MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 713
- 1,136
Habari waungwana wa jukwaa hili la Great Thinkers? Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mwaka 2015 Burundi iliingia kwenye fujo za uchaguzi baada ya aliyekiwa rais wakati huo hayati Nkurunziza kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu mfululizo.
Ikukumbwe kuwa rais Nkurunziza alipata urais kwa mara ya kwanza kupitia Bunge la Burundi baada ya Mkataba wa Arusha wa kurejesha amani nchini Burundi baada ya chana CNND kupitia uasi kuishinda serikali ya Burundi ya wakati huo.
Kuanzia hapo Nkurunziza akawa rais wa mpiti mpaka uchaguzi mwingine wa mwaka 2010 ambapo chama cha Nkurunziza cha CNND kilipata ushindi mkubwa sana baada ya wapinzani wa Burundi hasa Rwasa na wenzie kusisia uchaguzi ule.
Lakini cha kushangaza tena mwaka 2015 Nkurunziza alichukua form tena ya kugombea urais huku Warundi wakiingia mitaaani kwa maandamano ya kupinga kitendo hicho wakisema kinavunja katiba ya Burundi kwa rais kuongoza mihula mitatu. Lakini Nkurunziza akajitetea kuwa urais wa mara ya kwanza ulikuwa wa KUDRA maana hakuchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura.
Sasa hapa Tanzania naona kama mazingira ya Burundi yamehamia hapa kwa maana kuwa rais Samia Suluhu Hassan amekuwa rais kwa KUDRA za Mungu baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli.
Kwa mujibu wa hotuba yake ya Jana ya tarehe 15/September 2021 amesema mwaka 2025 rais anaweza kuwa mwanamke kwa maana pengine CCM itamsimamisha yeye.
Je, kama atashinda uchaguzi huo wa 2025 na kusimama tena mwaka 2030 katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho yake yote imesemama chochote kwa mazingira hayo? Na kama haijasema hatuoni kama itakuwa ndio mwanzo wa mgogoro wa kikatiba kama ilivyotokea Burundi mwaka 2015?