Yaliyonishangaza Dar es Salaam!

Yaliyonishangaza Dar es Salaam!

Nkuruvi

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
624
Reaction score
649
Habarini za jioni wadau!

Nilitoka kwenye jiji hili la Dar Es Salaam takribani miaka 15 iliyopita. Nimewasili hapa takribani kama wiki moja iliyopita na sasa ninaleta kwenu wadau uzoefu wangu mpya katika jiji hili kubwa kabisa nchini na lenye umaarufu Afrika nzima.

  1. Dar Es Salaam kuna wanao-ishi na kuna ambao wanasindikiza wenzao kuishi
Kuingia kwangu hapa mjini nimekaa Manzese, Mwananyamala na Baadae Kinondoni, aisee katika jiji hili kuna watu wanaishi kama Paradiso.

Nimeona watu wanakula bata utadhani wanaishi kwenye nchi tajiri ambapo kila kitu kipo sawa. Hakuna tofauti Weekend na siku za katikati ya wiki. Watu wanaendesha magari makali ya pesa mingi sana na wakiingia sheli ni full tank wakati sisi wengine hata pikipiki hatupigi full tank kwa jinsi mafuta yalivyopanda bei!

Hili nimeliona kwa jamaa yangu ambaye nilikuwa na appointment ya kukutana nae kikazi. Nimefika kwake Tegeta, Dah jamaa anamiliki Mansion! Upande wa pili, nimemtembelea jamaa yangu mwingine tulieachana nae muda mrefu, nikasikitika sana.

Maisha ni duni, chumba kimoja kina kimejaa full. Yaani kuna kitanda, kabati la nguo na vyombo, Ndoo za maji, anapikia humo humo, viatu vimo humo chumbani yaani ni full mchanganyiko, Baba na Mama wanalala na watoto hapo hapo.

Dah, tofauti ya maisha ni kubwa sana nikilinganisha hawa jamaa zangu wawili. Kweli kuna wanaoishi Dar Es Salaam na wengine wanawasindikiza wengine kuishi!

2. Kuna maeneo Dar es Salaam maadili ni F kabisa.
Yaani watu wanatukana mtaani na watoto wanasikia. Biashara ya Ngono ni kubwa sana, nimeona hapa Tiptop na Sinza. Aisee, nyuchi zinauzwa kama nyanya sokoni.

Ni kama watu hawana taarifa za maradhi ya ngono. Binafsi sitamani kumlea mwanangu kwenye jiji hili. Vitoto vidogo vimejiingiza kwenye ukahaba.

Mwananyamala, asubuhi nakutana na mwanamke amelewa chakari amevaa chupi tu, amelala Bar na jamaa wako pembeni wanajisifia wamemla mande matundu yote mawili. Hapo kuna watoto wanasikia hayo yote.

3. Utapeli ni mkubwa sana
Nimefika Karume kununua viatu, jamaa wameniuzia raba feki 30,000.00. Nyie wafanyabiashara wa Karume, ndo maana hilo soko linaunguaungua kila mwaka, mmejaa laana za utapeli. Yaani raba wameziosha vizuri zinang’aa kumbe chini soli imeisha kabisa.

Yaani wameunganisha vipande kwa gundi. Nimefika home, kufua na kuvaa nashangaa soli yote imenyofoka. Hovyo kabisa.

Haya wa mikoani wenzangu ongezeeni uzoefu mpya mnaokutana nao katika jiji hili!
 
Inategemea na tabia zako mfano Mimi naishi Temeke hila sijawaiga kukutana na Dada poa aliyevaa chupi. So Mkuu acha kutembelea madanguro

Then huyo jamaa anakaa one room usiseme anasindikiza wakati huko Bukoba watu wanalala kwenye nyumba za tope na zimeezekwa na makuti ya mawese
 
Dar Kama huna kazi utaishia kua mwizi, kibaka na tapeli tu. Huko hakuna Cha kula kwa ndugu, Kama ukienda kwa ndugu unakaribishwa nje na glass ya maji.

Hapo storry zitapigwa mpaka uondoke, na watu wa mikoani hawawezi elewa acha wazidi kwenda Dar kutafuta Maisha.
 
Inategemea na tabia zako mfano Mimi naishi Temeke hila sijawaiga kukutana na Dada poa aliyevaa chupi
So Mkuu acha kutembelea madanguro

Then huyo jamaa anakaa one room usiseme anasindikiza wakati huko Bukoba watu wanalala kwenye nyumba za tope na zimeezekwa na makuti ya mawese
Mkuu mi sio wa kutembelea madanguro, haya ninayoeleza nimekutana nayo mtaani sehemu za makazi ya watu
 
Dar Kama huna kazi utaishia kua mwizi, kibaka na tapeli tu. Huko hakuna Cha kula kwa ndugu, Kama ukienda kwa ndugu unakaribishwa nje na glass ya maji. Apo storry zitapigwa mpaka uondoke, na watu wa mikoani hawawezi elewa acha wazidi kwenda Dar kutafuta Maisha.
Kweli kabisa
 
Dah! najiuliza huo muda wa kufuatilia yote hayo na kuyaandika huyo jamaa wako wa mwenye maisha ya kitajiri ameutumia kufanya nini...
 
Wiki ijayo narudi zangu bushi, maisha ya mji huu yamenishinda
Acha umbea Hata huko mikoani watu wanafanyana mchana kweupeee wanakulana mande hivi…….DSM ni km mji mwingine tuu!! waweza pata mali au usipate chochote!!…..usitudanganye!!
 
Back
Top Bottom