubwa sana ambayo hatuifahamu. President and CiC kutoa kauli zile inaonekana kuna watu wanamtesa sana. Imagine gazeti lake la chama kaliita "vijigazeti". Yaani anatuambia kuwa gazeti lake la chama linampiga vita!Makubwa. Secondly, mama anasema hakujawahi kupatikana Rais Mwanamke.
Sijui yeye ni nani?Kudra za Mungu ni kwa sasa. 2025 zitakuwa kudra za nani?vilevile mama anasema wanawake wenzangu!Sijui nani anamdanganya mama. Wanaume wakiamua jambo lao ni hatari zaidi. Wanaume wanaweza kufanya chochote. Kuwagawa watu na kuwabagua wanaume ni kosa kubwa siyo tu kisiasa lakini pia ki-usalama.
Kuna watu wanamharibia mama. Saluti anazopigiwa na wanaume zinapigwa kwa amiri jeshi na siyo rais was wanawake. Amiri jeshi akionyesha udhaifu mkubwa kiasi hicho, basi ujue kilio chake kinafurahisha wabaya wake.
Nilimshauri kuwa JK atampoteza. Toka JK ametoka madarakani, nchi imebadilika sana kiintelijensia. Hii ni nchi na siyo NGO. Mama kuna muda anatuangusha sana.