Yaliyonipata nimeamini mke wa mtu ni sumu

Yaliyonipata nimeamini mke wa mtu ni sumu

Hebu malizia story buana mpakwa mafuta hahahahhaa
 
Daah pole mkuu kjj yaani wewe ni majanga mpaka unakufa,sema big up mwanaume rijali humkuta hayo huvaa ujasiri na kuingia hata kwenye kichaka cha miba usirudi nyuma
 
Aanhaa,,
Aseeeh Kile kipande ulichokiruka ,,,ungekiweka kwa story yako ndiyo ingenoga zaid[emoji12] [emoji12]
 
unawezaje kulala kwenye nyumba usiyoijua? bora hata ungekutwa guest..
 
Mkuu kisa hiki kilikutokea kweli au ni stori ya kufikirika?
kitunda iliwahi tokea hii story 2016 kijana mwanafunzi wa cbe alichofanywa sijuh kama uume wake upo active mungu atusaidie tamaa mbaya
 
Amani kwenu wadau

Jamani mpaka muda huu naandika habari hii ndio nimetoka hospital binafsi nilipokuwa nimepumzishwa nikitibiwa majeraha yaliotokana na kipigo kikali ambacho sikuwahi kukipata tangu kuzaliwa

Labda niwape kisa chenyewe mimi nilikutana na mwanamke mmoja nikamtongoza tukakubaliana,tukabadilishana namba,jioni baada ya kumaliza makusanyo ya pesa zangu kutoka kwa madalali wa mazao,na kumkabidhi mtu mwenye duka ambae nachukua bidhaa za kwenda nazo mkoani


Nikaona ni wakati muafaka wa kumpigia yule mwanamke,akanielekeza nikaona mwanaume wa mkoani nisijishushe nikachukua bajaji mpaka eneo la tukio,nikamjulisha nimewasili akaniambia geuka nyuma yako,

Tukaingia ndani ya ile nyumba macho yakakagua haraka nikajiridhisha hakuna mashaka,fasta nikampigia simu mamsapu kuwa kidogo biashara itachelewa,ili nipate muda wa siku mbili tatu nitumbue kwenye lile kasri,

Wakati tumekaa nikamdadisi yeye kumiliki lile jumba akanitoa wasiwasi kuwa hakuna tatizo wala mwanaume atakae nisumbua,

Nikapewa maji nikaoga,nikaingia chumbani nikampiga kimoko cha nguvu,wakati tumepumzika akaniambia yaani nyie wanaume wa mikoani kiboko yaani hii shughuli uliyonipigisha hapa ni dakika chache lakini umenichamua kila kona,hawa wetu wa jiji la bashite waliozoea pizza ,chips mayai wala hawaiwezi,

Nikamwambia ile ni trailer ngoja mvua ya mawe itakunyeshea nikapanda kwa mara nyingine duu katikati ya mtanange nikasikia mlango unagongwa,nikaendelea na pinda mgongo,mlango ukagongwa kwa mara nyingine ikiambatana na sauti,nikamuona yule mwanamke amefadhaika na ametulia,akaniambia vaa mume wangu,akapaza sauti yule mwanamke subiri navaa eeh jamaa akauliza unaogopa nini kutoka hivyo ulivyo wakati mimi ni mumeo

yule mwanamke akafungua mlango akili ya haraka ni kumvamia na ndoo yule mwenye mali kweli akili ilifanikiwa nikamwangusha nikatoka mbio yule bwana nae akatoka mbio akipiga kelele ya mwizi nikaona sasa kila nikikimbia nguvu zinaniishia na kile kiboksa nilichobaki nacho ni aibu nikaanguka kwa kuishiwa pumzi,

baada ya hapo kipigo haikielezeki nasikia,utakoma kutongoza mke wa mwanajeshi,mara mwingine haa mama lenarld amefanya jambo la aibu kituko hiki cha nini mwanaume ata havutii,wengine eehe labda akibadili gia hakanyagi klachi mmh lakini huyo mkaka kama dume la nyani

wengine mpake mafuta aliwe mtandao mara nasikia kuna gari limefika na watu wanakimbizana na nasikia hiro rigoni riko wapi,nikainuliwa nasikia yaani wew rijamaa unachukua mke wa poti,sikujibu nikapitishwa kituoni wakanihoji na kuniandikia,nikawaomba wanipeleke hospital binafsi,walikuwa waungwana wakakubali ombi langu

huko kitunda sijui nini kilimkuta yule mwanamke,jamani mke wa mtu ni sumu msiwasogelee na nyinyi wanawake muwe wakweli kuliko kudanganya kuwa huna mume kumbe yupo
Pole mkuu ila huna kosa
 
Kumbe ht marinda bado unayo!endelea tu kuna tunu kubwa zaid ya hiyo nayo ni kutolewa marinda yote..
 
Hivi iimichezo bado IPO huwa siiamini kbs
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom