Yaliyotokea Burundi 2015 yanaweza kutokea Tanzania 2025?

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
696
1,000
Habari waungwana wa jukwaa hili la Great Thinkers? Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mwaka 2015 Burundi iliingia kwenye fujo za uchaguzi baada ya aliyekiwa rais wakati huo hayati Nkurunziza kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu mfululizo.

Ikukumbwe kuwa rais Nkurunziza alipata urais kwa mara ya kwanza kupitia Bunge la Burundi baada ya Mkataba wa Arusha wa kurejesha amani nchini Burundi baada ya chana CNND kupitia uasi kuishinda serikali ya Burundi ya wakati huo.

Kuanzia hapo Nkurunziza akawa rais wa mpiti mpaka uchaguzi mwingine wa mwaka 2010 ambapo chama cha Nkurunziza cha CNND kilipata ushindi mkubwa sana baada ya wapinzani wa Burundi hasa Rwasa na wenzie kusisia uchaguzi ule.

Lakini cha kushangaza tena mwaka 2015 Nkurunziza alichukua form tena ya kugombea urais huku Warundi wakiingia mitaaani kwa maandamano ya kupinga kitendo hicho wakisema kinavunja katiba ya Burundi kwa rais kuongoza mihula mitatu. Lakini Nkurunziza akajitetea kuwa urais wa mara ya kwanza ulikuwa wa KUDRA maana hakuchaguliwa na wananchi kupitia sanduku la kura.

Sasa hapa Tanzania naona kama mazingira ya Burundi yamehamia hapa kwa maana kuwa rais Samia Suluhu Hassan amekuwa rais kwa KUDRA za Mungu baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli.

Kwa mujibu wa hotuba yake ya Jana ya tarehe 15/September 2021 amesema mwaka 2025 rais anaweza kuwa mwanamke kwa maana pengine CCM itamsimamisha yeye.

Je, kama atashinda uchaguzi huo wa 2025 na kusimama tena mwaka 2030 katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho yake yote imesemama chochote kwa mazingira hayo? Na kama haijasema hatuoni kama itakuwa ndio mwanzo wa mgogoro wa kikatiba kama ilivyotokea Burundi mwaka 2015?
 

Man Mvua

JF-Expert Member
Apr 12, 2016
2,053
2,000
Mkuu bado tupo 2021 wewe umefikaje 2030 ??

Au umepaa kama Mama wako aliyefika 2025 ??

KESHO NI YA MUNGU PEKEE ( sio kesho tu yaani dakika yako 1 ijayo HUIJUI so tulia tuu)
 

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
3,223
2,000
Sijui kiti Cha urais kina matatizo gani, nimpongeze Sana Rais wa ZAMBIA , kuachia kile kiti KWa amani na UTULIVU, kile kiti hasa Afrika akishaingia mtu hunogewa Sana ,
 

Fatma-Zehra

Senior Member
Oct 18, 2020
193
1,000
Kuna kila dalili mama hatagombea 2025. Inavyoonekana kuna vita kubwa sana ambayo hatuifahamu. President and CiC kutoa kauli zile inaonekana kuna watu wanamtesa sana. Imagine gazeti lake la chama kaliita "vijigazeti". Yaani anatuambia kuwa gazeti lake la chama linampiga vita!Makubwa. Secondly, mama anasema hakujawahi kupatikana Rais Mwanamke.

Sijui yeye ni nani?Kudra za Mungu ni kwa sasa. 2025 zitakuwa kudra za nani?vilevile mama anasema wanawake wenzangu!Sijui nani anamdanganya mama. Wanaume wakiamua jambo lao ni hatari zaidi. Wanaume wanaweza kufanya chochote. Kuwagawa watu na kuwabagua wanaume ni kosa kubwa siyo tu kisiasa lakini pia ki-usalama.

Kuna watu wanamharibia mama. Saluti anazopigiwa na wanaume zinapigwa kwa amiri jeshi na siyo rais was wanawake. Amiri jeshi akionyesha udhaifu mkubwa kiasi hicho, basi ujue kilio chake kinafurahisha wabaya wake.

Nilimshauri kuwa JK atampoteza. Toka JK ametoka madarakani, nchi imebadilika sana kiintelijensia. Hii ni nchi na siyo NGO. Mama kuna muda anatuangusha sana.
 

RAISI AJAYE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,754
2,000
Sijajua kwanini mama ametamka mapema haya!kaanza kampeni mapema mno!tena sana!!!kaamsha kambi zote zianze mambo yao!!!!Labda kama ana zuga kama kweli ni hatari sana!labda kama wanamuandaa Riz one au makamba kuchukua kiti kwa mgongo wa mama!!!!
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
8,548
2,000
Yeye anakamilisha muhula wake wa awamu ya tano 2025, maana waliomba ridhaa kwa pamoja na magu....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom